Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Mkuu umelaza hela Sana!!! Kwahyo hela na faida unayotarajia yaani hata haviendani!!
Boss hii 70m nikipata Mimi nitatuta coster mbili!!
Kila siku nalaza hamsini kwa kila moja
2@50,000/= 100,000/=
Kwamwezi zifanye kazi siku 26
100,000 x 26 =2,600,000 kwa mwezi
2,600,000 x 12 = 31,200,000/= kwa mwaka
31,200,000 x 3 =93,600,000/= kwa miaka mitatu
Hapa unakuwa umerudisha mtaji unaanza kula faida!!!
Mkuu ukipata zingine tumia na hii njia!!
Biashara za makaratasi hizi.

Acha kuishi kwa maisha ya kufikirika.
 
Kwenye real estate mimi huwa nasema Location ya nyumba yako ndio kila kitu. Kuna ndugu amejenga very nice modern family house in Chanika anapata shida kupata mpangaji wa kumpa 150,000 kwa mwezi. Lakini ndugu mwingine kajenga nyumba kama iyo tegeta masite anakula 600,000 kwa mwezi. Yaani nyumba haipitishi mwezi bila mpangaji.
On another note. Kuwekeza kwenye nyumba za kupangisha sio kitu kibaya hasa kwa watu wanaotafuta hela ya kula tu na kutunza pesa zao kwa usalama Lakini pia wafanya biashara wanaweza tumia hati kukopa bank. Mimi najua biashara za purukushani siwezi Kwaiyo ni bora nijenge nyumba za kupangisha na ninahakikisha najenga location zinazoeleweka.

Kwa mfano Dodoma ni mji unaokuwa kwa kasi, so ujanja ni kununua viwanja location nzuri na vilivyopimwa then unajenga vi appartment.

Pia kama una mtaji wa kutosha nunua mashamba nje ya mji lakini hakikisha huduma zipo karibu then pima viwanja uuze.
 
Kama anapata kodi nzuri inawezekana kabisa

Mimi hapa ndio plan yangu na nimeshajenga na ina wapangaji tayaru yote na mwaka huu nakula kwanza kodi kidogo

Mwakani naanza rooms zangu hapo hapo za self eneo ambalo zinaweza toka rooms 7 bei ya chini ni 90k per room.

Na zitajengwa kwa mixing ya ile ya kwanza na salary yangu
Hivi kipi bora na chenye faida zaidi,kujenga self au sebule na self??
 
Sasa kiwanja kinachopatikana kwa 3m kama ni Dar si anapata bagamoyo hiyo au kisarawe ndani ndani au karibu na mkuranga huko?? Sasa akijenga nyumba huko kodi si itakuwa 50k kwa mwezi na pengine pia asipate mtu wa kumpangisha. Elewa kwamba watu wanapenda kupanga karibu na mjini ambapo kwa mawazo yako kama unataka anunue kiwanja...ni bei kubwa.
Hii biashara huwa inachangamoto zake, na mara nyingi hela uliyoiwekeza huwa hairudi; ndio maana kuna baadhi ya hotel huwa zinachakaa, ingawa zinaingiza hela kila siku. Vinginevyo, ajikite kwenye uuzaji wa viwanja; ananunua pori, anaboresha kwa kuweka viwanja, na hatimaye kuuza.
 
Real Estate inaweza kuwa;

1. Kuwa na shamba, ukakodisha watu walime. Au ulime mwenyewe.

2. Kununua nyumba mbovu, unaimodify then unaiuza kwa bei ya juu.

3. Kununua nyumba, unajenga nyumba unai-list kwenye airbnb

4. Kununua kiwanja unajenga nyumba unakodisha kwa wapangaji.

5. Kununua viwanja, unapima then unauza.

6. Una kiwanja, wekezaji anakuja kujenga juu yake anakuwa anakupa commission ya mapato yake.

7. Una kiwanja, unajenga hoteli/ lodge/ guest house.

N.k
 
Huyo yupo hapa kupewa moyo kama ilivyo kwenye makundi ya WhatsApp.
Na hayupo tayari kuusema wala kuusikiliza ukweli na uhalisia.
Uhalisia naohitaji ni kama vile unaenda kupambana na mtu mwenye bastola ila umepewa mkuki na mshale , utaanza kulia na kulalamika kwamba umeshashindwa vita sababu hauna bastola kama unayeenda kupigana naye, ?
 
Mimi nimejenga nyumba bila hata kupiga hesabu,nina nyumba ina sebule tu kubwa,vyumba viwili kimoja master,jiko,public toilet..na veranda mbili.

Means gharama itakuwa imefikia huko kwenye mil 70.
Hongera mkuu atleast umeitumia kuwekeza kwenye kitu na kinaonekana, muhim kujua utaongeza vipi investment nyingine kwa kutumia ulivyonavyo.
 
Kwenye real estate mimi huwa nasema Location ya nyumba yako ndio kila kitu. Kuna ndugu amejenga very nice modern family house in Chanika anapata shida kupata mpangaji wa kumpa 150,000 kwa mwezi. Lakini ndugu mwingine kajenga nyumba kama iyo tegeta masite anakula 600,000 kwa mwezi. Yaani nyumba haipitishi mwezi bila mpangaji.
On another note. Kuwekeza kwenye nyumba za kupangisha sio kitu kibaya hasa kwa watu wanaotafuta hela ya kula tu na kutunza pesa zao kwa usalama Lakini pia wafanya biashara wanaweza tumia hati kukopa bank. Mimi najua biashara za purukushani siwezi Kwaiyo ni bora nijenge nyumba za kupangisha na ninahakikisha najenga location zinazoeleweka.

Kwa mfano Dodoma ni mji unaokuwa kwa kasi, so ujanja ni kununua viwanja location nzuri na vilivyopimwa then unajenga vi appartment.

Pia kama una mtaji wa kutosha nunua mashamba nje ya mji lakini hakikisha huduma zipo karibu then pima viwanja uuze.
Maelezo mazuri barikiwa mrembo, nimeokota kitu.
 
Hii biashara ni nzuri sana kama utakuwa na uvumilivu, na pia isiwe ni biashara ambayo unaitegemea sana yaani uwe na biashara nyingine pembeni, ngoja niangalie filamu ya mama alafu nitarudi hapa na maoni kwa kirefu zaidi

[emoji23][emoji23][emoji23] dah!
 
Kwenye real estate mimi huwa nasema Location ya nyumba yako ndio kila kitu. Kuna ndugu amejenga very nice modern family house in Chanika anapata shida kupata mpangaji wa kumpa 150,000 kwa mwezi. Lakini ndugu mwingine kajenga nyumba kama iyo tegeta masite anakula 600,000 kwa mwezi. Yaani nyumba haipitishi mwezi bila mpangaji.
On another note. Kuwekeza kwenye nyumba za kupangisha sio kitu kibaya hasa kwa watu wanaotafuta hela ya kula tu na kutunza pesa zao kwa usalama Lakini pia wafanya biashara wanaweza tumia hati kukopa bank. Mimi najua biashara za purukushani siwezi Kwaiyo ni bora nijenge nyumba za kupangisha na ninahakikisha najenga location zinazoeleweka.

Kwa mfano Dodoma ni mji unaokuwa kwa kasi, so ujanja ni kununua viwanja location nzuri na vilivyopimwa then unajenga vi appartment.

Pia kama una mtaji wa kutosha nunua mashamba nje ya mji lakini hakikisha huduma zipo karibu then pima viwanja uuze.
Kwenye location ni mchezo wa bahati nasibu mixer kamari!!
Hii inayoitwa Masaki leo hapo zamani ilikuwa ni mawe tupu , ujenzi wake ulikuwa mgumu na yalikuwa maeneo ya kuchimba kokoto miaka hiyo ya 80 , waliojenga pale walikuwa wanaonekana hqwapo sawa kichwani , ila ndo hivo , paka hit jackpot, , story ni hizo hizo kwa tegeta , bunju ,.nk
Kujenga sehemu , halafu paje kuwa Hot, ni swala la bahati , sio mkakati
 
Hehe, unalazimisha mfano ambao haufanani.
Interest rate ya Tanzania ni 15%, kwa hiyo kama umeweka investment ambayo haikuingizii faida ya aslimia 15 ya mtaji wako kwa mwaka, au angalau asilimia 10 basi bora uziweke hela benki.
Wewe unaingiza less than 3% kwa mwaka. Anza upya ili ujenge nyumba ya kupangisha, siyo ya kuishi watu.
Yaani, anza upya.
Bora umemuwekea kwenye mahesabu ya kibenki ataelewa
 
Kwenye location ni mchezo wa bahati nasibu mixer kamari!!
Hii inayoitwa Masaki leo hapo zamani ilikuwa ni mawe tupu , ujenzi wake ulikuwa mgumu na yalikuwa maeneo ya kuchimba kokoto miaka hiyo ya 80 , waliojenga pale walikuwa wanaonekana hqwapo sawa kichwani , ila ndo hivo , paka hit jackpot, , story ni hizo hizo kwa tegeta , bunju ,.nk
Kujenga sehemu , halafu paje kuwa Hot, ni swala la bahati , sio mkakati
Naomba kupishana na wewe kidogo. Mfano it is a common knowledge kwa sasa maeneo ya mwelekeo wa bagamoyo na karibu na beach ni hot cake. So kama unaweza nunua shamba maeneo ya bagamoyo kwa sasa, trust me lazima itakuja kukulipa tu. Kitu kingine angalia kama maeneo yaliyo karibu na hapo yamepimwa, kawaida maeneo yaliyopimwa yana attract middle and upper class of people. Na kwa DSM bado maeneo yaliyopimwa ni machache ukilinganisha na ambayo hayajapatiwa.
 
Beach plots nyingi (hadi third row) ni mahotel, arts galleries. Ukinunua bei ni kubwa, halafu itabidi ufanye amendment na planners wa ardhi wanataka pesa ndefu. Sasa hivi hazikamatiki, hata Buyuni, Pemba mnazi, mti mweupe beach plots hazikamatiki, GSM kakamata karibu zote na ni hotel sites.
Biashara ya real estate imekaa kimwinyi sana, simshauri mtu aweke mshahara au pensheni yake kwenye real estate. Ila kiukweli ukipata mashamba sehemu nzuri unaweza kula pesa ndefu.
 
Back
Top Bottom