Wazo zuri...Mimi kwenye hizo ngazi ulizoweka naangukia kwenye hilo kundi la wadogo.
USHAURI:
*Kwa kuanza lazima uwe na shughuli nyingine sambamba hadi hapo utakapoimarika..Fedha inayopatikana hapa kiuchumi inaitwa passive income..inapatikana kidogo kidogo.
- Hujasema uko wapi lakini nakushauri ujenge kwa kuzingatia mtindo wa maisha ya sasa..watu hawakai na familia kubwa kwa muda mrefu..watoto wanasoma shule za bweni hivyo vyumba viwili na ukumbi tosha sana.
- Angalia Mji uliopo kwa mfano Dodoma wafanyakazi wengi wako bado na familia zao Dar na maeneo mengine .hivyo rudia ujenzi niliokueleza hapo juu..vyumba viwili toshaa kwa maana ukubwa wa familia ni mdogo.
- Watu hawataki shida ya kuchangia vitu .hivyo ingia gharama za kila mpangaji kujitegemea kwenye huduma za maji,umeme nk
*Kuwa mbunifu kwenye ujenzi wa majengo yako na eneo ulilokuwa nalo..acha kujenga vyumba vikuubwa ambavyo vitakuchua eneo kubwa.
* Kuwa na mpango mzuri wa ujenzi .mfano eneo lako linatosha kujenga majengo manne..Anza kwanza na moja likamilishe hadi liishe na lianze kutoa huduma halafu fedha kidogo utakazokuwa unapata endelezea ujenzi wa sehemu inayofuatia .hapa wapo ambao wanaanzisha ujenzi wa majengo yote kwenye eneo na kuishia njiani kwa Fedha kwisha.
*Hakikisha eneo linakuwa na faragha na usalama kwa kujenga uzio ..
Kwa Leo hayo yanatosha kwa kuanzia.
Land Lord.