Naomba tuongee UHALISIA kuhusu biashara ya Real Estate kutumia mfano HAI

Thanks mkuu.
 
Mkuu Bavaria wewe ndio umetoa uchanganuzi mzuri katika huu uzi tena kwa ufupi zaidi[emoji119][emoji119][emoji120]!
 
Huwa biashara ya real estate watu wanazani ni kuuza Viwanja na Kupangisha nyumba lakini sio hivyo tu.
Real estate imegawanyika katika sehem mbalimbali kama vile Valuation, Property Management, Investment and finance analysis na Agency services.
Agency services ndio inahusisha kuuza na kupangisha Viwanja,nyumba,vyumba na apartments, hii unaweza ukafanya tuu ikaanzia locally au ukasajili kampuni kabisa.
Valuation ni uthamini hii ili ufanye lazima uwe umesomea na degree yake inatolewa pale Ardhi University inaitwa Bsc Land Management and Valuation nanusajiliwe na body ya wathamini.
Property Management inahusisha usimamizi wa majengo baada ya kujenga mwenye nyumba anakukabidhi wewe kama manager unakua unatafta wapangaji, unasimamia operation ya jengo nankumiusanyia Kodi anakualipa kiasi flani.Pia inahusisha na facilities management ambazo zipo kwenye jengo.Pia hii unaweza ukafanya lakini itakua vizuri ukiajiri wataalam waliosomea degree ya Property and Facilities Management pale Ardhi University.
Investment and Finance analysis unakua mshauri watu wanataka kununua nyumba Viwanja au kujenga. Kwa mfano mtu anataka ajenge nyumba na arudishe hela yake ndani ya miakakumi ajenge wapi na nyumba ya aina gani na ajengeje.Huwa hii ukifatilia kuhusu real estate unaeza ukafanya au uwatumie wataalam waliosomea Real estate, Investment and Finance pale Ardhi University.
Real estate developers kazi yao ni kujenga na kupangisha au kuuza.
 
What you think is really becomes your reality,. Kila mmoja na imani yake. Kwenye kila utakachokiamini basi utaletewa njia za kukupeleka huko kwenye hiyo imani yako. Ukiamini kwamba Real Estate investment hailipi uko sawa na atakayeamin Real estate inalipa naye yuko sawa. Kila mmoja atapata mifano ya imani yake
 
Haya majibu uliyatoaga kwa ujasiri utadhani ni kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…