MamboyaMaggy
New Member
- Aug 11, 2026
- 1
- 4
🚨 NAOMBA UFAFANUZI: HII NI HAKI KWELI?
Nimeamua kuandika hili kwa sababu naamini kuna watu wengi wanaweza kuwa wamepitia hali kama yangu bila kujua cha kufanya.
Nilienda kuomba mkopo benki, nikafanyiwa CRB check na nikakuta nina deni la Songesha. Nilipoanza kufuatilia, nikagundua kwamba deni hilo lilitokana na namba ya simu niliyomsajilia mtu mwingine, ambaye alikopa kupitia Songesha na hakulipa kwa takribani mwaka mzima.
Kwa kuwa taarifa ilikuwa imeingia kwenye jina langu, ilibidi mimi nilipie deni hilo la takribani TSh 15,000 ili kulisafisha. Baada ya kulipa, nilipewa clearance letter kama uthibitisho kwamba deni limelipwa.
Nikarudi benki nikiwa na clearance letter nikitarajia kwamba sasa suala limeisha.
Lakini nikaambiwa bado siwezi kupewa mkopo kwa sababu nina historia mbaya CRB, kwa sababu nilichelewa kulipa deni hilo kwa muda mrefu. Hata kama sasa nimeshalipa.
🤔 HAPA NDIPO NINAPOJIULIZA: HII NI HAKI KWELI?
Kama deni limeshalipwa, nina clearance letter na sina deni lolote ambalo sijalipa, kwa nini bado nichukuliwe kama mtu ambaye ni hatari kukopesheka?
Na zaidi ya hapo, deni lenyewe halikuwa la matumizi yangu lilitokana na mtu mwingine ambaye nilimsajilia namba yangu.
Kama kweli hii inatokana na sheria/taratibu za Bank of Tanzania (BOT), naomba mwenye uelewa anieleze:
👉 Je, mtu akilipa deni lake, taarifa ya CRB inapaswa kubaki na historia ya kuchelewa kulipa? Na nikweli ni mpaka miaka 6 ipite ndio jina linasafishwa?
👉 Je, benki zinaweza kumkatalia mtu mkopo kwa sababu ya historia hiyo hata kama deni limeshalipwa?
👉 Kuna muda maalum ambao mtu anatakiwa kusubiri baada ya kulipa deni kabla ya kuweza kupata mkopo tena?
👉 Na kwa mtu ambaye deni lilihusishwa na namba yake lakini hakutumia yeye, anawezaje kurekebisha taarifa hiyo kwenye CRB?
Kwa kweli hii imenifanya nijiulize: Mfumo huu unamlinda nani? Kama mtu ameshalipa deni na kusafisha jina lake, je, ni sahihi kuendelea kumzuia kupata huduma za kifedha?
Naomba BOT, CRB, wataalamu wa sheria za benki, au mtu yeyote mwenye uelewa wa hili atoe ufafanuzi.
Sio suala la TSh 15,000 tu. Ni suala la jinsi taarifa ya CRB inavyoweza kumuathiri mtu hata baada ya deni kulipwa.
📌 Naomba majibu yenye ushahidi/utaratibu rasmi kama yapo, ili wengine wenye changamoto kama hii wajue hatua sahihi za kuchukua.