Mkuu tafadhali naomba uchambuzi wako kwenye hizi simu mbili Xiaomi Mi 8 na Xiaomi Mi 11 Lite 5G
Xiaomi Mi 8 ni flagship ya 2018, Xiaomi Mi 11 Lite 5G ni midrange ya 2021. Kuna midrange nyingi za miaka ya karibuni zina nguvu kuliko flagship za 2018 na Xiaomi Mi 11 Lite 5G ni mfano wa hizo midrange.
Hizi simu hazipaswi kufananishwa kwa sababu Mi 11 Lite 5G ipo vizuri karibia kila kona.
1. Xiaomi Mi 11 Lite 5G Ina IP53 rating kwa hiyo ni splash resistance hiyo Mi 8 haina IP53 rating.
2. Kioo cha Mi 11 Lite 5G kina refresh rate ya 90Hz, cha Mi 8 kina 60Hz refresh rate
3. Xiaomi Mi 11 Lite 5G inatunza chaji kwa 19% zaidi ya Xiaomi Mi 8.
4. Display ya Xiaomi Mi 11 Lite 5G inafikia brightness ya 802nits ambayo ni asilimia 28 zaidi ya Xiaomi Mi 8 yenye 627nits.
5. Xiaomi Mi 11 Lite 5G inatumia Bluetooth version 5.2 wakati Xiaomi Mi 8 inatumia Bluetooth version 5.0
6. Kwenye performance Mi 11 Lite 5G ina uwezo mkubwa kwa 28% zaidi ya Xiaomi Mi 8 according to AnTuTu score (522000 vs 415000)
7. Chipset ya Qualcomm Snapdragon 778G ya kwenye Xiaomi Mi 11 Lite ina ulaji mzuri wa chaji kuliko Qualcomm Snapdragon 845 ya kwenye Xiaomi Mi 8.
8. Xiaomi Mi 11 Lite 5G inasupport HDR 10+, Xiaomi Mi 8 inaishia HDR 10 tu.
9. Xiaomi Mi 11 Lite 5G ina fingerprint scanner pembeni wakati Xiaomi Mi 8 ina fingerprint scanner nyuma ya simu
10. Xiaomi Mi 11 Lite ina sehemu ya kuwekea Memory Card hadi 1TB, Xiaomi Mi 8 haina.
11. Storage type ya Xiaomi Mi 11 Lite 5G ni UFS 2.2 ambayo ni faster kuliko ya kwenye Xiaomi Mi 8 ambayo ni UFS 2.1
12. Android 8.1 ya kwenye Xiaomi Mi 8 ni outdated kuliko Android 11 ya kwenye Xiaomi Mi 11 Lite, bila kusahau MIUI version.
13. 33W charger ya kwenye Xiaomi Mi 11 Lite 5G inachaji faster (1hr 4min) kuliko 18W ya Xiaomi Mi 8 (1hr 35min)
9. Xiaomi Mi 11 Lite 5G ina stereo speakers, Xiaomi Mi 8 ina Mono speaker.
10. Xiaomi Mi 11 Lite 5G inasupport 5G, Mi 8 haina 5G
Kitu kikubwa ambacho Xiaomi Mi 8 anamzidi Mi 11 Lite 5G ni camera tena in reality tofauti ni ndogo sana.
SUMMARY
Display- Mshindi ni Xiaomi Mi 11 Lite 5G
Battery- Mshindi ni Xiaomi Mi 11 Lite 5G
Performance- Mshindi ni Xiaomi Mi 11 Lite 5G
Camera- Mshindi ni Xiaomi Mi 8
Kiufupi Xiaomi Mi 11 Lite 5G ni nzuri kuliko Xiaomi Mi 8.