1kush africa
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 9,552
- 13,090
Uko sahihi,Kitu kingine ninachotaka kukuambia ni kwamba user reviews nyingi ni feki. Siku hizi gsmarena watu wanatumia majina tofauti tofauti kuponda simu wanazozichukia.
Hata mimi nimecomment kwenye simu tofauti kwa majina tofauti tofauti kwa simu ambazo hata sijawahi kuzitumia.
*Mfano mzuri kuna jamaa gsmarena anaitwa "Sin" huyu kazi yake ni kuingia kwenye kila simu ya Xiaomi na kusingizia kuwa amewahi kuitumia na akawa disappointed nayo.
*Kuna mwingine anajiita "you have to suffer" Huyu kazi yake ni kuponda kila simu ya Samsung na kusema kuwa ni simu mbaya, pia anaingia kwenye simu za Xiaomi na anazisifia hizo Xiaomi bila sababu ya msingi.
Kwa kutumia akili akili ndogo tu, binadamu wa kawaida asingebaki kwenye brand ileile kama kila simu anayoitumia kutoka kampuni hiyo ilimdissapoint, kuna sehemu hadi watu walimwambia ukweli kuhusu tabia yake.
- Kuna mmoja pia anaitwa Hanif Fikri, yeye ni fan wa Samsung na Xiaomi tu, na anacomment kwenye simu kadhaa za hizi kampuni mbili akidai amezitumia.
- Kuna mmoja nimemsahau jina, yeye kila simu ya Xiaomi anaiponda na anadai kuwa ameanza kumiliki Xiaomi miaka mingi na hadi leo anatumia Xiaomi ila kila Xiaomi aliyoitumia basi inamdisappoint kwenye same issues.
Mfano mwingine ingia kwenye page ya gsmarena ya Samsung Galaxy S23 Ultra, usome user reviews uone jinsi watu wanavyoponda na wengine wanatetea, hakuna ukweli wala uwazi wowote ule kupitia user reviews. Ninakesha sana gsmarena kusoma user reviews za simu hususani Samsung na Xiaomi hadi nimeanza kukariri watu na tabia zao, ndio maana na mimi nikaamua kujoin system.
Ukiingia YouTube nako, user reviews nyingi ni za kusifia tu, mpaka kero.
IN SHORT, SIKU HIZI SIAMINI USER REVIEWS.
Mie nimetokea tu kupenda sony xperia, sio kwamba ni simu bora kuliko zingine ila ndo nimejikuta napenda tu, ukiniuliza nn hasa napenda kwa sony ntakujibu nazipenda tu,
Samsung wako poa
Iphone wako poa
Na brand zingine ziko poa,
Kikubwa tumia simu upendayo full stop.