Naomba ufafanuzi kuhusu hii biashara ya maudhui mtandaoni

Last_Born

Member
Joined
Dec 9, 2022
Posts
69
Reaction score
100
Je, inawezekana kuanzisha na kuendesha biashara ya maudhui mtandaoni kama blogging au YouTube kama kina Millard Ayo, bila ada za awali (license fee) ? Kama vile mambo ya lecense za TCRA sijui BRELA, then nikaja kulipa baadae

Ikiwa kuna gharama, ni zipi zinaweza kulipwa baadaye baada ya kupata mapato? Nataka kuelewa mbinu bora za kuanza biashara kabla sijaingia kichwa kichwa
 
Kuanza kuzalisha au kufanya kazi za maudhui ya mtandaoni ni hatua nzuri, hasa kwa sababu ya fursa kubwa ya kufikia watu wengi kupitia majukwaa ya kidijitali. Unaweza kuanza bila hata kusajili mpaka pale ambapo utapoanza kupata faida kwa namna fulani.

Lakini pia kusajili ni muhimu hii inakusaidia ki usalama ya maudhui yako. So kwa bongo wengi wananzisha bila kusajili


Lakini kwa blog ili iende vizuri kuna vigharama kidogo vya awali vya kulipia
 
Vigharama kidogo kwenye blog Unamaanisha nin 🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…