Naomba ufafanuzi kuhusu sheria mpya

Naomba ufafanuzi kuhusu sheria mpya

Mzee makoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
3,482
Reaction score
4,673
wiki hii kuna miswada imepelekwa bungeni kufanyiwa marekebisho, ikiwemo sheria ya kwamba polisi hawaruhusiwi kumpeleka mtu mahakaman had wakamilishe upelelezi.

Je na ile sheria inayowapa nguvu upande wa mashtaka na police kumkamata mtu pindi mahakama inapomuachia baada yakukaa ndani muda mrefu, na upande wa mashtaka hawaleti shaidi, au hawakamilishi upelelezi,

Je, hiyo sheria ya mtuhumiwa kukamatwa baada ya kuachiwa na mahakama, nayo ilifanyiwa amendment au? Hii Nchi Ina sheria za hovyo sana
 
Kama ushahidi wameshaupata ndio wanaweza kukumata na kesho yake kukupeleka Mahakamani.
Pia usisahau hiyo sheria haijafuta mahabusu za Polisi. So polisi wanaweza kikushikilia katika mahabusu Hizo kwa muda. Though it is legally improper
 
Naomba kujua , hii sheria ina tekelezwa kwa hawa mahabusu wa baada ya sheria kupita au hata wale walio kamatwa tangu januari na wako mahabusu naupelelezi unaendelea , je hii sheria si inaruhusu hawa mahabusu watolewe kwa dhamana mpaka upelelezi utakapo kamilika ?? maana kuna ndugu yangu ana miezi mitatu tangu aweke mahabusu kila siku upelelezi hauja kamilika anafikishwa mahamani na kuto ruhusiwa kujibu kitu anarudishw mahabusu, eti upelelezi hauja kamilika.

Je hii sheria hairuhusu hawa kutolewa wakae nje kwa dhamana mpaka upelelezi utakapo kamilika?
 
Back
Top Bottom