#COVID19 Naomba ufafanuzi kutokana na hali ya Covid 19 nchini Ujerumani

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Jana tarehe 7.4. 2021, Radio DW iliutangazia ulimwengu kwamba Ujerumani imepata maambukizi mapya ya Corona kwa kiwango kikubwa sana na wanajiandaa kusitisha baadhi ya shughuli ili kujikinga na maambukizi.

Kutokana na taarifa hiyo, naomba mnisaidie kujibu maswali haya:

(1) Je, Ujerumani haijapata chanjo ya Corona?

(2) Kama wamepata chanjo, kwa nini maambukizi yanazidi kuongezeka?

(3) Kama hawajapata chanjo, kwa nini hawajapata?

Ahsante, ndugu zanguni.
 
Jana tarehe 7.4.2021,Radio DW iliutangazia ulimwengu kwamba Ujerumani imepata maambukizi mapya ya Corona kwa kiwango kikubwa sana na wanajiandaa kusitisha baadhi ya shughuli ili kujikinga na maambukizi....
Ujerumani Imepitisha Chanjo nne (4) kutumika nchini mwao Astrazeneca, Pfizer, Moderna na Johnson & Johnson Vaccines.

Uwiano wa Ugawaji chanjo nchini Ujerumani ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine za ulaya, Mathalani mpaka Aprili 6, 2021 ni watu takriban Milioni 10 tu wamepewa walau chanjo moja ya Covid19 ambao ni sawa na asilimia 13% ya Wajerumani Milioni 83 (kwa takwimu za mwaka 2019), huku asilimia 5.6% tu wakiwa wamepewa 'full dose'.

Hiki ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi nyingine kama Israel ambayo imetoa dozi walau moja kwa asilimia 58% ya watu wake, Uingereza imetoa asilimia 47% kwa watu wake, Chile asilimia 37% ikifuatiwa na Marekani ikiwachanja asilimia 33% ya watu wake.

Hata hivyo hatua zinazochukuliwa Ujerumani si kali kama kwingineko, Pichani ni miongoni mwa hatua zilizotangazwa januari mwaka huu kuzuia Usambaaji zaidi wa Covid19.

56193824_7.png
 
Jana tarehe 7.4.2021,Radio DW iliutangazia ulimwengu kwamba Ujerumani imepata maambukizi mapya ya Corona kwa kiwango kikubwa sana na wanajiandaa kusitisha baadhi ya shughuli ili kujikinga na maambukizi...
kuna species zaidi ya 100 za corona na bado wanaweza kubadilika watakavyo

Chanjo iliandaliwa kwa specie gani? tatizo linaanzia hapa
 
Ujerumani Imepitisha Chanjo nne (4) kutumika nchini mwao Astrazeneca, Pfizer, Moderna na Johnson & Johnson Vaccines.

Uwiano wa Ugawaji chanjo nchini Ujerumani ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine za ulaya, Mathalani mpaka Aprili 6, 2021 ni watu takriban Milioni 10 tu wamepewa walau chanjo moja ya Covid19 ambao ni sawa na asilimia 13% ya Wajerumani Milioni 83 (kwa takwimu za mwaka 2019), huku asilimia 5.6% tu wakiwa wamepewa 'full dose'...
Safi kabisa hivi ndivyo JF ilipaswa kuwa yaani FACTS FACTS FACTS sio assumptions na ujuaji.
 
Jana tarehe 7.4.2021,Radio DW iliutangazia ulimwengu kwamba Ujerumani imepata maambukizi mapya ya Corona kwa kiwango kikubwa sana na wanajiandaa kusitisha baadhi ya shughuli ili kujikinga na maambukizi...
Waambie waombe Mungu, korona itapotea. Mungu oyeee
 
Ujerumani Imepitisha Chanjo nne (4) kutumika nchini mwao Astrazeneca, Pfizer, Moderna na Johnson & Johnson Vaccines.

Uwiano wa Ugawaji chanjo nchini Ujerumani ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine za ulaya, Mathalani mpaka Aprili 6, 2021 ni watu takriban Milioni 10 tu wamepewa walau chanjo moja ya Covid19 ambao ni sawa na asilimia 13% ya Wajerumani Milioni 83 (kwa takwimu za mwaka 2019), huku asilimia 5.6% tu wakiwa wamepewa 'full dose'.

Hiki ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi nyingine kama Israel ambayo imetoa dozi walau moja kwa asilimia 58% ya watu wake, Uingereza imetoa asilimia 47% kwa watu wake, Chile asilimia 37% ikifuatiwa na Marekani ikiwachanja asilimia 33% ya watu wake.

Hata hivyo hatua zinazochukuliwa Ujerumani si kali kama kwingineko, Pichani ni miongoni mwa hatua zilizotangazwa januari mwaka huu kuzuia Usambaaji zaidi wa Covid19.

View attachment 1747052
Kwani nchi gani mkuu ambayo kwa asilimia kubwa watu wake wamepewa full dose ya chanjo ya corona?
 
Ni nchi kama Israel, ambayo kufikia Aprili 7, 2021 angalau 54% ya watu wake (watu milioni 4.8) wamepewa 'full dose'

Huku Chile ni 22% ya watu wake (sawa na watu Milioni 4.2) 'full dose'

Na Marekani ni asilimia 19% (sawa na watu milioni 64) 'full dose'.
 
Wameji-rock down mwaka mzima tunaenda wa pili, wanavaa barakoa mbili kwa mpigo, wanazo chanjo said ya aina tatu (Johnson& Johnson walikosea wakachanganya chanjo ya covid na powder ya watoto lol!) Wanapesa, Wana huduma madhubuti za kijamii na hasa afya ila bado covid inawapukutisha bado waafrika hamjiulizi kuwa mbinu zao sio sahihi na kuona umuhimu wa kuja na mbinu zetu?

Nifollow hapa hapa JF nitakuja na mbinu effective ya kujikinga na virusi hivi na vile vitakavyokuja kwa 99%. Sijawahi kuandika utani hapa JF!
 
Nashukuru kwa kushiriki katika mjadala. Niliona nilete hii mada ili kwa pamoja tuweze kuona kama kweli sisi watanzania tunahitaji kupata chanjo hizo kwa sasa wakati wenye uwezo wa kila aina wameshindwa kwa kiasi hicho.
 
Wameji-rock down mwaka mzima tunaenda wa pili, wanavaa barakoa mbili kwa mpigo, wanazo chanjo said ya aina tatu (Johnson& Johnson walikosea wakachanganya chanjo ya covid na powder ya watoto lol!) Wanapesa, Wana huduma madhubuti za kijamii na hasa afya ila bado covid inawapukutisha bado waafrika hamjiulizi kuwa mbinu zao sio sahihi na kuona umuhimu wa kuja na mbinu zetu?
Nifollow hapa hapa JF nitakuja na mbinu effective ya kujikinga na virusi hivi na vile vitakavyokuja kwa 99%....sijawahi kuandika utani hapa JF!
1617986190908.png
 
Kuji-rock down ndiyo nini? Mara nyingi mtu anaposhindwa kuandika maneno rahisi (sizungumzi typo) unakuta na uekewa wake ni finyu. Angalia hiyo chati nilikuwekea hapo juu (kama unajua kusoma) uone vifo vingi ni watu wazee ambao huku kwetu hakuna, yaani wameshatangulia mbele za haki.
 
Nashukuru kwa kushiriki katika mjadala. Niliona nilete hii mada ili kwa pamoja tuweze kuona kama kweli sisi watanzania tunahitaji kupata chanjo hizo kwa sasa wakati wenye uwezo wa kila aina wameshindwa kwa kiasi hicho.
Umefanya vizuri kuuliza kuliko wengine wanaofanya ubishi na kutunga uongo. Nchi nyingi bado hali ya chanjo siyo nzuri i.e. wamechanjwa watu wachache sana hivyo bado huwezi kuona impact. Kitaalam wanasema angalau inatakiwa zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wawe wamechanjwa. Hata hivyo sehemu kama UK faida ya chanjo imeshaanza kuonekana kwani wamejitahidi kuchanja watu wengi. Soma hii article hapa:
 
Kuji-rock down ndiyo nini? Mara nyingi mtu anaposhindwa kuandika maneno rahisi (sizungumzi typo) unakuta na uekewa wake ni finyu. Angalia hiyo chati nilikuwekea hapo juu (kama unajua kusoma) uone vifo vingi ni watu wazee ambao huku kwetu hakuna, yaani wameshatangulia mbele za haki.
Kumbe huku wazee hakuna? Acha kutumia hisia(emotions) kufikiri!

Angalianpia case fatality ya nchi kama Brazil na Chile.

Lock/rock ni vitu viwili tofauti... mother tongue, kanda ya ziwa R na L tunazitumia kama herufi moja, sorry! Watu wajinga kama wewe huwa hawaoni maudhui bali makosa ya sarufi...(nina degree ya linguistics mkuu!)
 
Kama una degree ya linguistic basi utakuwa kilaza mkubwa. Tongue ndiyo inaandika maneno? Miaka yote uliyokaa shuleni hukujifunza kuandika maneno? Matamshi yanaweza kuwa magumu kutamka lakini siyo kuandika. Kuandika unajifunza tangu darasa la kwanza. Kila jamii ingetoa sababu za kijinga kama hizi dunia hii kungekuwa na lugha ya kiingereza? Back to the topic: Unajua idadi ya wazee iliyopo nchi kama UK au USA? Unajua idadi iliyopo Tanzania?
 
Safi kabisa hivi ndivyo JF ilipaswa kuwa yaani FACTS FACTS FACTS sio assumptions na ujuaji.
Ni kweli, jamaa amefanya uunguana sana kumjibu jamaa kwa fact kwa sababu itasaidia wengine ambao maswali ya mwanzisha mada alitaka kuwapotosha! Jamaa analenga kwamba chanjo haina maana kwa sababu, mbona Wajerumani wamechanjwa lakini wakufa tu?! Ni mtetezi wa wanyonge aka taga gang, mwananchi wa jamuhuri ya malaika kule ambapo hakuna corona!
 
Back
Top Bottom