Naomba ufafanuzi kwa anayetumia majiko haya ya induction je yanafaa kwa uchumi wa kitanzania

Naomba ufafanuzi kwa anayetumia majiko haya ya induction je yanafaa kwa uchumi wa kitanzania

ya induction umeme wote unaenda kwenye kupika
ya umeme ya kawaida, 40% ya umeme inapika, 60% ya umeme inapotea kama joto
ya kawaida achana nayo
Hivi ukiweka mkono unaungua?
 
Aiseee, ngoja tusubiri solar city kama ya elon musk kule texas
Solar city si kuwa kila nyumba yawekewa solar ni kwamba umeme unazalishwa kwa solar ila bado mtalipa bill kama kawaida

Hata Tanzania wanaanza utekelezaji mwaka ujao unakamilika 150MW
 
Unatumia umeme wa elfu 9 kwa muda gani?maana tumeambiwa yanalamba unit 2 kila baada ya saa 1?
Tufanye anapika kwa masaa 3 kila siku, kwa mwezi ni Unit 180 ambazo tayari zimezidi alichosema yeye.
Umeme wa 9000 kwa wasiojua maana ya umeme wanapata unit 70-90
 
Aluminium sio chuma na haiwez kufanya kazi kwa majiko hayo . Kujua sufuria zake wewe gusisha sumaku (magnetic field) ikishika basi ujue hiyo inafaa.

Ni mazuri sana japo kama upo sehemu yenye umeme mdogo ni rahisi kuungua (kufa)

Nadhani ni cheap zaidi kuliko hata gas na mkaa
Aluminium sio asili ya chuma?, au yanahitaji sufuria nzito kama zile za pressure cooker?
 
Huyu anayesema umeme unapote hajui hata maana ya induction. Ni kuwa haya majiko yanapika bila kutoa joto hata kidogo. Sufuria inayoshikwa na sumaku ndo inaweza kupika ukiweka ya kawaida hata haliwaki. Kinachochomwa ni chakula kilichomo kwenye sufuria and sufuria ikiwa tupu halichomi chcochote na halitatoa joto.
 
Back
Top Bottom