Naomba ufafanuzi wa gari aina ya Toyota Rumion

Kuna garage flan nilienda mkoani Dodoma nikakuta kuna fundi anafanya service ya engine oil kwenye Toyota Rumion anaweka oil hyo ya SAE40 kwa kweli nilijikuta naongea kimoyomoyo "kukosa maarifa ni umasikini mkubwa sana" . Garage za chini ya mwembe hapana aisee fundi ameshindwa kujua oil sahihi ya ile gari😣 mmiliki wa ile gari naye ni much know kweli😀kwa jinsi nilivyowakuta wanapiga story zao ikanipa ishara hiyo. Nilitamani ata nimwambie ile haikuwa oil sahihi kwa ile gari ila kwa muonekano na uongeaji wa yule jamaa nikaona ni jambo la busara kukaa kimya nifanye kilicho nipeleka niondoke.
 
Imagine gari kama hiyo anakuja kuuziwa mtu!Ndiyo maana kununua gari kutoka kwa rangi nyeusi ni uwendawazimu mkubwa sana.
 
Hii gari ya lumion ina mfumo wa tofauti wa gearbox, unaitwa CVT, so haitumii oil ya gear box ya kawaida ambazo zinawekwa kwenye gari zenye gear box za kawaida.
 

Ni oil ipi iliyo sahihi? Tusiojua tujue kabla hatujapokea vineriti vyetu?
 
Hii gari ya lumion ina mfumo wa tofauti wa gearbox, unaitwa CVT, so haitumii oil ya gear box ya kawaida ambazo zinawekwa kwenye gari zenye gear box za kawaida. View attachment 1774868
Huo utumiaji wa hiyo oil ya CVT ulielekezwa na mtu au ulisoma kwenye manual ya gari?maana nijuavyo mimi gari nyingi za Japan hata kama ina user manual inakuwa imeandikwa kijapan,kwahiyo tusiwalaumu sana wanojiwekea oil za kawaida kwenye hizo gari,ukweli ni kuwa hawajapata tu mtu wa kuwafungua macho kama ulivyofunguliwa wewe...
 
Karibuni kwenye garage yangu.Natoa huduma za kuondoa thermostat kwenye gari lako bure kabisa bila malipo.Pia engine oil za SAE40 zinapatika kwa hela ya Kitanzania 1,500/= tu kwa lita.Napatikana chini ya mwembe maarufu hapa Tandale kama mwembe wa Yanga.Karibuni sana.
 
Achilia mbali hilo,kuna magari mengi sana ambayo hayaruhusu kubadilisha gearbox oil iliyokuja na gari lakini watu wanabadilisha ATF iliyokuja na gari kama hilo kila baada ya 5000KM na kuweka ATF fake.Kumiliki gari kwa rangi nyeusi ni changamoto kwelikweli!
 
Nazifahamu hizo gari sio kwa kusoma manual kwa kutazama presentation yake. Hizo oil za CVT ni specific kwa gari zenye huo mfumo wa transmission ya aina ya CVT.

Huu ni mfumo mpya wa gear box tofauti na ule tumezoea wa gear box yenye counter gear ndani yake.

Hii ina kitu kinaitwa CVT chain na pulleys mbili ambazo zinabalance power kulingana na unavyokanyaga.

Kama unamtu anayo hii gari jaribu kuichukua uiendeshe halafu sikilizia kama utasikia inabadili gear (ile kama inastuka hivi kutoka gear moja kwenda nyingine). Hiyo kitu katu hautasikia sababu hii haina mfumo wa gear zile za sequence bali inatumia mfumo wa Continuous variance.

Sasa wengi mkinunua hizi gari, specifically hii lumion, mnaweka ila hydraulic ya kawaida bila kuzingatia swala la utofauti. Na kama ulikuwa haujui tu kuna mafundi wengi tu hawajui hiyo kitu wanafanya kimazoea tu kuweka oil kimaozea, ukikutana na gari kama za NISSAN, zenye CVT haichelewi kukuletea sarakasi baada ya muda.

Hapa chini nakuwekea picha za kampuni tofauti tofauti uone zina hiyo transmission fluid ila watu huwa wananunua za kawaida na kuweka kwenye gari yenye cvt.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…