Naomba ufafanuzi wa gari aina ya Toyota Rumion

Naomba ufafanuzi wa gari aina ya Toyota Rumion

Kitu kimoja ambacho watu wengi wenye vi baby woka hamkijui ni kwamba, watu wenye magari yenye "misuli" sio watu wa ligi. Wengi ni watu wenye hela zao, na hawana mpango wa kufa kizembe siku za hivi karibuni kwa ligi za kiboya.

Sasa wewe na ki passo chako, ki rumion sijui ki ist ukimuovateki mtu kama huyo barabarani, unakuja kujisifu hapa kwamba "umetunishiana misuli" na magari ya maana 😆😆 In short hutu tu baby woka twa kijapani hatuwezi kutunishiana msuli na gari yoyote ya maana, sema tu sio kila mtu anataka ligi barabarani.
Gari za maana ni zipi?
 
DAR - Mwanza nimewakimbiza Sana na mashine Yangu sidhani nilikuwa nabishana na Prado, Nissan X trail nakumbuka raum,rush na IST niliwaumiza Sana walipokuwa wanafanya ligi...hii ndinga nikienda nayo mkoani ni kwenda wa speed 150 - 170 km/h
Tatizo ni kwamba wakati wewe unawaza mnashindana wenzio hawana mawazo hayo
 
Kuna siku nilienda kula na kuisahau kuizima.imekaa inawaka na A\C ndani kwa dk 45.kurudi nilishangaa sana.toka siku hiyo napenda kuhakikisha mara mbili mbili kama nimeizima.
 
Kubadili gearbox oil sio tatizo as long as utaweka yenye standard inayotakiwa kwa gari husika. Kiusalama ni vema ukacheki na kubadili hizo vitu zote wewe mwenyewe.

Mfano, break pads na shoes, mafuta ya break, oil ya engine na gear box, coolant, thermostat inatakiwa ubadili nayo kama unamudu gharama ingawa sio lazima maana watu wengi huwa hawajui thermostat huwa zina muda wake wa kutumika sio forever part ile....
Safi sana unatoa point kitaalam zaidi
 
Nazifahamu hizo gari sio kwa kusoma manual kwa kutazama presentation yake. Hizo oil za CVT ni specific kwa gari zenye huo mfumo wa transmission ya aina ya CVT.

Huu ni mfumo mpya wa gear box tofauti na ule tumezoea wa gear box yenye counter gear ndani yake.

Hii ina kitu kinaitwa CVT chain na pulleys mbili ambazo zinabalance power kulingana na unavyokanyaga.

Kama unamtu anayo hii gari jaribu kuichukua uiendeshe halafu sikilizia kama utasikia inabadili gear (ile kama inastuka hivi kutoka gear moja kwenda nyingine). Hiyo kitu katu hautasikia sababu hii haina mfumo wa gear zile za sequence bali inatumia mfumo wa Continuous variance.

Sasa wengi mkinunua hizi gari, specifically hii lumion, mnaweka ila hydraulic ya kawaida bila kuzingatia swala la utofauti. Na kama ulikuwa haujui tu kuna mafundi wengi tu hawajui hiyo kitu wanafanya kimazoea tu kuweka oil kimaozea, ukikutana na gari kama za NISSAN, zenye CVT haichelewi kukuletea sarakasi baada ya muda.

Hapa chini nakuwekea picha za kampuni tofauti tofauti uone zina hiyo transmission fluid ila watu huwa wananunua za kawaida na kuweka kwenye gari yenye cvt..... View attachment 1775964
Na je ni oil gani nzuri naweza kuitumia kwa aina hio ya gari?
 
Watalam kwema, mm ni mTumish wa umma and nipo mkoani. Kwa sasa natumia Passo na ni gari yangu ya 2 kumiliki nikitokea kwenye toyota oppa.

Nimependa passo sababu ya ulaji wa mafuta, confotability na pia ni pana sana ndani kuliko ist, ist hainesi kama passo. Shida ya passo miguu ya mbele otherwise ni gari nzuri sana.

Nataka nishift kwenda Toyota Rumion, nimefanya comparison na honda crosroad kwa mafundi kadhaa nikaambiwa rumion nzuri zaidi ya honda. Chaguo langu la kwanza ilikuwa honda, ila kwa usharuri wa mafundi nimehamasika rumion.

Najua humu kuna wachabuzi wazuri zaidi wa haya magari, mimi sijui hata kubadili tyre tu nitaita funi.

Naomba kupewa ushuri
 
Back
Top Bottom