Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi ukianza kutoa Mafunzo ya FOREX naomba tujuzane ili na mimi niweze kupata ufahamu na mawazo yakinifu maana kuna mahali ulisema kuna mambo unamalizia kisha utafungua darsa la kutoa Mafunzo ya FOREX Asante.Nitumie PM boss, nitarudi kwako June nikiweka mambo yote sawa. Nafungua ofisi mpya very soon, km una vigezo unaweza kuwa kati ya waajiwa wa mwanzo kabisa.
Mkuu jamaa hawezi kutoa formula hata siku moja.wewe hujiulizi kwanini hao wanaojua huwa wanakuchenga? Formula inauzwa nenda kwa Dr wa mifugo muyaweke sawa boss.Hongera sana kwa hatua uliyofikia ndugu, binafsi natarajia kuanza kufuga broiler 1000 ningependa sana kujua jinsi ya kutengeneza chakula ili kupunguza gharama, naamini wapo watu wengi sana wanatamani kujua jinsi ya kuanda chakula bila ya kununua na wapo watu wanaojua jinsi ya kuandaa ila ukiwaomba msaada wa kuelekezwa unapigwa chenga, sasa basi mkuu ebu tufikirie kama itawezekana utupe somo hapa jinsi ya kuanda chakula cha kuku haswa broilers na layers naamini itakuwa msaada mkubwa kwa wafugaji wengi waliopo humu.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] , Huyu anaweza akawa mtume wa Mungu anaweza toa msaada ngoja tusubiri tuone. Yupo mmoja alianza vizuri akaishia kati kati.Mkuu jamaa hawezi kutoa formula hata siku moja.wewe hujiulizi kwanini hao wanaojua huwa wanakuchenga? Formula inauzwa nenda kwa Dr wa mifugo muyaweke sawa boss.
Usitegemee mteremko wa hivyo
Mbn unausemea moyo kaka..??Mkuu jamaa hawezi kutoa formula hata siku moja.wewe hujiulizi kwanini hao wanaojua huwa wanakuchenga? Formula inauzwa nenda kwa Dr wa mifugo muyaweke sawa boss.
Usitegemee mteremko wa hivyo
Mimi nimeishi mazingira ya wafugaji na watengenezaji wa chakula. Mimi mwenyewe Niko kwenye mpango wa kutengeneza formula yangu, kwa msaada ya Dr wa mifugo lakini huwezi kumfuata mtengezaji wa chakula akupe formula yake, sijawahi kuona kitu kama hicho, maana kuna madr wanauza hiyo formula hadi mil 1. Sasa kuna mtu atakupata bure?Mbn unausemea moyo kaka..??
Haaaha kweli man jamaa anaweza kutoa ngoja tusubiri[emoji1] [emoji1] [emoji1] , Huyu anaweza akawa mtume wa Mungu anaweza toa msaada ngoja tusubiri tuone. Yupo mmoja alianza vizuri akaishia kati kati.
Safi. Well said. Basi tutaomba wewe formula yako kama hutajali...!!! Toa kma sadaka kakaMimi nimeishi mazingira ya wafugaji na watengenezaji wa chakula. Mimi mwenyewe Niko kwenye mpango wa kutengeneza formula yangu, kwa msaada ya Dr wa mifugo lakini huwezi kumfuata mtengezaji wa chakula akupe formula yake, sijawahi kuona kitu kama hicho, maana kuna madr wanauza hiyo formula hadi mil 1. Sasa kuna mtu atakupata bure?
Watanzania tunapenda mteremko saaaana, hivi unajua kupitia hiyo formula watu wanakua matajiri wakubwa? Sasa kuna utajiri unapatikana kirahisi?
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]Safi. Well said. Basi tutaomba wewe formula yako kama hutajali...!!! Toa kma sadaka kaka
Hahahahahahahaha[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
CongratulationDepends na wapi ulipo, wapi ni karibu kutoka makazi yako ya kudumu.
Mimi nimekodi hekari 70 bonde la ruvu, ambapo nalima mpunga, mahindi, bustani (bamia, nyanya, mboga mboga, biringanya nk). Huku mashamba bei average ni 100,000 kwa mwaka. Rutuba si ya kutilia mashaka, wazaramu hawana muda kbs na kikimo.
Changamoto.
Hakuna kilimo kipindi kama hiki cha mvua, mashamba yote yanajaa maji kutoka mtoni, ni kama floods tuseme.
Hakuna maafisa wa kilimo, so itabidi uwawele wewe mwenyewe, mimi hua nachukua wataalamu wa Balton.
Hakuna wafanyakazi... Mimi si mbaguzi, lkn kiukweli watu wa pwani ni wazito sana, hawataki kazi kbs, wao ni Vigodoro, ngoma, uzinzi na maneno. So wafanyakazo mpk uwatoe mkoani huko.
Salute Bosses!!
Kwanza nitangulize shukrani zangu za dhati kwa wote waliobahatika kusoma uzi wangu niliouweka hapa miezi kadhaa iliyopita na tukaShare ideas mbali mbali za kibiashara. Lkn zaidi nimefarijika sana kuwa uzi ule umewafumbua macho watu kadhaa, na kuna wengine kupitia uzi ule wametoka from their comfort zone na kuanza kufanya kitu.
Link ni hii kama hukuusoma: Jinsi nilivyofanikiwa kutengeneza Sh. Milioni 19.9 ndani ya siku 35 kwa kutumia Milioni 3.8
Utangulizi
Biashara yangu ya kwanza nilianza miaka mi4 iliyopita nikiwa chuo mwaka wa 1.View attachment 512741Kampuni yangu ya kwanza ikiwa na miezi 9.
View attachment 512742Kampuni yangu ikiwa na miaka mi2.![]()
View attachment 5127431 ya operations ya kampuni yangu. (Picha ya weekend hii). View attachment 512745Weekend hii.
Basically sikua na mtaji mzito sana, hapa hua nakosa kuaminiwa kila sehemu, mtaji wng wa kwanza ulikua ni posho tuliyokuwa tukipewa tukiwa JKT na chenji nilizobaki nazo kutoka advance. Nilianza kwa ufugaji wa kuku 50 wa broiler, lkn leo tunavyoongea kila mwezi nazalisha thousands of chickens na nimediversify mpk kuwekeza mashambani.Heka 6 za cabbage, drip irrigation.![]()
Natengeneza chakula changu mwenyewe cha kuku, ambapo karibu 50% ya malighafi nazalisha mwenyewe kutoka kwenye mashamba yangu. Msibu huu, umekua wa neema sana, nina heka 48 za mahindi na 15 za mihogo, zote zikiwa miono.Shamba langu la mahindi![]()
Hapa kati vitu vingi sana sana sana vimetokea - nimefata tubiashara twingi twingi twa kunisogeza, nimepanda, nimeshuka, kusumbuana na mabenki, kuzurura ofisi za watu nk nk... but all I can say is 'the journey has been so boring & interesting at the same time'.
Kwasasa pia nina shares 25% kwenye kampuni ya technology niseme ICT. Ambapo naweza sema nimekuapo tangu wakati ikiwa bado ipo kwenye ideation phase mpk sasa kdg kuna mwanga unaonekana.
Nipo kwenye mchakato pia kua ktk kampuni yangu ya 3, a sort of partnership to be exact. Hii yote ni katika jitihada zangu za kutimiza malengo niliyojiwekea ya kuwa na vyanzo vya pesa kutoka makampuni 5 tofauti kabla sijatimiza miaka 25.
Mafanikio
Kusimama ktk ujasiriamali hadi leo hasa kwa nchi km TZ si jambo dogo, ni mafanikio makubwa sana, achilia mbali kukuza biashara from scratch.
Lkn nimeweza kutambulika kitaifa na kimataifa.
Ni ngumu sana kujiita mfanyabiashara makini kama TPSF hawakufahamu.Nikiwa na mkurugenzi wa TPSF Dr. Simbeye![]()
Nimepata awards 4 za kimataifa ktk biashara kutoka organisations mbali mbali ikiwemo Mastercard foundation.moja kati ya award niliyopata mwaka jana.![]()
Nimekua featured kwenye media stations nyingi sana kitaifa na kimataifa. Mfano:
Forbes, CNN Africa, BBC World Service (outlook), BBC Africa, How we made it in Africa, Africa Successive Stories, The incubators Africa, SABC, Venture Africa, African Business Magazine nk nk. Nimefanya interviews nyingi sana zingine hata sikumbuki.
Nimepata fursa ya kualikwa kuzungumza ama kuattend conferences kubwa as an entrepreneur. Mfano mwaka jana nilizungumza kwenye conference kubwa sn duniani huko Washington DC na nikaalikwa VIP experience katika TEDx Michigan. Hapa Bongo pia nimeongea kwenye conference za kuandaa sera za kilimo mwaka 2016 na mwaka huu pia. Pia nimealikwa kwenye talks hizi za uhamasishaji mara kadhaa.
Pia mwaka jana nilialikwa kwenye conference kubwa sana ya kilimo hapo Nairobi, ambapo 1 ya wageni rasmi alikuepo Bill Gates. Hii ilikua mara yangu ya kwanza kumwamkia Dr. J. Kikwete in person.
![]()
Tangu nimeanza biashara nimezunguka nchi nyingi sana. Kitu kizuri zaidi ktk kutembea ni kukutana na watu, watu wa faida kama My business mentor Vusi Thembekwayo, Alex Okosi (CEO wa MTV Afriva), Prof. Thom Jayne, Richard Maponya, Chimamanda Ngozi, Ahmed Ahmad Alhendawi (UN secretary general's envoy on youth), Mo Dewji, Dr. Strive Masiyiwa (CEO Econet), Acha Leke (CEO McKinsey Afr), Dr. Fred Swaniker, Agnes Kalibata... hii list ni ndefu sana, sitaki nikuchoshe.
Mwisho
Katika kipindi hiki ambacho rate ya graduates wanaoingia mtaani ni kubwa kuliko uwezo wa serikali wa kuajiri, nahisi ujasiriamali ndio njia rahisi ya mtu kuingiza mkono kinywani, na kuacha kutegemea wazazi. Pia kuna ndugu zng wale 10,000 - kutokua na cheti si mwisho wako wa maisha.
Sasa nimeona ni jambo la kheri kama nitashare na wewe chochote ninachokifahamu kuhusu biashara. Pia naamini humu JF kuna watu wa kila calibre, so kwa kitu ambacho sitaweza kutoa ufafanuzi makini nakaribisha watu wengine watoe mawazo yao.
Nafahamu JF kuna watu wanaonifahamu either kwa kuniona/kunisoma kwa media ama kumeet in person, naomba ufiche identity yangu kama mimi nilivyoamua kuificha. Ni suala la kuheshimiana tu. The goal is to be successful not to be famous.
Karibuni sana. Nitajitahidi kujibu maswali yote kadri niwezavyo.
Salute!!
Muhimu
Sitoi mawasiliano, na wala sitojibu P.M
Kuna msemo wazungu wanasema "No one is busy, it's just a matter of priorities".
Niseme tu wazi, kuRun biashara ukiwa umeajiriwa ni changamoto kubwa sana sana. Unajua biashara yoyote inakuja na risks nyingi, na unapokua mbali na biashara yako, basi unaongeza risk juu ya risk ambazo hauzimanage wewe kama wewe. Mimi nikiwa nasoma chuo ilikua rahisi, as you know elimu yetu chuo haiko tight sana, inakupa muda mwingi wa kua free... hata usipoattend lectures mchana usiku unaeza kesha na ukawa hauna utofauti na aliyeingia pindi.
Changamoto ilikuja kipindi cha field (sisi tunaita Practical training). But ilikua rahisi kudeal na hii situation, na inaweza kuwork hata kwako.
**Kuwa muwazi.
Kama mkataba wako unakuruhusu kumiliki biashara nje ya ofisi, basi usiwafiche waajiriwa wenzio, boss wako nk. Hii itakupa wewe advantage 1, endapo utakua na dharura basi wenzio hapo ofisini hawatakuwa na maswali mengi ya utata utata, so itakufanya ww uwe usijifeel insecured. Kama Boss wako ni mwelewa itakua rahisi zaidi kwako.
**Strong team.
Hapa ndio inabidi uweke nguvu nyingi zaidi. Kuwa na team makini kwenye biashara yako kwa kiasi fulani itaweza kufeel ile gap ya wewe kutokuwepo. Team ambayo kila mtu yupo accountable, integrity ya hali ya juu na watu wanaothamini unachofanya. Pia unaweza kuwapa motisha kwa kuwaahidi equity ktk kampuni. Mfn kuwaambia, kama biashara itatengeneza faida ya mil 10 kwa mwezi, basi nitawapa 20% kama bonus. Hii inawapa morale ya kupiga mzigo haswa.
Tuvute subira tuuh.Haaaha kweli man jamaa anaweza kutoa ngoja tusubiri
Hahahahahahahaha
Alishakataa hiyo kitu! Ukipitia comments za mwanzo kuna Jamaa aliomba hiyo formula!Tuvute subira tuuh.
Kuna mpvmbavu aliingia hapa akaniName call akaweka pa1 na moja ya article ambayo nilikua featured. Hii kitu imenidisappoint sana, hata nguvu ya kurudi huku kujibu comments ikaisha, coz ule ni usaliti na unafiki wa kiwango cha standard gauge.Mkuu hapo kwenye kuku naomba unisaidie!
Ni aina gani nzuri ya kuku wa mayai?
Na je nikifuga vizuri kwa kufuata formula zote wanaweza kuanza kutaga kwa umri gani?
Na je, nitagunduaje pale ninaponunua vifaranga nisipewe vidume(vijogoo)?
Maana mwaka Jana nilinunua vifaranga 200 ila sehemu kubwa yalikuja kuwa majogoo!
Naomba msaada wako ndugu ONTARIO
Ni kweli mkuu pole sana,unajua kwa mafanikio yako wengi wanatamani hata wakuone kwa macho tu, kwani sio kitu kidogo ulichofanya!Kuna mpvmbavu aliingia hapa akaniName call akaweka pa1 na moja ya article ambayo nilikua featured. Hii kitu imenidisappoint sana, hata nguvu ya kurudi huku kujibu comments ikaisha, coz ule ni usaliti na unafiki wa kiwango cha standard gauge.
Unajua swala la kua anonymous hapa JF kuna umuhumu wake, naweza kuwa free kuchangia jukwaa lolote na kwa uhuru wote, tofauti na ninapofahamu kua watu wanajua identity yangu. Najua watu wakinifahamu nitapata usumbufu sana FB, IG, twitter nk nk. Kitu ambacho sikitaki, yani yule bwege kunianika hapa nimekuta notification 146 FB pamoja na messenger. Bado kuna mijitu mingine ilikua inafurahia mimi kuanikwa hapa wakati wao wapo anonymous. Shame!!
Boss!! Layer wamechezewa sana hapa bongo. Yani nikisema sana namaanisha sana. Kuna chanjo lazima kuku wa layer apigwe ile dakika katotolewa kabla hajamaliza siku inaitwa Mareks vaccination. Wasipopewa hiyo chanjo kuku hawawezi kukatiza salama hadi kufika miezi 6. Sasa kikawaida hii chanjo inabidi itolewe na kampuni inayototolesha. Lkn kwasasa ni wizi, hawatoi kabisa - mbaya zaidi kifaranga huwezi kumjua, apewe asipewe huwezi kumtofautisha.
Njia pekee ni kupata vifaranga wa kenya kampuni ya KenChick, hawa hua wana product ya kueleweka. Tatizo ni kuwa serikali kupitia wizara husika ilishapiga marufuku importation ya DOCs kutoka nchi nyingine hasa kwajili ya kuepuka Avian Influenza ama bird's flue. lkn bado hao kuku wa KenChick wanaingia Bongo kimagumashi, wanapitishwa kwa siri sana, na bei yao kdg imechangamka.
Kama utatumia kampuni ya Bongo, basi hakikisha unanunua vifaranga direct kutoka kwenye deport ya Silverland, wapo pale vetenary nyuma ya wizara ya kilimo. Ukinunua interchick ni kama unabet boss. Layers wanachezewa sana aisee.
Pia si rahisi kupewa majogoo, yani labda uwe mzembe kupita maelezo. Hao utofauti wao upo kuanzia vilemba, kucha na midomo.
Kuku bora wa layer inabidi aanze kudondosha yai mwezi wa 5 na wiki 1. Mwezi wa 6 inabidi achanganye sasa kutaga. Baada ya hapo akiwa na huduma nzuri inabidi adondoshe mayai miezi 18 hadi wanauzwa.