Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

Kaka hongera sana sana aisee, sasa mm nataka kufanya biashara ya kusambaza unga wa sembe na dona kwa APA Arusha so naomba ushauri wako kk, na biashara hii nategemea kuaanza soon Early of July baada ya kumaliza process ya kufunga machine so more info plz.
 
Nitumie PM boss, nitarudi kwako June nikiweka mambo yote sawa. Nafungua ofisi mpya very soon, km una vigezo unaweza kuwa kati ya waajiwa wa mwanzo kabisa.
Kiongozi ukianza kutoa Mafunzo ya FOREX naomba tujuzane ili na mimi niweze kupata ufahamu na mawazo yakinifu maana kuna mahali ulisema kuna mambo unamalizia kisha utafungua darsa la kutoa Mafunzo ya FOREX Asante.
 
Hongera sana kwa hatua uliyofikia ndugu, binafsi natarajia kuanza kufuga broiler 1000 ningependa sana kujua jinsi ya kutengeneza chakula ili kupunguza gharama, naamini wapo watu wengi sana wanatamani kujua jinsi ya kuanda chakula bila ya kununua na wapo watu wanaojua jinsi ya kuandaa ila ukiwaomba msaada wa kuelekezwa unapigwa chenga, sasa basi mkuu ebu tufikirie kama itawezekana utupe somo hapa jinsi ya kuanda chakula cha kuku haswa broilers na layers naamini itakuwa msaada mkubwa kwa wafugaji wengi waliopo humu.
 
Big up sana.

Kijana mwenzangu kutoa ndio siri pekee ya utajiri. Na wewe unalifanya hilo, uongezewe zaidi
 
Mkuu jamaa hawezi kutoa formula hata siku moja.wewe hujiulizi kwanini hao wanaojua huwa wanakuchenga? Formula inauzwa nenda kwa Dr wa mifugo muyaweke sawa boss.

Usitegemee mteremko wa hivyo
 
Mkuu jamaa hawezi kutoa formula hata siku moja.wewe hujiulizi kwanini hao wanaojua huwa wanakuchenga? Formula inauzwa nenda kwa Dr wa mifugo muyaweke sawa boss.

Usitegemee mteremko wa hivyo
[emoji1] [emoji1] [emoji1] , Huyu anaweza akawa mtume wa Mungu anaweza toa msaada ngoja tusubiri tuone. Yupo mmoja alianza vizuri akaishia kati kati.
 
Mkuu jamaa hawezi kutoa formula hata siku moja.wewe hujiulizi kwanini hao wanaojua huwa wanakuchenga? Formula inauzwa nenda kwa Dr wa mifugo muyaweke sawa boss.

Usitegemee mteremko wa hivyo
Mbn unausemea moyo kaka..??
 
Mbn unausemea moyo kaka..??
Mimi nimeishi mazingira ya wafugaji na watengenezaji wa chakula. Mimi mwenyewe Niko kwenye mpango wa kutengeneza formula yangu, kwa msaada ya Dr wa mifugo lakini huwezi kumfuata mtengezaji wa chakula akupe formula yake, sijawahi kuona kitu kama hicho, maana kuna madr wanauza hiyo formula hadi mil 1. Sasa kuna mtu atakupata bure?

Watanzania tunapenda mteremko saaaana, hivi unajua kupitia hiyo formula watu wanakua matajiri wakubwa? Sasa kuna utajiri unapatikana kirahisi?
 
Safi. Well said. Basi tutaomba wewe formula yako kama hutajali...!!! Toa kma sadaka kaka
 
Congratulation

 
Mkuu hapo kwenye kuku naomba unisaidie!
Ni aina gani nzuri ya kuku wa mayai?
Na je nikifuga vizuri kwa kufuata formula zote wanaweza kuanza kutaga kwa umri gani?
Na je, nitagunduaje pale ninaponunua vifaranga nisipewe vidume(vijogoo)?
Maana mwaka Jana nilinunua vifaranga 200 ila sehemu kubwa yalikuja kuwa majogoo!
Naomba msaada wako ndugu ONTARIO
 
Kuna mpvmbavu aliingia hapa akaniName call akaweka pa1 na moja ya article ambayo nilikua featured. Hii kitu imenidisappoint sana, hata nguvu ya kurudi huku kujibu comments ikaisha, coz ule ni usaliti na unafiki wa kiwango cha standard gauge.

Unajua swala la kua anonymous hapa JF kuna umuhumu wake, naweza kuwa free kuchangia jukwaa lolote na kwa uhuru wote, tofauti na ninapofahamu kua watu wanajua identity yangu. Najua watu wakinifahamu nitapata usumbufu sana FB, IG, twitter nk nk. Kitu ambacho sikitaki, yani yule bwege kunianika hapa nimekuta notification 146 FB pamoja na messenger. Bado kuna mijitu mingine ilikua inafurahia mimi kuanikwa hapa wakati wao wapo anonymous. Shame!!

Boss!! Layer wamechezewa sana hapa bongo. Yani nikisema sana namaanisha sana. Kuna chanjo lazima kuku wa layer apigwe ile dakika katotolewa kabla hajamaliza siku inaitwa Mareks vaccination. Wasipopewa hiyo chanjo kuku hawawezi kukatiza salama hadi kufika miezi 6. Sasa kikawaida hii chanjo inabidi itolewe na kampuni inayototolesha. Lkn kwasasa ni wizi, hawatoi kabisa - mbaya zaidi kifaranga huwezi kumjua, apewe asipewe huwezi kumtofautisha.

Njia pekee ni kupata vifaranga wa kenya kampuni ya KenChick, hawa hua wana product ya kueleweka. Tatizo ni kuwa serikali kupitia wizara husika ilishapiga marufuku importation ya DOCs kutoka nchi nyingine hasa kwajili ya kuepuka Avian Influenza ama bird's flue. lkn bado hao kuku wa KenChick wanaingia Bongo kimagumashi, wanapitishwa kwa siri sana, na bei yao kdg imechangamka.

Kama utatumia kampuni ya Bongo, basi hakikisha unanunua vifaranga direct kutoka kwenye deport ya Silverland, wapo pale vetenary nyuma ya wizara ya kilimo. Ukinunua interchick ni kama unabet boss. Layers wanachezewa sana aisee.

Pia si rahisi kupewa majogoo, yani labda uwe mzembe kupita maelezo. Hao utofauti wao upo kuanzia vilemba, kucha na midomo.

Kuku bora wa layer inabidi aanze kudondosha yai mwezi wa 5 na wiki 1. Mwezi wa 6 inabidi achanganye sasa kutaga. Baada ya hapo akiwa na huduma nzuri inabidi adondoshe mayai miezi 18 hadi wanauzwa.
 
Ni kweli mkuu pole sana,unajua kwa mafanikio yako wengi wanatamani hata wakuone kwa macho tu, kwani sio kitu kidogo ulichofanya!
Usikate tamaa mkuu ni wengi tunakufuatilia humu Na unatusaidia sana vijana wenzio!
Nakuomba usikate tamaa kutusaidia pale unapopata jambo la kutushirikisha!.ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…