Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

boss hivi ukipacking nyama ya kuku hivyo si unatakiwa upige na chemical zinazozuia chakula kuharibika
 
Boss Mimi mwenyewe yule jamaa sikumkubali wala nini, alizingua sana.

But usikate tamaa endelea kutupa madini kaka.

Hapo kwenye vifaranga kutoka Kenya huwa vinapatikana wapi haswa kwa hapa bongo? Yaani daaaa hii nchi yetu ujanja ujanja mwingi sana sijui kwanini yaani.

Na kwenye vifaranga wa kuku wa nyama ni kampuni gani iko vizuri?
 
How to penetrate in Tanzania market for gas [emoji618]️ products
 
Pole sana mkuu..kila mtu na mawazo yake..nadhan ulishampa maelekezo sasa kwa yeye aliona kama cc tunafaidi sana uwepo wako akaamua kukuchanganya ..pole sana
 
Alishakataa hiyo kitu! Ukipitia comments za mwanzo kuna Jamaa aliomba hiyo formula!
Mwenyewe natamani hata akipatikana mtu wa uhakika nimlipe anifundishe
Duh kumbe ameshagoma kutoa, kweli kimfaacho mtu chake, mkuu ikiwezekana tuunganishe nguvu tutafute mtu tumlipe. Kama kuna wengine wapo interested they can join pia tuunganishe nguvu.
 
Hongera sana Ontario kwa consultation unayotupatia ktk jukwaa hili.

Je, unayo idea juu ya Ukandarasi (Building and Civil works Contractor)?

Kama unayo idea/ufahamu juu ya hilo, tunaomba utupatie ufafanuzi hii biashara ikoje, inalipa au la!
 
Duuuh,kumbe kuna watu walikuharibia aisee[emoji134] [emoji134] [emoji134] pole sana.......Hao ndio binadamu mkuu hawaelewi na uliweka angalizo hapo juu!!!
 
duuuh!!!!
dunia kuna watu na viatu.
hakika mkuu unaangukia kwenye kundi la kwanza. hongera sana.
ya kwangu ni haya hapa.
1.mradi wa kufuga nyuki eneo mikoa ya pwani dar, moro, pwan na tanga.
kwa kuanza na mizinga mitano ya kisasa inaweza kugharimu kiasi gani kama unasehemu, eneo la kufungia.
makadilio ya usimamizi, mradi ukienda vizuri return yake?
masoko, yaaninupatikanaji haswa soko la nje ya nchi
2 . Mradi wa kuku wa mayai japo wengi nimeona wameuliza sana, hivo kwa maono inawezekana kukawa na wazalishaji wengi zaidi miaka ya mbele maana interest za watu zipo juu sana
kwa mtu anaeanza na kiasi cha kuku 50 wa mayai hapa gharama zikoje yaani kuanzia banda mpaka wanafikisha miezi 5ya kwanza.
asante na MUNGU Akubariki sana.
 
Mkuu hongera sana kwa hatua kubwa uliyopiga, pia nimekua nikifuatilia kwa makini sana thread zako nyingi san na nyingi ni za faida sana kwangu binafsi ujasiliamali katika kilimo umenivutia sana na nimehamasika sana tatzo ni how to get started katika hii inatokana na maeneo ya uputkanaji wa mashamba pia initial capital inayohitajika kwa mfano nikiwa na 2m naweza anza na kitu gani na kwa kiasi gani ili kiwe effective. Ahsante Mungu akubariki.
 
Ontario wewe ni mkali na pia biashara ipo tu kwenye DNA yako tofauti na wengine ambao wanafanya kwa kujaribu. Kuna maamuzi mengine unafanya kwenye kazi zako yanaonekana rahisi lakini kwa mortal beings wengine ni mtihani mkubwa. Mungu akubariki sana.

Changamoto kubwa inayotukabili wajasiriamali wa Tanzania ni kutotafuta taarifa za kutosha za masoko kiasi kwamba soko la dar likijaa basi tunakosa kwa kuuza.

Pia tunakata tamaa mapema endapo biashara inazingua bila kuchunguza tumekwama wapi na kwa sababu zipi. Vijana tusikate tamaa kwani afrika mashariki kuna soko kubwa sana la watu zaidi ya million 100 kwa ajili yetu.
 
Solute sana mkuu Ontario, Nimekufahamu kuanzia ule uzi wa "matrekta" .
Mm pia ni kijana kama wewe, nilidrop chuo baada ya wazazi kushindwa kunilipia ada kutokana na umasikini. Jana nimeona uzi wako kuhusu foreign Currency EXchange(FOREX), nimehamasika mwaka huu nisome BBA in finance Open university huku nikijichanga taratibu, kwa malengo ya kujiunga forex soon and not later than 2year from now. Natumaini ntakuwa ambassador wako mzuri kanda ya ziwa.

Kwenye blue print yangu nataka nianze na kununua samaki na kuwasambaza mjini maana nipo karibu na ziwa Victoria, baada ya hapo nitajichovya kwenye kilimo angalau misimu miwili na ntakuwa namaliza masomo yangu na hapo sasa ndipo nitajiunga na FOREX.

Sasa mimi nataka unisaidie hapa:
1. How can I stay motivated throughout the time amid different challenges especially when you have no a secure job?

2. In case I'm desperate how should I warm up to stay in a track?

3. Je kuna wakati unaskia kukata tamaa hasa pale mambo yanapokuwa magumu? Na huwa unafanyaje ili ubaki motivated?

Na mwisho kabisa naomba uwe mentor wangu kwenye masuala ya ujasiriamali na biashara.
 

Usinisahau kwenye training
 
Ninatamani sana kuwa mjasiriamali.tatizo kibarua kimenikamata kwelikweli na nahofia nikiacha kibarua changu mbelen ninaweza ku fail na sasa hivi ajira ni ngumu usawa huu wa magu nitakufa njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…