Kuna mpvmbavu aliingia hapa akaniName call akaweka pa1 na moja ya article ambayo nilikua featured. Hii kitu imenidisappoint sana, hata nguvu ya kurudi huku kujibu comments ikaisha, coz ule ni usaliti na unafiki wa kiwango cha standard gauge.
Unajua swala la kua anonymous hapa JF kuna umuhumu wake, naweza kuwa free kuchangia jukwaa lolote na kwa uhuru wote, tofauti na ninapofahamu kua watu wanajua identity yangu. Najua watu wakinifahamu nitapata usumbufu sana FB, IG, twitter nk nk. Kitu ambacho sikitaki, yani yule bwege kunianika hapa nimekuta notification 146 FB pamoja na messenger. Bado kuna mijitu mingine ilikua inafurahia mimi kuanikwa hapa wakati wao wapo anonymous. Shame!!
Boss!! Layer wamechezewa sana hapa bongo. Yani nikisema sana namaanisha sana. Kuna chanjo lazima kuku wa layer apigwe ile dakika katotolewa kabla hajamaliza siku inaitwa Mareks vaccination. Wasipopewa hiyo chanjo kuku hawawezi kukatiza salama hadi kufika miezi 6. Sasa kikawaida hii chanjo inabidi itolewe na kampuni inayototolesha. Lkn kwasasa ni wizi, hawatoi kabisa - mbaya zaidi kifaranga huwezi kumjua, apewe asipewe huwezi kumtofautisha.
Njia pekee ni kupata vifaranga wa kenya kampuni ya KenChick, hawa hua wana product ya kueleweka. Tatizo ni kuwa serikali kupitia wizara husika ilishapiga marufuku importation ya DOCs kutoka nchi nyingine hasa kwajili ya kuepuka Avian Influenza ama bird's flue. lkn bado hao kuku wa KenChick wanaingia Bongo kimagumashi, wanapitishwa kwa siri sana, na bei yao kdg imechangamka.
Kama utatumia kampuni ya Bongo, basi hakikisha unanunua vifaranga direct kutoka kwenye deport ya Silverland, wapo pale vetenary nyuma ya wizara ya kilimo. Ukinunua interchick ni kama unabet boss. Layers wanachezewa sana aisee.
Pia si rahisi kupewa majogoo, yani labda uwe mzembe kupita maelezo. Hao utofauti wao upo kuanzia vilemba, kucha na midomo.
Kuku bora wa layer inabidi aanze kudondosha yai mwezi wa 5 na wiki 1. Mwezi wa 6 inabidi achanganye sasa kutaga. Baada ya hapo akiwa na huduma nzuri inabidi adondoshe mayai miezi 18 hadi wanauzwa.