Wakuu ni wakati mwingine tena:
Vocha hizi tunazotumia kuongeza salio kwa ajili ya mawasiliano kwenye mitandao mbalimbali, matumizi yake yameenea sana sasa hasa karne hii.
Hii inanifanya nione biashara ya kuuza vocha za jumla kuwa inaweza kuwa ni yenye kutoka sanaa na outturn yake ikawa ya kuridhisha.
Kwa mfano kuna jamaa fulani pale maeneo ya Temeke anauza vocha kwa jumla wateja wamepanga mstari kusubiri huduma.
Yeye anauza:-
500 kwa 475 Tsh .
1000 kwa 950 Tsh.
Sijajua upande mwingine wa shillingi. Yeye ananunuaje na anazipata wapi hapa Dsm na utaratibu umekaajee. Hebu nipate mawazo yenu wakubwa.
Mna maoni gani katika hili?
Asanteni sana wakuu.
View attachment 1474098View attachment 1474099