Naomba ushauri biashara ya kusajili laini na kuuza vocha

Asante kwa ushauri
 
Kila siku akawa na wastani wa wateja ishirini wanaotoa elfu tano kwa siku.. kwa kamisheni hiyo mpaka mwisho wa mwezi inakuwa ndefu

Mpe ushauri wa kufanya kazi nyingine sio unamwambia aache bila njia mbadala na wazo lake

Ukiwa na wateja mfano tano watoa 5000 kila siku kamisheni inaweza kuwa jumla kama 750 hivi tena inaweza isifike. Maana mtu akitoa laki 3+ kamisheni ni 1000.

Nahisi ulinielewa tofauti hapo awali mkuu.

Kaulizia uwakala nimemwambia ukichaa wa hiyo biashara, ni yeye akae atafakari akitaka wazo atapewa.

Ukiona wakala ana pesa na karidhika na uwakala mchunguze vizuri, unaweza shika kichwa ukasema Looh! Umzaniaye siye kumbe ndiye.
 
Habari,
Yeyote mwenye uwelewa na biashara ya kuuza vocha za mitandao ya simu mbalimbali kwa kutumia mobistock.
 
Line moja unatumia kuuza vocha aina zote Tanzania hii.

Na kuuza vifurushi vyote vya Tigo.

Pia unauza na luku kupitia line hiyo hiyo.
 
Kuna wakala anakuunga.

Kwa mara ya kwanza ukiweka tsh 10000 kugeuza kuwa vocha unakatwa buku baada ya hapo hukatwi tena.

Unaendelea na kuuza vocha.
 
Ni nzri ndugu..ndo nnayoitumia shop...kwa siku ukiwa na mzunguko mzur ht vocha laki unauza....!!mimi kwa mzunguko wangu mpk naitumia kutoa pesa kwa wateja...!!ananijazia float ya vocha nampa cash

Namkadiria kiwango cha makato kweny kutoa pesa....maisha yanaendelea
 
Thread za namna hii zikienda sana basi page 5 sijui shida nini
 
Wakuu ni wakati mwingine tena:

Vocha hizi tunazotumia kuongeza salio kwa ajili ya mawasiliano kwenye mitandao mbalimbali, matumizi yake yameenea sana sasa hasa karne hii.

Hii inanifanya nione biashara ya kuuza vocha za jumla kuwa inaweza kuwa ni yenye kutoka sanaa na outturn yake ikawa ya kuridhisha.

Kwa mfano kuna jamaa fulani pale maeneo ya Temeke anauza vocha kwa jumla wateja wamepanga mstari kusubiri huduma.

Yeye anauza:-
500 kwa 475 Tsh .
1000 kwa 950 Tsh.

Sijajua upande mwingine wa shillingi. Yeye ananunuaje na anazipata wapi hapa Dsm na utaratibu umekaajee. Hebu nipate mawazo yenu wakubwa.

Mna maoni gani katika hili?

Asanteni sana wakuu.

 
Mada zenye viwango kama hizi huwa hazipati wachangiaji kabisa
 
Reactions: apk
Vocha mfano ya HALOTEL ukichukua PCs 11000 za buku buku unauziwa 925 Jumla ya PCs hizo ni 10175000TZS. Hiyo ukitaka nitakupa namba za watakaokuuzia kwa being iyo. Ukitaka kuchanganya za 2000,500,&5000 ni wewe tu kulingana na mahitaji ya solo lako.

Pia airtel na voda wao Ukienda kwa wale voda shop ama airtel shop wanaweza wakakuuzia kwa 930 kama muongeaji sana kama MIE ila watakuuzia kwa 935 kwa ile alfu moja sasa unazidisha ama kugawa ila thamani yake Iko ivyo ivyo.

Hawa ukichukua mzigo Wa kuanzia 5M mkuu watakuuzia. Togo sijawahi ziuza mana eneo nililo kuwa nauzia Tigo haishiki kabisa.

Inataoka sana ila ujue Milioni kumi plus unapata faida ya laki moja ila ukimaliza mzigo Wa Milioni 20 kwa siku Uko njema sana mzazi
 
Shukran sana mkuu. Nimepata mwanga pa kuanzia
Nimeku-PM ili kupata contacts
 
Umemuona mtu anauza na bei unaijua, ungeanza na huyo jamaa kumuuliza angekuambia kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…