Naomba Ushauri: Binti yangu amepangiwa Chuo na huku alishaanza masomo ya Pre-Form 5

Hivyo combination amechaguliwa na mwalimu wake wa taaluma hapo shuleni sababu ana pass marks za masomo ya science na Arts zote
pamoja na pass ya math except physics ndio amekosa pass marks.
Bongo tunasafari ndefu sana
 
Nashauri aende atakuja kuwa mtu asiye julikana na utakuja kunishukuru badae
 

Kama una uwezo peleka mtoto kwa system yote ya Tanzania, for 1 to 6, watoto wa sasa ni wa dogo Sana, mwache alelewe miaka mingine 2 akiwa chini ya uangalizi.

Usikubali ku peleka huyo mtoto chuo na kupata uhuru wote wa chuo akiwa na huo umri ni hatari kwa binti yetu, please, please ndugu peleka mtoto wetu form five.

Hata kama hauna uwezo wewe jitahidi, atapata mkopo ataendelea huko mbele. Usiikatishe hii safari ya Shule ya mtoto kama una huo uwezo mpeleke secondary ya private.
 
Surely, Kama wamepata opportunity ya kwenda chuo waende tu

Kwanza ajira za siku hizi wanabeba sana watu wenye cerificates na diploma

Kupanga ni kuchagua
 
muache aendelee na Advance hiyo course ni kimeo
 
Asante sana ndugu kwa ushauri nimekuelewa vizuri .!ubarikiwe.
 
anaweza akaenda chuo na pia ukienda kwenye website ya nacte wametoa ruhusa ya kubadili coarse kama haujaipenda hiyo waliokuchagulia sio lazima asome hiyo coarse anaweza kuibadili pia hata chaguo la chuo anaweza kubadili pia...
 
Acha kumdanganya mwenzio..!! Kila kozi kuna waliotoboa na walishindwa..!
 
Mwache aende akasome Kurasini. Chuo kikuu hata kutokea kutasini atafika tu, tena huku akiwa na profession tayari. Huko form five say akifeli, bado anakuwa hana profession.
 
Majoblesi na waliosoma kimagumash wanaogopa f5 hatari!

Mpeleke binti f5 akapge hyo Hge, uhakika wa kufaulu ni mkubwa sana akikaza kidogo tu.

History 2 itamfumua ubongo na kuwa mbish hasa na ataelewa mifumo kibao ya duniaa. Hata la putin na ukren atalijua.

Econo atakuwa na ufaham mpana kuliko wengi wanavojua. Hata mfumko atajua unakujaje na kuishaje.

Then ataenda chuo kikuu kwa ufadhl wa heslb akiwa na miaka 19!
 
najua wengi watakuambia kuwa hyo course haina market/ajira lakini usilolijua hicho chuo 70% wanakuwa wako selected na wahusika wa mambo fulani ya nchi na mpaka anachaguliwa kuja hapo ujue kuna pendekezo kutoka kwa mwalimu/walimu ambao wako taasisi fulani kuwa anafaa kuja kusoma hyo course hapo chuoni.

So endapo yale waliyokuwa wanayataka akaendelea nayo na kuyakuza utashangaa tu field anapelekwa sehemu zile za inner cycle au akimaliza chuo anapelekwa nje au katika ofisi fulani na pia tarajieni kubadilika kuanzia mavazi/tabia/mpka mfumo mzima wa maisha.
Talking with experience
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…