Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aise brother una dharau wewe ...
Ina maana mwalimu hana hadhi ya kuendesha gari la 18 M....
Miaka yote ambayo ameitumikia serikali kama alishasomesha watoto wake wote, ameshajenga nyumba zake, ana miradi yake, akinunua gari hata m 30 tatizo liko wapi..?
Zipo japo chache sanaHizi sidhani kama kuna makampuni ya Japan yanayouza used cars ambayo bado wanazo,labda kama atanunua ya mkononi ambayo obvious itakuwa imechoka sana...
Ni kweli mkuu ....me nilimshangaa..nikahisi atakuwa ni mkurugenzi wa TRA makao makuu ndiyo maana anadharau walimu ijapokuwa amepita mikononi mwa walimu..Dah umetoa maneno mdomoni kwangu kabisa mkuu, mtu kama ameshafanikisha malengo yake mengine ya muhimu kwanini nayeye sipate raha?. Kwanza M18 sio hela kubwa sana, kuna watu wananunua gari M50. Au kuna sehemu imeandikwa Walimu hawaruhusiwi ku-enjoy maisha. Maisha haya tunayaishi mara moja tu inafika kipindi mtu inabidi afurahie matunda yake.
Rav 4 old model. Achana na nissan achana na subaru. Mtafutie gari litakalompa amaniMama yangu ni mwalimu na anastaafu mwaka huu, na alikuwa anafikiria kununua gari. Kati ya haya lipi unaona linamfaa kwa budget isiyozidi 18M?. Mimi nilikuwa nafikiria haya, unaweza kuongeza unayodhani yanafaa zaidi.
Forester 2007 (najua 08 ndio bora zaidi lakini budget ndio tatizo)
Nissan xtrail.
Hii rav 4 ina amani gani ikishaanza yale matege mkuu...?Rav 4 old model. Achana na nissan achana na subaru. Mtafutie gari litakalompa amani
Tatizo watu hawayahudumii magari yao vizuri, mjomba wangu anatumia hiyo RAV 4 old model tangu astaafu na kila xmass inaenda moshi hadi leo ile gari haina matege ipo kwenye hali nzuri kabisa na plate number yake ni ya muda tu namba AX...Huwa nashindwa kuelewa kwanini wengine za kwao zina matege!!Hii rav 4 ina amani gani ikishaanza yale matege mkuu...?
Hakuna gari linalomnyima mtu amani endapo una hela za kulifanyia ukarabati wa spea genuine....kuzingatia service zenye ubora, matunzo binafsi...
Hizo subaru na Nissan kuna watu wanazo mwaka wa 8 sasa na wanapeta coz wanazingatia masharti yake na matunzo
Bila hivyo hata hiyo rav 4 mnayoiona ni jembe, itamshimda....kuna watu wengi ninaona zimewashinda
Point hapo ni kuwa...mjomba wako anajiweza na ni mtunzaji.....hakuna gari baya duniani endapo wewe ni mtunzaji na una uwezo wa kulinunulia spea original kwa wakati...Tatizo watu hawayahudumii magari yao vizuri, mjomba wangu anatumia hiyo RAV 4 old model tangu astaafu na kila xmass inaenda moshi hadi leo ile gari haina matege ipo kwenye hali nzuri kabisa na plate number yake ni ya muda tu namba AX...Huwa nashindwa kuelewa kwanini wengine za kwao zina matege!!
I appreciate that! Ishu kubwa naamini ni utunzaji wa gari na kuchagua gari kutokana na matumizi yako tu!! Ila still hakuna gari baya!Point hapo ni kuwa...mjomba wako anajiweza na ni mtunzaji.....hakuna gari baya duniani endapo wewe ni mtunzaji na una uwezo wa kulinunulia spea original kwa wakati...
Na hakuna gari baya la kampuni ya Toyota kama RAV 4 ikikutana na mtu mwenye hela kiduchu, bahili na ambaye si mtunzaji.....hapo ndiyo utagundua bora IST kuliko RAV 4..
Na ukitaka kugundua dalili ya kwanza kwa mtu ambaye RAV imenshinda, utaona matege ya kutosha...kisha mtumiaji atalalamika ulaji wa mafuta kwenye ile 3s engine.
Ushauri wangu kwa mstaafu....ni bora achukue Noah old model yenye 3s injini coz itamfaa kwa safari, nafasi ya kutosha ya mizigo na familia...pia kama ana bishara za maduka inaweza kubeba mizigo mingi ya maboksi ...bora noah kuliko RAV 4 old model yenye injini ile ile 3s, nafasi ndani kiduchu imebana mwisho watu 5 bora hata spacio new model ina uwezo wa kubeba abiria 7..
Mtazamo wangu.
Mkuu chukua toyota rush. Gari inafanana na rav4 kwa size ni ndogo kidogo sana. Ila engine yake ni 1500cc, ulaji wa mafuta ni sawa na probox ila ni gari ya hadhi ukilinganisha na raum na zingine. Pia ni gari ipo juu hata bush unakatiza nayo bila shida.