Naomba ushauri: Hati ya kiwanja ni ya mke wangu pekee au naweza kubadilisha majina?

Naomba ushauri: Hati ya kiwanja ni ya mke wangu pekee au naweza kubadilisha majina?

Nkulu wa nchito

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
1,112
Reaction score
1,429
Wana jukwaa habari zenu
Mimi na mke wangu tumefunga ndoa miaka kadhaa iliyopita na tulikuwa tunaishi mikoa tofauti kuna kipindi aliniambia tununue kiwanja nikamwambia sawa basi wakati nipo mkoa ambao nilikua nafanya kazi akasema tuchange hela tununue akanitajia bei nikatoa nae akatoa huko alipoenda alikuwa na mama ake mzazi wakanunua mimi kipind chote hicho sikuwahi kuulizia hati ya kiwanja lakini kwenye kiwanja nimefika mara tatu.

Sasa toka mwaka jana nikawa namwambia nataka kuiona hati ya kiwanja. Juzi kanionyesha nimekuta kaandika jina lake tu halafu mashahidi ni mama ake na wengine kawaandika hapo sasa nauliza je naweza kubadili hii hati nikaandika majina mawili yaan jina langu na lake
 
je naweza kubadili hii hati nikaandika majina mawili yaan jina langu na lake
Hapo jibu ni moja tu, nenda ukauze kiwanja kisha unaemuuzia akuuzie tena upya ndio utaandika majina yako na majina yake

Yaan hapo huwezi kufuta jina kwenye hati limeshaandikwa mchakato ni kumuuzia mtu kisha yule akuuzie tena upya ndio unabadirisha majina mnaweka majina yenu wote, lakini sababu ni nini haswa mpaka unataka kufanya hivyo kwani mkeo haumwamini?
 
Back
Top Bottom