Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Muongezee muda wa mkataba ukishapata hela unayoitaka mwambie unauza pikipiki ujilipe hela unayo mdai.
 
Tambua kwamba ushapigwa hiyo hela, next time usiache deni liwe kubwa...
 
Ongea naye kisha chunguza
 
Kwa hapo mulipofukia nenda polisi tu
 
Hiyo ishakuwa ni hasara tayari ukitaka kuipata hela yako ni mpanga umfungulie kesi na bado unaweza usiipate hiyo hela pia

Chukua pikipik
 
HILI KOSA LILIANZIA SIKU YA KWANZA... KURUHUSU DENI LA MWEZI MMOJA... HUTAKIWI KURUHUSU DENI HATA LA SIKU MOJA... HAPO HAPO UNAVUNJA MKATABA... LAKINI UKILIMBIKIZA... BAADAE UNAUMIA WEWE...
 
Sio yangu mkuu nimepewa niisimamie tu maana mwenyewe yupo mbali, kuirudisha bila angalao hata nusu ya hesabu anayodaiwa sasa mwenye mali atanielewa kweli
Hufai kuwa kiongozi,bodaboda mmoja tu kakushinda kusimamia ukipewa kiwanda utaweza,u litakiwa umpe hesabu ya wiki sio mwezi,huwezi kukaa na hela mwezi mzima,alivyozingua mwezi wa kwanza ulitakiwa kumnyanganya chombo,sasa imefika miezi mitatu,aliywkupa chombo atakuzarau au hatokuamini tena
 
Kubali hasara uliyopata uchukue bodaboda kwa kumsamehe hiyo hela au uendelee kupata hasara...maana miezi 3 yote sijui ulikubali vipi akae muda wote huo hajaleta hela
 
Kama una mkataba wa kisheria, basi chukua hatua za kisheria mkuu
 
Mkuu ndo utaratibu niliokuta huku mkoani nishawahi kusimamia dereva dar ilikua analeta hesabu kwa wiki ila huku madereva wote wanataka kwa mwezi hata mimi pia nakumbuka nilikataa hili suala la hesabu kwa mwezi nikamwambia mwenye chombo hesabu inabidi kwa wiki aksema wiki dereva anaweza akakwamba nikamwambia basi iwe wiki mbili maana mwezi mmoja ni parefu muda uwe mfupi ili akiwa mbabaishaji ijulikane mapema ila nikafatilia nikaona ndo utaratibu wa hapa huo hata mwenye chombo anajua hesabu inafatakiwa kwa mwezi alikwepo kipindi mkataba unasainiwa
 
Wewe ni msimamizi wa hovyo. Hakuna jambo jingine huyo ndugu yako atakupa usimamie.
Alinikabizi nimsimamie baada ya yeye mwenyewe kushindwana nae alafu huku mikoani hali ni tofauti na dar nilipopazoea, hawa bodaboda kama ujawahi ku-deal nao ni rahisi sana kutoa lawama kwa msimamizi wake
 
HILI KOSA LILIANZIA SIKU YA KWANZA... KURUHUSU DENI LA MWEZI MMOJA... HUTAKIWI KURUHUSU DENI HATA LA SIKU MOJA... HAPO HAPO UNAVUNJA MKATABA... LAKINI UKILIMBIKIZA... BAADAE UNAUMIA WEWE...
Sio deni lote la kwangu kuna deni jingine nimerithi kwa mwenye mali aliniachia nimfatilie bodaboda akiwa bado kiasi fulani cha pesa hajaleta kwa makubaliano akilipwa hela yake ya ujenzi anamalizia yote hayo mwenye mali anajua
 
Pole uko mkoa gani mkuu?
 
Kubali hasara uliyopata uchukue bodaboda kwa kumsamehe hiyo hela au uendelee kupata hasara...maana miezi 3 yote sijui ulikubali vipi akae muda wote huo hajaleta hela
Nimeachiwa nimfatilie akiwa ana deni mwenye chombo ilitakiwa kusafiri ndo akaniambia niwe namfatilia
 
Pole uko mkoa gani mkuu?
Nipo iringa, nimeona bora nichukue pikipiki ipaki tu amekuja na mke wake ambae ndio alikua shaidi wake kipindi tunasaini nikamwambia anipe funguo tunavunja mkataba, kwa mara ya kwanza maisha yangu mtu mzima kabisa pamoja na mkewe wamenipigia magoti mpaka wanatoa machozi kuniomba niwavulie., nimeumia kinoma lakini sina jinsi nimekataa ombi lao nimechukua chombo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…