Naomba ushauri kuhusu huyu bodaboda

Kwa akili zako fyatu za kumsubiri bodaboda akulipe malimbikizo miezi mitatu yote trust me, hufai hata kusimamia ugawaji wa soda kwenye msiba uko kijijini
Ni ni vyema ukauliza vizuri kuliko kutoa lugha ambayo sio nzuri., by the way shukrani kwa mchango wako mkuu nashukuru sana mkuu
 
Kawaida asipoleta pesa ndani ya siku 10 ndio mkataba unavunjwa bhana au 15 na hapo hamdaiani

sasa huyu jamaa anaomba ushauri wakat angerejea kusoma mkataba unasemaje
Nilipewa nimsimamie na mmiliki wa pikipiki maana yeye ana safari na atakaa muda mrefu kipindi napewa jukumi la usimamizi kulikua na balance ambayo bado dereva hajaleta na huku mikoani ndo utaratibu wa hesabu inaletwa kwa mwezi mimi pia nilivyosoma mkataba nilishangaa nikamwambia mwenye pikipiki ili suala sio sawa inabidi hesabu iletwe kwa wiki akaniambia ndo utaratibu wa huku ulivyo
 
Sawa mkuu
 
Gari ukimkabizi dreva tabu
Pikipiki nayo tabu
Bus nayo tabu tu

Madreva wengi wao hawana uchungu na mali ya tajiri. Anachoangalia masilahi yake (salary and Posho) hata akilibamiza, akilinokisha injini sawa tuu, si gari sio lake!! So, anajua tajiri yupo atalitengeneza ama atalifanyia overhauls kwa gharama zake. Lakini kuna madereva wengine wanajitambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…