Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
usijaribu kuingia kilimo cha greenhouse (hema) ni utapeli. kuhusu kulima bora ulime tikiti. nyanya bei yake inabadirika haraka na haitabiriki. pia tikiti unaweza safirisha hata soko la mbali.Iko hivi, nimejipanga kufanya kilimo cha umwagiliaji msimu wa kiangazi. Nina shamba ekari 4. Natarajia kiangazi kikianza nichimbe maji then nifunge pampu. Nitakuwa napandisha maji kwa generator kwenda kwenye simtank alafu namwagilia kwa mipira (drip irrigation). Sasa kuna mambo yananichanganya kiasi.
N.B: Sitalima kwenye Green house kwa sasa, nitatumia open system, lakini nitazungushia shamba langu fence kwa ajili ya usalama. Pia kwa sasa nimelima mahindi kwa sababu nilikuwa nasafisha shamba na kutoa visiki. Natanguliza shukrani.
- Je, nilime nyanya au tikiti maji.? Nimekuwa nikifuatilia mahitaji ya haya mazao, na kwa eneo langu zao lolote kati ya haya linakubali. Swali langu, nahitaji kulima zao ambalo litakuwa cost effective lakini liwe na uzalishaji mkubwa kwa kila ekari. Naomba wazoefu mnisaidie, Je, kwa ekari moja nikilima nyanya nitapata mkwanja kiasi gani, na nikilima tikiti nitapata kiasi gani. Tupieni na uzoefu wa marketing, ipi ni rahisi kuuzika. Tukadirie kwamba other factors remain costant.