Naomba ushauri kutokana na changamoto ninazopitia ofisini ninapofanyia kazi

Mboka man

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
478
Reaction score
1,647
Nina kama week mbili tangu nianze kazi ila kuna changamoto ninapitia hapa

1. Changamoto ya kwanza kuna supervisor full time kunifanyia visa mara kila saa natishiwa kufukuzwa kazi

2. Work mate niliokutana nao ofisini hawanipi ushirikiano vitu vingi vya msingi hawanielekezi

3. Upande wa boss wangu ambae alikuwa anakubali utendaji wangu wa kazi sasa hivi kanibadilikia full kunifokea full kupewa maonyo kuhusu kufukuzwa

4. Ofisini nipo kama mwana mkiwa naona kama niko motoni lawama na vitisho vimekuwa vingi

Hapa nilipo sijui hatma yangu katika hii ofisi.
 
Wanakufokea tu bila sababu??? Wewe ndio unaleta sababu za kufokewa so jitahidi ufanye kazi inavyotakiwa kuepuka makosa mara kwa mara ili wakose nafasi ya kukufokea na visa.

Ukiwa ofisi mpya sharti uwe mchangamfu ili wakuchangamkie ukijitenga hakuna wakukusogelea watakuacha hapo uhangaike mwenyewe
Changamka!
Jichanganye!
Jifanye mjinga
Jipendekeze
 
Nina kama week mbili tangu nianze kazi ila kuna changamoto ninapitia hapa

1.changamoto ya kwanza kuna supervisor full time kunifanyia visa mara kila saa natishiwa kufukuzwa kazi

2. Work mate niliokutana nao ofisi hawanipi ushirikiano vitu vingi vya msingi hawanielekezi

3.Upande wa boss wangu ambae alikuwa anakubali utendaji wangu wa kazi sasa hivi kanibadilikia full kunifokea full kupewa ma onyo kuhusu kufukuzwa

4.ofisini nipo kama mwana mkiwa naona kama niko motoni lawama na vitisho vimekuwa vingi

Hapa nilipo sijui hatma yangu katika hii ofisiii
Soma kwa majibu job description yako na utekeleze kazi kwa mujibu wa hiyo job description utawasambarayisha
 
Nina kama week mbili tangu nianze kazi ila kuna changamoto ninapitia hapa

1. Changamoto ya kwanza kuna supervisor full time kunifanyia visa mara kila saa natishiwa kufukuzwa kazi

2. Work mate niliokutana nao ofisi hawanipi ushirikiano vitu vingi vya msingi hawanielekezi

3. Upande wa boss wangu ambae alikuwa anakubali utendaji wangu wa kazi sasa hivi kanibadilikia full kunifokea full kupewa maonyo kuhusu kufukuzwa

4. Ofisini nipo kama mwana mkiwa naona kama niko motoni lawama na vitisho vimekuwa vingi

Hapa nilipo sijui hatma yangu katika hii ofisi.

Labda kiwango cha Elimu yako kinawatisha.
 
Ulipewa job description?? Fanya ujasusi mkuu 😊 unaweza kua CHOCHOTE ukiamua......
 
Tuanzie kwa Boss, alikusifiaje utendaji wako wa kazi hapo awali ikiwa hata kazi yenyewe hujui kutaka wenzio wakuonyeshe.

Ninachohisi mimi uliingia kazini na mbwembwe nyingi za kuwa ni mtaalam wa kazi.
Itakuwa Boss alitangaza ujio wako kwa sifa nyingi baada ya kudanganya kwenye CV yako na hii ilikutengenezea mazingira ya kuwa tishio 'threat' kwa wafanyakazi wenzio kupelekea chuki. Binadamu tuna kawaida ya kuchukia wale tunaowaona tishio kwetu.

Sasa baada ya kuona uhalisia ndio maana mambo yamebadilika.

Kazini sio sehemu ya kutaka upendo, upendo kautafute nyumbani na Agape.

Kwa dalili zilizopo hapo hutopaweza, komaa komaa huku ukitafuta ustaarabu mwingine.

Tuachage kudanganya kwenye CV zetu. Ndio yale mambo ya kuandika kwenye CV kuwa unajua French unaajiriwa anakuja mfaransa unaanza kuongea mistari ya Awilo Longomba, Je M'appelle kupe kupe ndibamba.
 
Nina kama week mbili tangu nianze kazi ila kuna changamoto ninapitia hapa

1. Changamoto ya kwanza kuna supervisor full time kunifanyia visa mara kila saa natishiwa kufukuzwa kazi

2. Work mate niliokutana nao ofisi hawanipi ushirikiano vitu vingi vya msingi hawanielekezi

3. Upande wa boss wangu ambae alikuwa anakubali utendaji wangu wa kazi sasa hivi kanibadilikia full kunifokea full kupewa maonyo kuhusu kufukuzwa

4. Ofisini nipo kama mwana mkiwa naona kama niko motoni lawama na vitisho vimekuwa vingi

Hapa nilipo sijui hatma yangu katika hii ofisi.
Anza kutafuta kazi sehemu nyingine.
 
Wanakufokea tu bila sababu???
Wewe ndio unaleta sababu za kufokewa so jitahidi ufanye kazi inavyotakiwa kuepuka makosa mara kwa mara ili wakose nafasi ya kukufokea na visa.

Ukiwa ofisi mpya sharti uwe mchangamfu ili wakuchangamkie ukijitenga hakuna wakukusogelea watakuacha hapo uhangaike mwenyewe
Changamka!
Jichanganye!
Jifanye mjinga
Jipendekeze
Unakuta umemaliza kazi zako huna kitu cha kufanya umetulia boss akikuta umetulia huna cha kufanya anaanza kukufokea kwanini umekaa idle

Ukimwambia umemaliza majukumu yako ukoo free anakutafutia kazi yeyote ya kufanya hata kama ikoo njee ya majukumu yako
 
Amini katika ufanisi wako na ufanye majukumu yako kama inavyopaswa. Kazi yako ndio iwe sifa yako.

Usitarajie urafiki ama kupendwa, hapo kila mtu anaangalia maslahi yake na yeyote anaehisi maslahi yake yapo matatani lazima ataleta chuki, rejea supervisor wako.

Usijikweze sana kuwa wewe unajua zaidi hilo litapekea kuchukiwa zaidi.

Boss sio rafiki yako, usitarajie upendo wake kwako, yeye anataka nguvu na ufanisi wako tu kama vile wewe unavyotaka ujira wako.
Mpe ufanisi wako ili akupe ujira wako. Mambo ya kupendwa muachie mpenzi wako.

Muhimu zaidi ni amani ya nafsi yako. Sifa ya kuiona kazi nzuri ni kufanya katika mazingira yanayokupa amani. Ukikosa amani kazini ni sawa na kuwa jela tu.

Kazi mbaya ukiwa nayo, hivyo komaa hapo ulipo huku ukitazama njia mbadala. Sikushauri kuacha kazi kabla kupata kazi.

Mwisho, muweke Mungu wake mbele kila hatua. Usitoke kwako kwenda kazini kabla kumuomba Mungu wako akuepushe na shari.
Utastaajabu ni mangapi yanafanyika na watu makazini (ushirikina) kutetea nafasi zao, bila ya Mungu ni ngumu kutoboa.

Kila la heri.
 
Back
Top Bottom