Tuanzie kwa Boss, alikusifiaje utendaji wako wa kazi hapo awali ikiwa hata kazi yenyewe hujui kutaka wenzio wakuonyeshe.
Ninachohisi mimi uliingia kazini na mbwembwe nyingi za kuwa ni mtaalam wa kazi.
Italian Boss alitangaza ujio wako kwa sifa nyingi baada ya kudanganya kwenye CV yako na hii ilikutengenezea mazingira ya kuwa tishio 'threat' kwa wafanyakazi wenzio kupelekea chuki. Binadamu tuna kawaida ya kuchukia wale tunaowaona matishio kwetu.
Sasa baada ya kuona uhalisia ndio maana mambo yamebadilika.
Kazini sio sehemu ya kutaka upendo, upendo kautafute nyumbani na Agape.
Kwa dalili zilizopo hapa hutopaweza, komaa komaa huku ukitafuta ustaarabu mwingine.
Tuachage kudanganya kwenye CV zetu. Ndio yale mambo ya kuandika kwenye CV kuwa unajua French unaajiriwa anakuja mfaransa unaanza kuongea mistari ya Awilo Longomba.