Naomba ushauri: Mchepuko wangu ameolewa leo, nimekubwa na msongo wa mawazo

Haya mambo ya uzinzi ndio yanasababisha ndoa nyingi siku hizi kuwa jehanam maana watu mnajisifu kabisa kuwa na michepuko.
Kabla hujanitazama mimi kwa kunihukumu jitazame moyoni kwako kama u msafi kuliko mimi.
 
MIMI nadhani inabidi uiheshimu ndoa yake kama yeye alivyokuwa anaiheshimu ndoa yako...amesha kuwa mke wa mtu...na wewe ni mume wa mtu...ni vibaya sana kuharibbu ndoa ya watu kwa sababu zinazozuilika ni bora ukatafuta mchepuko mwingine...!
 
....i used to be the other man, now it's flipped i dont want you with another man....Nelly.
 
Mimi niliona sio vema kumkataza asiolewe maana mimi nina mke, lakini huyu mdada tulielewana sana, aliheshimu ndoa yangu sana, alikua mshauri mzuri mpaka kwenye masuala yangu ya kifamilia na kikazi.
Upuuzi mtupu... Yaani unashindwa kumshirikisha mkeo kwa kumdharau kuwa hawezi toa ushauri katika nyumba yenu unajidai kumuona huyo mchepuko ndo mshauri wako...

Sasa subiri huyo mchepuko wako aje akulalamikie kuwa mme wake hamshirikishi hapo ndo UKAE UKIJUA KUWA HATA MKEO ANASIKILIZWA AKITOA USHAURI KUSAIDIA FAMILIA YA MCHEPUKO WAKE.
 
watu wachache kama nyinyi na huyo mchepuko wako ndio mnafanya hii dunia watu waone ina machungu na kuchukia mapenzi wakati mwingine kuuana wewe badala ya kuachana naye kipindi yuko kwenye uchumba ulikua bado unaye kaolewa na bado utaendelea kuwa naye...huna aibu na akili watu kama nyinyi mnastahili kifo
 
lakini mbona ameonesha bado anaupendo kwa mke wake hilo haujaliona mpaka hata amekataa kumuoa huyo mwanamke.
hujamuelewa anachosema, ni kwamba wanaume mnasemaga mnachepuka kwa tamaa bila hisia lakini mleta mada ana hisia nzito sana juu ya mchepuko wake.

Ndo mjue wapo pia wanawake wanaochepuka bila hisia na mapenzi yanabaki kwa waume zao.
 
Pole sana kwa mkeo na kwa jamaa anayejichukulia bomu...

Unarudi nyumbani na stress, mkeo anakubembeleza akijua ni mambo ya kazi kumbe mchepuko kaolewa...

Jamani ndoa, ndoa hizi ndoa jamani!!!
This thing called marriage is just stupidity
 
Mmmh wanawake walio kwenye ndoa weng wanateseka jmn. Hpo hasira zote utahamishia kwa mke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…