Naomba ushauri: Mchepuko wangu ameolewa leo, nimekubwa na msongo wa mawazo

Tofautisha kati ya tamaa na upendo ingekuwa ni tamaa tu asingeumia huyo mwanamke kuolewa ila kwa vile ni mapenzi ndo maana kaumia haijalishi kama bado anampenda mkewe au la hapo tatizo ni kwamba kampenda na mchepuko wakati mnasemaga huko nje huwa hampendagi
lakini mbona ameonesha bado anaupendo kwa mke wake hilo haujaliona mpaka hata amekataa kumuoa huyo mwanamke.
 
Wewe roho inakuuma kuona leo kuna jamaa anaenda kukesha pale unapopumzikaga.
Ni wivu tu huna stress hapo.

Stress ni hapo usikie mkeo anachepuka halafu hujamkamata na kumuuliza unaona jau kwa anavyokuheshimu.
 
Kuna mwingine anakaa hpo mtaa wa chin mchukue awe mshaur wako
 
wa kushauriwa na kuonewa huruma ni huyo aliyemuoa mkeo mdogo. maana lazima atalea watoto wasio wake, yaani watoto wako
 
Jianamke linakuganda ulioe ili litoe nuksi na kupigwa chapa ya married kumbe nyuma ya pazia limeishi kwa mapenzi makubwa na mwanaume mwingine tena hata kuachana ni basi tu haikuwa na namna, sasa hapo unategemea hiyo ndoa kudumu kweli!,
 
Nimekurupuka nikajua mkeo ndo anaolewa kumbe mchepuko.HAYA NI MATUMIZI MABAYA YA UANAUME.
 

Kuna kuchepuka ile mara moja moja (one night stand) hapo hamna feelings za mapenzi ila tamaa, na kuna ule mchepuko wa kudumu, huu kusema ukweli kuna mapemzi flani yapo hapo ndio maana tunahonga n.k ila mke anabaki kuwa mke hamna namna mwanaume atamchagua mchepuko wake badala ya mke ikitokea anatakiwa kifanya maamuzi
 
Muhadithie mkeo akupe ushauri
 
Dah!!!... Wanaume wenzangu mnazidi kumpa point 3 shetani..
Hivi kweli kabisa una ndoa yako halafu unakuja kuomba ushauri tukushauri kuhusu mchepuko wako, that means tunashiriki kuharibu ndoa yako indirectly...
Mi Nakushauri nenda kanisani kaombewe na utubu.. Umuombe sana Mungu akupe roho ya kumuogopa na kumuona kila ufikiriapo uzinzi...
Kisha nenda nyumban muite mkeo mwambie akae muangaliene Kama dakika mbili bila kukwepesha macho na muda huo ujisemee kimoyomoyo akusamehe Kwa kwenda kinyume na kiapo chenu... Ujumbe utamfikia maana nafsi zenu zitaongea kimyakimya... Kisha ukimaliza umpende mkeo...
Utahisi naongea ujinga... Ukiona Vipi potezea halafu endelea kuchepuka na mke wa mtu.. Ila ujue naww una mke..
Good morning
 
Hata kwa wanawake pia ni hivyo hivyo
 
Shost eeh utajipa stress bureee,wengi wanaokoment humu nimegundua ni vitoto vya sekondari na vyuo,wanapass time to, that's y hata kushiriki minakasha humu nimepunguza kwa asilimia 90,nimeona ntajipa kisukari buleee kusoma ama kujadil mada za kisekondari kila leo
 
Hahahahah anataka tumfariji,kila Leo wanasema michepuko ni kwaajil ya tamaa,ni wa kutumiwa na kusepa,sasa sijui mwanaume huyu yamemsibu yepi ama yeye sio kama hawa wanaume wa jf ambao wanawatumia michepuko,wanapiga na kusepaaa?hahahah
Hahaha labda kajisahau kajua yuko Facebook. Amesahau kuwa wanaume wote wa Jf hawababaishwi na wanawake hata wakiachwa hawaumii sana sana wanakuwa wamepewa nafasi ya kuvuta chombo kipya, na hata wakitaka mchezo kutoka kwa ma ex wao ni fasta tu hata kama wameolewa. Mkaribishe mgeni Jf
 
Ni kweli aisee mimi siku hizi sijisumbui kubishana na mtu kwa facts, kama nitatoa fact basi ni kwa ufupi maana nimegundua kuna watu wapo kwaajili ya kutujaza upepo na mimi kujaa nimegoma
 
Hahahaaaahhahhaha stress za nini??? Si alikuomba umuoe mke wa pili uligoma??? Acha balaa relax
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…