seriousman
Member
- May 29, 2019
- 17
- 20
Habari zenu wadau wa Jamiiforums.
Ni mara yangu ya kwanza kutuma ujumbe wenye maudhui kama haya hapa jukwaani.
Naomba mnipe ushauri jinsi ya kukabiliana na stress zinazonikabili.
Suala liko hivi; mwaka jana Oktoba mpenzi (mchepuko) wangu alipata mchumba akaja kuniuliza nikubali au nikatae asiolewe.
Mimi niliona sio vema kumkataza asiolewe maana mimi nina mke, lakini huyu mdada tulielewana sana, aliheshimu ndoa yangu sana, alikua mshauri mzuri mpaka kwenye masuala yangu ya kifamilia na kikazi.
Kuna wakati alikua akinishawishi nimuoe awe mke wa pili, lakini sikuwahi kuwaza kuwa na mke zaidi ya mmoja hivyo nilikataa, akasema sio shida anataka tuendelee kuwa wapenzi no matter what.
Sasa baada ya kumshauri akubali kuolewa, kweli jamaa mwezi Januari akaleta barua, kisha taratibu zote zikafuata.
Sasa leo ndio siku wapo wanafunga ndoa, kuna bonge la sherehe, dada zake (shemeji zangu) wamenipigia simu niende, rafiki zake wa karibu wa kazini kwao wamenipigia simu niende lakini moyo umeshindwa kabisa japo zawadi nilinunua nikampa rafiki yake akapeleka.
Wakuu huyu mwanamke ameolewa kwa ruhusa yangu lakini nimepata stress tangu juzi kila ninachofanya hakiendi, kila ninachoshika hakiendi, yaani nahisi kama akili zangu zimesimama kufanya kazi.
Nisadieni namna ya kukabiliana na hali hii ndugu zangu. Naomba msinitukane, msinihukumu wakuu, nisaidieni natokaje kwenye huu msongo wa mawazo.