Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Umeongea vyema sana mkuu, hakika umeonyesha ukomavu ushauri mzuri sema sijui kama ndugu yetu huyu ataupokea, ni heri anaekushauru kwa kukuponya ingawa inauma kuliko anaekushauri kinafiki na kuukubali ujinga unaoufanya
 
Namuona huyo mwanamke mwenye miaka 42 atavyozeeka bila mume.....kweli mume wa mtu sumu.
Sumu yake ni nini?
Hata mke wa mtu ni sumu,

Lakini wewe mwenye mume wa mtu, wewe ni nani zaidi ya hao tunaowaona mitaani hawana waume na wako tayari kutembea na mtu yeyote
Kutokana na hali ya maisha, na bi mdogo ambaye, unapata huduma zote na unajaliwa?

Ila kumbuka hata wewe mwenye ukileta upuuzi kama huo utatimuliwa tu , hakuna excuse kuwa wewe ni mke wa ndoa
 
Mie nahisi kama ushauri wako sio realistic kama unavyomtaka mleta mada awe realistic. Haya ni maisha and we live once. Huyo unayemuita "mchepuko" naye ni binadamu na ana moyo wa nyama unaoumia kama binadamu mwingine. Binafsi ndoa ni ule uridhiano wa wawili kuishi pamoja. Hayo mengine ya kanisani au misikitini ni makaratasi tu na formality za kumanipulate ubongo wetu uamini kuwa ndoa ni hicho kipande cha karatasi. Bi mdogo na bi mkubwa wote wana nafasi sawa tu. Wote ni wanawake na wote wamezaa na jamaa. Hicho kikaratasi cha ndoa hakimfanyi bi mkubwa kuwa tofauti na mwenzake. Hebu niambie tofauti ni ipi kati ya bi mkubwa na bi mdogo ukiweka pembeni hicho cheti cha ndoa? Wote ni wanawake, wote wamezaa na wote wanapendwa na mleta mada.
 

Inategemea sana mkuu, ndugu wa kuzaliwa nao sometimes na wao ndo walewale, binadamu tuna jema basi? Do ur part, muombe Mungu sana akupe maarifa na hekima then plan for your retirement days....
 
Naweka kituo hapa akija nitaendelea kabla ya kutoa ushauri
 
Huyo dada mjinga angemchuna bwana ajitengeneze empire yake atafte mume, sasa inaonyesha mke mzito kiuchumi na mwanaume sasa anaanza kuzeeka na akili ziinamrudia anaona arudi kwa bibi mkubwa wa kuzeeka naye, sasa bibi mdogo akitibua huyu mzee na akistaafu atakufa siku si zake, hafu nyumba za mitala hazijawahigi kuwa na amani loh. Huyu arudi KWA mke mkubwa tu Basi akiendelea na mchepuko atakufa siku si zake,
 
Ngoja amalize nimpe ushauri maana hata mimi mzee wangu ana wake watatu
 
Sio kanda ya ziwa tu weny

Da Ahsante sana ndugu, umenikuna, nilikuwa natafuta jibu, maana sumikukubaliana naye kabisa
 
Very true
 
Siyo kweli, hiyo empire angeitengeneza vipi, nilimchukulia kama mke hasa, na hana tofauti na mke mkubwa, na sasa hivi naye yupo over 40, ukisema mke mkubwa mzito kiuchumi, mimi naona vile vile sio sawa kwani yeye alikosa nini cha kumfanya asiwe mzito, wote wana nyumba na wote watoto wao wameenda shule,kusema mimi nimezeeka nayo sio kweli, kwa taarifa yaani sasa hivi, Mungu apitishie mbali ndio naanza kuona utamu wa maisha, hiyo naisikilizia hasa, nataka nianze sasa kutalii sehemu mbalimbali,

Na kwa taarifa yake nilikuwa nimejipanga kuzeeka naye kwa kuwa nilishaanza kumtafutia kiwanja huko jirani na kijijini kwetu ili kibeneke liendelee, hata gari ningemnunulia,

Halafu mbona namwona naye kama anamabadiliko ya kiutu uzima kulikomimi, kitu gani kinakufanya umwone yeye ni kijana zaidi yangu,
Kumbuka tumeachana miaka minane tu, ujana wote kamaliza akiwa na mimi, leo hii mimi nikienda Club natoka na mtoto wa 25, na wala haoni aibu kukaa na mimi, vipi yeye anaweza kutoka na mtoto wa 25 na akawa happy, au huyo kijana anaweza kuwa happy.

Ila tatizo lingine kubwa ni nalo liona nyinyi wanawake mna chuki na husuda kwa wenzenu wenye maisha mazuri, na hayo maneno yenu ndio chanson cha kuwaingiza chaka na kuharibu kabisa maisha yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…