Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Du , kusema sikuwa na la kujibu ilibidi nikawa chini kwanza nitafakari, akili haikunipa kabisa,

Suala sio kwa nini kanunua na kuficha hivyo vitu kwa ndugu yake, ila ni kuwa inaonesha sasa haya ni maandalizi ya kunikimbia na pesa zangu,

Sikumuliza chochote, ila baada nilikuwa kama najisemeshakuwa nimeota kama kuna mizigo unaleta hapa nyumbani, akasema ndoto tu hizo,

Baadaye tena nikamwambia mbona nasikia kuna vitu umenunua umehifadhi kwa ndugu yako, kwa nini usilete hapa? Akanijibu nimekuambia sijanunua kitu mimi, na nilishakukataza mmambo ya kusikia sikia huko nje usiwe unaniletea hapa, umesikia wewe,

Nikamwambia basi sio kusikia tu ila niliokotaga risiti hapa ndani ila sikutaka kukuambia, akasema nipe hiyo risiti, nikamwambia niliiacha hapa hapa, nikijua siku moja utaniambia

Akasema mimi sijui una niuliza kitu gani maana na wewe sasa hivi umekuwa mswahili kweli,

Aliendelea sasa kulalamika hasa kuwa namtuhumu kwa mamvo mengi,sasa mala sio mwaminifu mala mwizi, hivi kama hivyo vitu nimenunua, hapa si kwangu kwa nini nisilete hapa nyumbani,

Na wakati unaona hata magodoro hapa sio mazuri, na kitanda chenyewe cha zamani!
 
😂😂😂😂😂
Dah
 
😂😂😂😂😂
Salaleeeh!! We baba wewe
 
SASA NINI CHA KUFANYA:
Kwanza mzee wangu lazima uweke BOUNDARY/LIMIT. Huyo bi mdogo kashasahau nafasi yake, hivyo ni wajibu wako kumkumbusha vividly bila kumuangalia usoni.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 umenichekesha kingisimani uwiiii

Miaka 18 aweke boundary leo 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nadhani uzi ufungwe tuu, umeshamaliza kila kitu.

He have to be realistic kwamba huyo ni mchepuko tuu na anatakiwa akate connection naye za kimaisha, wabakishe connection kwenye watoto tuu.

Huyu mchepuko wake itafika muda atadai wawe na hadhi 50/50 na mke halali wa ndoa. Na kwa sheria zetu zilivyo tayari huyo mchepuko anatambulika kama mke halali wa jamaa na kimaslahi anatakiwa apate 50/50 na mke mkubwa.

Kaka mkubwa bado hajachelewa,anatakiwa achukue maamuzi magumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…