Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Watu viherehere Kaka,Mwitore wasikuharakishe,hawana ushauri wanataka umalize wakushambulie na,kukucheka.
Shunie
Epsy
Carha
Maya ETC
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]dawa hata ikiwa chungu shurti umeze Ili upone
 
Nadhani uzi ufungwe tuu, umeshamaliza kila kitu.

He have to be realistic kwamba huyo ni mchepuko tuu na anatakiwa akate connection naye za kimaisha, wabakishe connection kwenye watoto tuu.

Huyu mchepuko wake itafika muda atadai wawe na hadhi 50/50 na mke halali wa ndoa. Na kwa sheria zetu zilivyo tayari huyo mchepuko anatambulika kama mke halali wa jamaa na kimaslahi anatakiwa apate 50/50 na mke mkubwa.

Kaka mkubwa bado hajachelewa,anatakiwa achukue maamuzi magumu.
[emoji1666][emoji1666][emoji1666] anataka kuhalalisha mchepuko. Huyo mchepuko alimtega na jamaa akaingia lwenye 18. Wala hakuna mapenzi hapo
 
Acha kumdhihaki mwenye uhitaji wa ushauri,kuna siku utakuwa muhitaji utadhihakiwa na wewe
[emoji1][emoji1]life is too short to be serious that's why pressure zinawaua wallah, mi enjoying my life why should I bother kwa choice ya mtu alochagua na alijua matokeo yake
 
Kwa jinsi elimu nzuri ya sasa ilivyo ghali kama unayapenda mabao yako,ni heri kuwa na watoto wachache maana ukiwa nao wengi utakamuliwa hatari.

Yaani mtoa Uzi atateseka mpaka siku anaondoka duniani.
Usijifariji eti utastafu na utapata 250 mil hili sahau,kumbuka huyu fala wetu ametengeneza utaratibu Mpya,kuanzia 2023 watakaostafu watapewa kidogo kidogo.
Utauza viwanja mpaka basi.

Kuhusu watoto utawalea wao na wajukuu mpaka unaondoka duniani.
Kumbuka ajira zimekuwa ngumu,watazaa na kulelewa hapo hapo hao wajukuu.
Hata uwafungulie biashara,zitakuwa zinakufa tu,maisha ya sasa sio mchezo hasa ukiwa baba ambae atawajari sana watoto na kutaka kuona wanaweza simama wenyewe hapa lazima utatumia nguvu ambayo hata hukuwah itumia hapo kabla.

Kila la kheri mkuu
 
Mimi bwana hata sitaki kukuelewa baba yangu. Nisamehe bure. Sijaitambua imani yako mpaka sasa inayoruhusu wewe kuhalalisha MCHEPUKO kuitwa mke. Kwangu atabaki kuitwa MCHEPUKO tu. Mke gani anafichwa kama gunia la bangi.

Halafu mzee wangu katika calculations zako naona kbs umeshapiga hesabu jinsi mambo yakishabumburuka utakavyoanza tengwa maana unatolea mifano hai ya wanafamilia jinsi wamtelekezwa na familia zao wamebaki mama na watoto zao. Binafsi siwezi kukutenga kabisa hata ungekua umetutengaje.

Nikusifie kabisa katika wababa na wewe ni baba. You seem to be a very nice man, friend and father. Nachosikitika akiguswa MCHEPUKO unafura tu.
Nionacho.. MCHEPUKO WAKO NI FUNGU LA KUKOSA. Na mambo yake anajilinganisha na mke halali. Hakuna mke mdogo hapo. Labda tupunguze makali kwa kusema mzazi mwenzako.

Sijui ndo tuseme uchawi, sijui mahaba ama nini sijui. Sijui ni akili zako timamu uliamua iwe hivi sielewi. Ila ulikosea toka mwanzo. Na angeenda kusema kwa mke mkubwa ndo ingekua ahueni kwako. Ilivyo siri hivi ndo inazidi kuharibu. Ndo unazidi mpa nafasi huyu MCHEPUKO azidi kupata nguvu.

Kwa upeo wangu, huyu mchepuko amekua na wewe since day one kwa tamaa. Ulienda na gari ukiwa na nduguye. Akajuona na akajua una uwezo kumzidi nduguye sijui shemeji. Akaja kwako akajolengesha. Alishapiga mahesabu hapa ndo pa kuponea. Wewe unaamini anakupenda[emoji23][emoji23] this is so FUNNY... nakuhakikishia mnaishi kimazoea tu. Fulia mkose hela ya kula ndo utaelewa. Yaan mchepuko una nguvu hivi?

Halaf unakua mkali ukiulizwa juu ya mke mkubwa unampa muda saa ngapi kwanini. Hapa unaulizwa ili watu wabalance story wajue namna ya kukusaidia. Haijawahi kuwepo balance kwenye mapenz asilani. Hapa usituongopee. Kulipa ada na matumizi si kila kitu. Hapo uko hai. Ukadondoka kama leo watoto ndo wanapeleka vurugu na mchepuko kwa mke juu ya mali. Nasema tutauaanaaa...

Kabla hujamalizaaa... chukua mke.. nenda nae vaccation mwambie una mambo wataka mweleza. Mwambie A to Z. Sisi wanawake tukipenda huwa tunakua waelewa sana tukiambia ukweli. Mweleze kila kitu ili uwe huru. Najisikia huruma sana juu yako hakika maana kuhandle mambo makubwa hivi hapana.

Nilichogundua pia mke wako ana mkono wa baraka sana ndo maana Mungu anamjalia anapata sana. Zaidi nasikitika watoto qa mchepuko kukwambia eti si uende kwako. Kwahiyo wanaelewa kila kitu. Kama wangekua wanakuheshim wasingekua na la kusema asilani juu yako. Mama yao pia anawajaza ujinga.

Naomba ukamweleze MKEO kabla hayajamfikia kupitia watu baki usije jutia.
Nakuombea Amani ya moyo sana mzee wangu. Pole sana. Kuna mambo hukutokea na usijue yametokea aje. Kama ametumia nguvu za giza na alijua una ndoa Mungu adeal naye sawasawa na mapenz yake kwa kuvuruga mji wa mwenzake.

ACHANA NA MCHEPUKO. GHARAMA INAZIDI KUPANDA.
Agiza chochote kwa mangi hapo nakuja kulipa.

Kamwe mchepuko hauwezi kuwa halali kisa tuu mmezaa.

Mimi nimemshauri kama anataka awe official basi ni mpaka mke wake aridhie, tofauti na hapo huo utabaki kuwa mpango wa kando tuu.
 
Kwa jinsi elimu nzuri ya sasa ilivyo ghali kama unayapenda mabao yako,ni heri kuwa na watoto wachache maana ukiwa nao wengi utakamuliwa hatari.

Yaani mtoa Uzi atateseka mpaka siku anaondoka duniani.
Usijifariji eti utastafu na utapata 250 mil hili sahau,kumbuka huyu fala wetu ametengeneza utaratibu Mpya,kuanzia 2023 watakaostafu watapewa kidogo kidogo.
Utauza viwanja mpaka basi.

Kuhusu watoto utawalea wao na wajukuu mpaka unaondoka duniani.
Kumbuka ajira zimekuwa ngumu,watazaa na kulelewa hapo hapo hao wajukuu.
Hata uwafungulie biashara,zitakuwa zinakufa tu,maisha ya sasa sio mchezo hasa ukiwa baba ambae atawajari sana watoto na kutaka kuona wanaweza simama wenyewe hapa lazima utatumia nguvu ambayo hata hukuwah itumia hapo kabla.

Kila la kheri mkuu
Hii comment ina lengo gani mkuu
 
Back
Top Bottom