Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Ukiona mitala haina Amani jua mwanaume maskini huyoo!ishu sip amani au furaha hapa kutambulika km mke rasmi halali na haki zote za msingi apate.Kingine hao wenye ndoa za mmoja na kama hivi watoto michepuko kama yotee na mwingine ana ndoa kanisani na ana mke kimila mpk watatu hapo furaha iko wapi.Sisemi wenye mitala kua hawachepuki ila wakichepuko ni ukahaba na hulka maana wamehalalishiwa kuoa wanne kabisaa.huko kumchuna si akili pia uwe nayo..huyo alinogewa akazaa na tena akijipa moyo ataolewa mke wa pili.
Hakuna mume wa mke mmoja tukubali tukatae!Ingawa tunajipa moyo kua miye ni mke wa kanisani siachiki lakini wengi wanaishi for the sake of watoto tu!Kinaaafiki mnooo au Mali maana wakiwaza kugawana mtu anaona kuanza moja itakua jau!Au ndo Mme anakukimbia anadaaanga anarudi akizeeka anasubiri kufa kanisa lisimtenge.


Sent using Jamii Forums mobile app
Bwana mitala huwa shida tu vile watetea ume grow hyo environment na dini inakuruhusu, wengine tumekuwa haya mapicha nyumba ndugu twasoma huku mitandaoni tuna Bibi na babu, ba mkubwa na uncle's wanazeeka bila mitala na familia imara na wanazeeka Hadi uzeeni. To me multiple partners ni janga linalonyima watu wengi furaha ingawa watajidai mara mila, sijui Imani sijui blah blah, so mtu KWA hyo issue sioni huruma maana yalikuwa maamuzi dont Make people wakuhurumie kwa uamuzi wako wa maisha
 
Mwitore, mimi ni kaka yako mkubwa! Ni retired officer, ninacho takukushauri ni kwamba; mosi, usijilaumu kwa yaliyo kukuta. Hayo siyo mageni katika Dunia hii. Wanaume wote wenye nafuu ya kipato huwa yanawakuta haya. Huyo mwanamke alijilenge umpe mimba kwasababu alijua uwezo wa kumsaidia kulea huyo mtoto unao.

Pili, huyo mwanamke inabidi umwache kwa amani ! Unaachana nae taratibu wala usimwambie unakusudia kumwacha kwa faida ya watoto wako wasiathirike kisaikolojia. Wanawake wengi at 40s huwa very ambitious. Usipokuwa makini yatakukuta makubwa. Kimsingi dalili ya mawingu ni mvua. Alipo kuambia akuage wewe nani, jua kuwa amejiandaa kwa mapambano. Mpangie vyumba viwili kwaajili yake na watoto. Lakini punguza frequency za kwenda. Ikibidi usiende hata miezi miwili mfululizo ila matumizi mtumie kwa kutumia mitandao .

Mwisho, rudi kwa mkeo mkubwa 100%. Hujachelewa.
Ahsante
 
Jamani mambo na visa ni vingi sana kuliko mnavyo fikiri, naona comment nyingine zinachoma haswa,
Niombe nikate story short, nasubirie tu ushauri wenu,lakini toka huo mwaka 2018,
Alirudi nikamkubiria kukaa ,

Lakini visa nivikubwa zaidi, zaidi sana, mpaka nahisi kama ameheuka,

Nimeshaitisha Vinson’s zaidi ya nane,

Nimeshampiga mpaka jicho likataka kutoka

keshanipeleka polisi

Nimeshampleka ustawi wa jamii,
Ambapo alitaka tugawane nyumba baada ya kuuzwa

Nimeshafungua kesi mahakama ya wilaya

Tumehudhuliamala nane, nikaifuta baada ya kuona, mwenendo wake kama gakutegemea nitaanda mahakamani ili tuachane, ingawa keshanieleza mala kibao tuachane, nilivyofanya kweli akapooza sana

Ameendelea kwenda kwenye huko polini kwa nguvu bila ruhusa yangu zaidi hata mala 20

Ameshatangaza kwa majirani sana kwamba mimi sitaki wageni ingawa ni uongo, mpaka hapa nyumbani napachukia

Baadhi ya ndugu zangu wanamfahamu, hata mama yangu alishakuja kwake na akalala

Kutokana na visa vyake ndugu zangu hawampendi

Nilishawapeleka watoto nyumbani kwa bibi yao yaani mama yangu wakakaa huko kama wiki moja, na mmoja anasoma huku huko

Kila dalili hawapendi kukaa kule

Majina ya watoto niliyafuta kwa hati nikaweka yangu
 
13.- sasa tunafukuzwa kabisa kule nyumbani kwetu,
Namwona nwenzangu anasusua kuondoka, naagiza gari linafika saa kumi usiku, tunapakia mizigo by saa11 asubuhi, tunaondoka
Makao mapya tunafika saa saa mbili asubuhi asubuhi,


Milango miwili wa mbele mkubwa na wa jikoni
Nilinunua pale pale alaf, ile mieupe, sikumbuki vizuri bei yake ila nadhani ni kama 200000
Andika kama mwazoni aise
 
Naweza kusema alijisahau sana, side chick alichukua hisia zote Ila nakubali kitu kimoja, hakuacha familia nyuma, wengine hapa wametelekeza familia kabisa, watoto wameshindwa kusoma, mama amedevelop sonona lakini huyu kajitahidi pamoja na kuanguka hakusahau watoto, wamesoma na wana maisha yao. Hiyo ni point ya kuichukua, do whatever you do...usiache watoto kama yatima.

Tukumbuke tu kuwa wengi hapa dhambi ya uzinzi inatutafuna, nashangaa tukirusha mawe wakati tunaishi nyumba ya vioo.
Ni sahihi unacho kisema Mimi simlaumu Mzee kwa hayo aliyoyafanya kwa sababu Huyo mwanamke tayari alikuwa ameshafika nae mbali na kuwa na familia nae ...nacho mlaumu Ni kuendelea kumng'ang'ania Huyo mama hata pale ambapo Huyo mwanamke alipoanza kuonyesha dalili za kuwa adui wa maisha yake' .. hii Ni mbaya Sana kwa ustawi wa afya yake' na maisha yake' yote kwa ujumla
 
25–nikamwandikia message nipo hapo ulipo naomba tuonane, akakataa katakata, baadaye nikadanya nimeibiwa simu yangu ndogo yenye pesa naomba unitumie pesa angalau ya guest ili nioge na kulala kesho niondoke,
Hakunijibu tena,
Mpaka kesho yake asubuhi, akanitumia 50000 Lakini baada ya msg nyingi sana
Khaaaaaaaaaa

Ni upendo au Nini?
 
Kwanin wewe kila post unakua mtu wa kupinga tu oppose au negative why kama unaumia acha kusoma lazima? Dingilii yupo njema tu matunzo anatoa ata mungu awez muhukumu labda kwa matendo mengne ya tofauti we vipi ulitaman we ndo uwe mke mdogo uzitwange izo pesa
 
Mbona hujaja na I'd yako wanaume huu Uzi umewa touch you have to learn bila hvo uzeeni mtakufa siku si zenu,mna invest kwa michepuko mara wake mnajisahau nguvu zikiwaisha na mkifulia ndo janga
Hii yangu mbona, mi huwa mara nying msomaji hivo najua timbwili lako, hivo jiskie huru bibie!! Jiskie upo sebleni chumbani[emoji28]
 
27- namwomba yule rafiki ajaribu amwambie nina maongezi naye lakini, anajibu sisi tumekuja kwa shughuli ya mtoto, nikamwomba basi naomba niongee na wewe,
Akasema lakini nikupe simu ya mzee ili alinipe ruhusu ya kuongea na wewe,

Yule rafiki yangu alinivuta shati kwa ghafla bila kutegemea,
Akaniambia tuondoke, ‘kumbe mwanamke mwenyewe ndio huyu, mbona yupo,(primitive sana) mmm yaani mke wangu Primitive, aliishia tu kuniambia yule sio mwanamke wa kunisumbua mimi, yaani sio hadhi yangu kabisa, kwamba ana mwonekano wa kishamba hasa, acha tabia yake.
SIO MKE WAKO MKUU

NA NI KWELI KWA HAYA MATUKIO SIJUI HATA NGUVU YA KUMUITA MKE UNAIPATA WAPI!!!??

KUZAA HATA PANYA WANAZAA (MNISAMEHE WANAWAKE WENZANGU)
 
Watoto wake sasa ndio wamemaliza la saba, nikawatafutia shule nzuri huko kanda, nauli kwenda tu ukihumuisha vikorokoro vyote tokea hapa mpaka afike shule kwa mmoja sio chini ya 200000, bado ada ambayo kwa mmoja kila baada ya miezi 3 ni sh500000 na mwingine kila baada ya miezi 3 ni 450000, na wakirudi unatuma pesa kama 100000, kwa mmoja

Sio kwamba nina pesa nyingi kiasi hicho lakini waswahili wanasema maji ukishayavulia nguo huna budi kuyaoga,

Sasa umeshawaingiza huko inabidi tu waendelee na mimi meenyewe umri ndio nnasogemea, na kustaafu Ndio huko kunapiga hodi,

Vijana huko makazini ndio kila siku wanakuuliza ‘utastaafu lini ‘ wakikuona unakopa hata sh 100000 wanakushangaa kweli, maana wanajua una mabillion bank.

Hata ukiwaambia jamani nasomesha, wanakuuliza mpaka sasa hivi una somesha tu? Ee ulichelewa kuzaa, na anayekuuliza hivyo ana miaka 30 hata mke hana, sasa anafikiri mpaka apate mtoto wa 3 tu atakuwa na umri gani?
Mpaka mtoto wa mwisho amalize chuo,

Mimi sasa mwaka kesho mtoto wa tatu anamaliza chuo, na nitakuwa na 51 Mungu akijalia huyu wa form 4 naye amalize chuo nitakuwa na 55, sio mbaya sana

Ok
Sasa pesa ndio hiyo imepotea kwenye kuku,

Wazo lililoniijia haraka baada ya kutafakari sana ni KUPIGA BEI ILE NYUMBA,

Sasa nitamshawishi vipi mwenzangu? Ikawa sasa ni ishu.
Ukitilia maana pale ameshakaa zaidi ya miaka kumi, na ameshajenga mtandao wa kutosha na akina mama wenzake wenye nyumba na kulinga juu,

Ila sasa kabla ya yote hayo kuna mambo yalikuwa yananiudhi mimi binafsi mpaka nikawa naona wazo la kijana linapata nguvu, alikuwa anapenda sana kusifisifia nyumba za watu, kuanzia nyumba imeisha vizuri, ina garden, mala gari nzuri, ingawa hata mimi nilikuwa na gari ya kutembelea baadaye nikaipiga bei,

Mala watu wanamsema kwa kuwa yeye ni binti mdogo kwa nini anakubali kuwa nyumba ndogo, na hivyo vyote ananieleza,
Mimi nikawa namjibu wewe angalia familia yako, kama ni watoto unao, kama shule nzuri hata watoto wako wanasoma shule nzuri, wakati meingine hata kuwazidi wakwao, una as vizuri, mimi nakupenda, unakula vizuri, na hili la kula kuna hata ndugu waliolewa kabisa makanisani , wakija kumtembelea pale Ndio huwa kipindi cha kubadili mboga,

Sasa nikiona amezidi namuuliza niambie hapa wanaokusema wewe, alivyonitajia mpaka nikashangaa, mmoja mme kwa mwaka anakaa hapo nyumbani kwa wiki mbili tu, mwingine mmewe alishafariki muda mwingi yupo baa, mwingine na mume wake wapo wanauza genge la nyanya pamoja. Watoto hata nguo za kushindia shida Mwingine kila siku na mumewe ugonvi, sasa namuuliza wanakuzidi nini hao mpaka uumie na maneno yao,

Nikamwambia PENDA MME NA WATOTO WAKO, hayo mengine ni mwembwe tu za hapa duniani, maisha ni wewe mwenyewe unayachukuliaje, ukiwa wanazidi waambie mimi nampenda huyu huyu.

Lakini nikaona tena yanazidi, mala mume wa mama fulani anasema wewe mbaya sana mbona umekutana naye bars Arabia hukumsalimia, nikamuuliza mbona yeye hakunisalimu, hata hivyo kama ni yule mimi nimemzidi umri yeye ndio alitakiwa anisalimie, lakini hili sio tatizo, kumbe huyo bwana kaniona njiani narudi nyumbani usiku wa 3 mimi akili yangu yote ipo nyumbani,

Nikamwambia ukionesha dalili ya kunidharau hata hao watu watatudharau,

Ila kwa ufupi, yule aliyekuwa na nyumba nzuri na garden sasa hivi yupo gerezani, yule mama mmewe wanaonana kwa mwaka wk mmewe kafariki, yule chapombe naye hatunaye, wale genge ni choka mbaya majuzi nilipita huko,

Hizo taarifa kila alipokuwa akinipa nikawa na Namuuliza umejifunza nini hapo kuhusu maisha,
Lakini haelewi kitu,

Maamuzi niliyochukuani kuuza nyumba na kama nilivyowaeleza hapo mwanzo kile kiwanja kilikuwa eneo linalolipa, kwa hiyo sikupata shida kuuza, na kwa kilikuwa kimeendelezwa sana, kuanzia nyumba kubwa iliyoishia lenta, ile nyumba ya nyumba vitatu tuliyokuwa tukiishi, pamoja na Banda kubwa la kuku, na eneo kubwa tu Kinabalu kwa ajili ya garden na parking hata ya gari ndogo 6

Baada ya yeye kukubali lakini kwa mabishanomakali ,

Tulimpata mteja wa 80M lakini kwa malipo ya 40M kila baada ya miezi 2

Hiyo ilikuwa 2016 November, na ilitakiwa baada ya miezi miwili baada ya kukamilisha malipo tuondoke, ambayo ingekuwa ni April 2017

Kwa ufupi mteja alikuwa muungwana sana,
By December malipo ya kwanza yalikamilika (40,000,000) CASH

nini kilitokea, kumbuka nilikuwa na madeni yanayokaribia mil 15M,
Hapo nyumba imeshauzwa na bado installment 1 ambayo by February lazima ilipwe na sisi tuwaachie wenye nyumba yao, maana sisi hatuna chetu tena, nikama tunarudi kwenye kile chumba kimoja,

JE WEWE KAMA BABA UTAANZA KUFANYA NINI?
Kumbuka kuna katabia fulani nilianza kukaona kwa mke wangu, hasa hasa ka kunidharau na kuwa karibu na vijamaa jamaa.

Na hata wakati mwingine kama simpigii simu anaweza kukaa hata siku nne bila kunitafuta

NGOJA NIONDOE MACHUNGU
ENDELEENI KUNIOMBEA
Nimeipenda hii episode
 
Na hiyo ndiyo Raha ya uislamu..

Viongozi wa kikristo wakosee siku Mona waseme mwanaume wa kikristo aoe mke zaidi ya mmoja utaona vurugu lake [emoji23][emoji23]
Mama weweeee....mjini hapatakalikaa utashangaa mke mkubwa analetewa wake wanne na watoto wawili kila mmoja yaani![emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji16][emoji16]!!!Wanaume wa kikristoo wana watoto njee!na wanachepukaa haswaaa na wanaoa siku Hizi wake wawili wawili mpk watatu!hyo sheria wanatamaani iondolewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIO MKE WAKO MKUU

NA NI KWELI KWA HAYA MATUKIO SIJUI HATA NGUVU YA KUMUITA MKE UNAIPATA WAPI!!!??

KUZAA HATA PANYA WANAZAA (MNISAMEHE WANAWAKE WENZANGU)
Mkiw kuna Mali sehemu huwa mnasema sheria ukiishi na MTU miezi 3 mfululizo ni mkeo,huyu kaishi naye yangu yuko 22 hadi sawa yupo 42 ni nani?
 
Ona sasa mmemvuruga mheshimiwa imepelekea mtiririko mbaya mwishoni na story imekatwa dah!!.
 
Achana na huyo mwanamke na elekeza mapenz kwa bi mkubwa ili upate mtu wa kukusitiri uzeeni..

Umri ulio nao sio wa kukimbizana na mapenzi..

Kwa kweli mzee pole sana ila jitaid kurud kwa bi mkubwa muombe msamaha mmalize uzee wenu salama..
 
Hapana ni vizazi tofauti. Lakini pia kumbuka amekaa na huyu mama kwa 20 years hivi. Basi tu ni kuwa jamaa alimpenda mwanamke, ila mwanamke kwakuwa siku zote aliona yeye ni nyumba ndogo na hakuwa na heshima hata ya kutambulishwa kwa bi mkubwa, ameamua kuandaa maisha yake. Uwezekano mkubwa kama alivyosema huyu bwana, mwanamke alifundishwa na wanawake wenzie ajitengezee masiah tofauti na haya ya huyu mzee.
Mwanamke hajitambui hata Kama alikuwa anajiona kuwa yeye Ni nyumba ndogo but the way huyu baba alivyojitoa kwake alipaswa kumshukuru umejengewa nyumba .umepewa mtaji wa biashara Mara kibao .. amemsaidia kunyanyuka hata pale alipokuwa anafeli still alikuwa nae pa1 ... Amemkuta na maisha magumu anaishi ktk Hali ambayo Ni low class kabisa akamuheshimisha ...

The way alivyokuwa amemuweka vizuri ktk position ya kimaisha Huyo mama alikuwa anaishi ktk nafuu kubwa ya maisha kuliko wanawake wengi wa kitanzania Kuna Wanawake wengi wakitanzania wameolewa lakini Wana maisha magumu yaliyokosa sinto fahamu lakini Huyo dada ijapokuwa hakuwa na ndoa but alibahatika kuishi ktik maisha yenye nafuu kubwa..

So alipaswa kushukuru kwa kile Ambacho dunia imemjaalia na kumshukuru baba wa watu kwa kumtoa ktika dhiki na kumpatia dira ya maisha yake' ''' Hiki Ambacho amemlipa huyu Mzee Ni ushetani mkubwa Sana huyu Mzee hakustahiki kulipwa hivi hata kwa bahati mbaya ...... Imagine Mimi tu ikitokea Nika muhonga mwanamke 500k usiku nalala naota mazimwi Yana nikimbiza sembuse Huyo Mzee wa watu ........ Aahhh mamaeee some women are [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Back
Top Bottom