Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Nimesoma karibu visa vyote ulivyoandika na nimeshawishika kuandika hivi vimstari vichache.

Kimoja kati ya haya yafuatayo huenda ikawa sawa

1. Una zile wanaaita laana za ukoo au umechezewa/Umetekwa akili kimazingara ama na huyo unayemuita mke mdogo au mtu mwingine tu (ndugu, jamaa, rafiki au mtu baki tu).
Mwanadamu mwenye ufahamu wa kawaida hawezi fanyiwa hayo uliyoyaandika umefanyiwa au fanya hayo uliyoandika umefanya na akaendelea kuona ni sawa tu.

2. Hiki ni kisa tu umeamua kufanya utunzi kwa nia ya kuelimisha. Kama nimesoma vizuri zile sehemu za mwanzo umeeleza kuwa mke mkubwa hana taarifa kama una mpango wa kando, lakini ukifuatilia mtirirko wa matukio ni kama maisha yako kwa kiasi kikubwa umetumia muda mrefu kuishi nyumba moja na huyo mpango wako wa kando.
Na kuna mahali umeeleza ya kwamba mpango wako wa kando wafahamika kwa nduguzo nawe kwa nduguze, sasa napata wakati mgumu kuelewa iweje taarifa hizi zikose mfikia mkeo wa kwanza.

3. Mkuu kama wewe unaona ni sawa kuwa na mpango wa kando, iweje umzue mpango wako wa kando kuwa na mpango wake wa kando?

4. Mwisho, hizi mambo za mipango ya kando hebu waachie watu wako na discpline ya kudeal na hizi mambo.
Hatujawasiliana toka aondoke kesho anafunga mwezi,
Namshukuru Mungu sasa hivi wala roho yangu haiumii tena, nimeshamwona taka taka, na kusema kweli na mchukia vibaya sana, usiku na mchana naomba asirudi maana sijui ninaweza kumfanya kitu gani



Ameshanitamkia kuwa yupo hapa kwa ajili ya nyumba tu sisi mimi,

Ameshanitamkia mpaka tugawane vyumba,
 
OMBI WAKUU NA USHAURI

hii nyumba niifanye nini, ni nyumba kubwa,
Ipo kwenye kiwanja cha eka moja,

Eneo ni ni zuri sana, sasa hivi nyumba ni nyingi, lakini ya kwangu kila mtu anaitamani,

Ila bado haijaisha,

Madilirisha nilishaweka ya aluminium bado matatu tu ya dining room
UZA NYUMBA,,KAMA MBWAI MBWAI TU,,MAANA ANAKUTISHIA NA MKE WAKO MKUBWA,,JIANDAE ATAKUJA KUWASHA MOTO HUKO NYUMBA KUBWA ILA JIKAZE KIUME UMUELEZE BI MKUBWA KABLA HAJAFIKA YEYE.

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
Nachofahamu mimi ni kuwa wapo watu wamezaliwa kuishi maisha ya 'levels' fulani tu.
Ukilazimisha waishi nje ya hapo utaumia wewe.

Kwanza jaribu kutumia muda wako mwingi na mkeo mkubwa(wa ndoa), maana ulichokifuata huko nyumba ndogo hukipati tena zaidi ya maumivu.
Umekwepa kumzungumzia mkeo wa ndoa kwa sababu aidha ni mwema nafsi inakusuta au anamapungufu yaliyokufanya utoke nje ya ndoa unayaona ambayo huoni kama ni mapungufu tena.
Kwa mujibu wa simulizi yako, njia pekee ya kuponya akili yako ni kupata faraja ya familia yako inayokupenda. Ni rahisi familia yako kukuelewa(hata kama kuna wakati ulikosa kutimiza wajibu wako vizuri kwa kubanwa na nyumba ndogo) maana unaelekea mengi mazuri ulifanya kwa ajili yao.

Nashawishika kusema, hadi sasa kuna mambo hujaweza kuyatolea maamuzi, na bila kufanya kiume hutaweza kwani pamoja na kuwa mke mdogo hayupo lakini unatumia muda mwingi sana kumfikiria yeye, nyumba na vitu ulivyopoteza kwa ajili yake. Na kwa kufikiria sana hayo hutaweza kufanya maamuzi sahihi. Ulimpenda sana lakini sasa hakufai tena, na ukifanya kosa njano itakuwa nyekundu.
Nilitegemea sana wakati unauza nyumba tayari unajambo la kufanya.

POLE SANA, POLE TENA.
 
Mtoe out muulize anataka nini na miaka 42?,akirudi mpokee kwa upole wala usimuulize ulikua wapi.Usiwaze kuhusu mali,msugue vizuri huyu mwanamke atulie kichwani.Kua mbunifu kitandani,najua unampenda huezi muacha.Usipende kushika simu ya mwanamke,broo epuka hilo.Usimchunge sana,mwache awe huru pia,Baba mbemto vizuri atatulia kama moja.
 
Bwana mitala huwa shida tu vile watetea ume grow hyo environment na dini inakuruhusu, wengine tumekuwa haya mapicha nyumba ndugu twasoma huku mitandaoni tuna Bibi na babu, ba mkubwa na uncle's wanazeeka bila mitala na familia imara na wanazeeka Hadi uzeeni. To me multiple partners ni janga linalonyima watu wengi furaha ingawa watajidai mara mila, sijui Imani sijui blah blah, so mtu KWA hyo issue sioni huruma maana yalikuwa maamuzi dont Make people wakuhurumie kwa uamuzi wako wa maisha
Usikariri pia kwa kua mitala haina Amani basi ndo kote ,wapo wenye mitala na wako poa kama hao wenye single wife wanavoishi kwa amani pia.Sio kila mitala ina shida ndani yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe akili zako siyo nzuri,daima nitakwambia ukweli. Either huna malezi mazuri au kaelimu ulichonacho kanakufanya ujione unajua sana
Afadhali umeona mkuu
Huyu mwanamke hana malez mazur kabsaa
Kwa ufupi ni wale wanawake wahuni Sana
 
Jiulize kwann unahela lakini anazingua?unamuanzishia miradi ya hela na bado hatulii?.Jiulize mbona wanawake wengine wanaishi nyumba za nyasi na hawazingui.Hebu angalia idara ya kitandani.Kuna kitu unaficha tu hapa,ila mvute kihisia,usimpige,kaeni mshauriane.Jaribu kumkotroli asiende Morogoro bila we kuwepo.
 
Ndoa hizi[emoji3][emoji3]

Nina aunt yangu mke wa mjomba wangu yule mwanamke ana Moyo Aisee..tena moyo wa kipekee sijapata kuona..yule mumewe anazaa nje na mtoto anapelekewa yeye alee..na si ile bahati mbaya labda mtoto mmoja la hasha..!!..watoto watatu..juzi juzi hapa kataka kuletewa wengine wawili wadogo kaona imetosha kagoma kuwapokea..wanaume Hawa[emoji23][emoji23][emoji23]
Huyo mke mpk ibilisi anamuogopa.Haahahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto niliokuta nitawalea tena kama wangu wa kuzaa; ila watoto wakunikuta silei, na sio kwamba ntawachukia NO! Sioni sababu ya kulea watoto ambao wazazi wao wamewazaa kwa malengo.
Baba yao alijua ana commitment na mama yao alijua pia na bado wakaamua kuzaa kwanini washindwe kulea[emoji849][emoji849]
Mwanamke anaezaa na Mme wa mtu na anajua kama kaoa ni juhaaa...narudia ttena ni mjingaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom