Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Nakubaliana na
2. Anasema mmoja kati ya watoto anasoma huko nyumbani kwawazazi
Bi mkubwa siyo mpumbavu hivyo, huyu jamaa inaonekana alihama kabisa nyumbani. Na chanzo cha yeye mpaka leo kupokea 120,000 tokea kwa watoto walioajiriwa anakielewa!

4. Kweli kabisa mambo haya yana wenyewe wanaoweza kuyamudu, hii michezo haihitaji hasira, akili nyingi nguvu kidogo, na siyo vice versa.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Akili hawana
Mimi siwezi kumuonea huruma mtu mjinga kama huyu...Sina huruma za kijinga namna hiyo...
Eti naye anajidai kichwa Cha moto!
Nashangaa hata wanaompa pole sijui wanampa pole za nini!

Dawa ya hawa Wazee wanaojitoa ufahamu ni kuporwa kila kitu huko nje wanakomangamanga.
Na akirudi nyumbani kwake halali ni kufukuza tu...haiwezekani jitu limezurura huko mwisho mzigo abebe mkewe asiye na hatia.
 
Wakati mwingine vaa viatu vya bi mkubwa.
Ungeweza? Naamini mbunye zote ziko sawa tu, au Kuna kipya ulikikuta kwa bi mdogo ?
 
Nimesoma story yako karibia kila kipengele ila Kuna maelezo sijaelewa vzr
Picha linaanzia Dar means maisha yenu yote ni Dsm!!
Watoto wanakua umri wa kwenda shule unawatafutia shule nje ya dar ambayo nauli inagharimu karibia 200k kwa wote wawili, means muda mwingi hawapo nyumbani siku ile unataka kumpiga mama yao watoto nao wanakushikia mawe wanakuambia uende kwenu let's say walikua likizo
Wasiwasi wangu unaanzia hapa👇👇👇

Graduation; sijui Ni ya kumaliza darasa la 7 au form 4 muda huo huyo mchepuko wako hakuepo nyumbani anakuja dar bila kufika nyumbani kwako mnaenda kwenye graduation unamsalimia anauchuna unataka kuongea nae anagoma muda wa kulishwa keki unataka kulishwa na mwanao unagoma swali je watoto walihamia Dar au shule ilikua nje ya dsm ila graduation ilifanyikia dsm (chai).
Swali lingine penye utata je watoto hawako Tena boarding school make Kuna mmoja Yuko Kwa mama yako anasomea huko japo hapataki

Anyway story yako ni nzuri inafunza lakini maswali ya sintofahamu ni mengi kuliko kawaida natamani niseme Ni chai lakini members wa Jf watanimeza jumlajumla!!!
Pengine hiki Ni kisa kilikutokea lakini Kuna mambo umeongeza mpk umepoteza content nzima.

Jamiiforums; we dare to talk openly.😆😆😆

cc: Mwitore
 
HuYu mzee yuko kwenye dennial stage. Bado hajaweza kumove on. Apelekwe kw wanasaikolojia. Lakini akubali hapakua na mapenZi toka mwanzo.
Nimewaza nafikiri huyu bwana kuna uwezekano mkubwa kuwa alitelekeza familia kubwa labda ndio maana hii ya huyu bi mdogo inamuuma sana haweza move on.
 
Kaonane na msaikolojia haraka iwezekanavyo akusaidie dada
Dah kama kuandika yanayowaumiza na michepuko ni tatizo Basi nyie mnaosoma na kuumia mtafte wataalamu kwanza Wala, Mimi mzima yangu kuandika huo ushauri wa wataalamu fanyeni nyie kwanza. Pole ukweli huuma
 
Pole sana mkuu kaka yaani duu, yaani jamani kaka zetu mngekuwa mnajua kidogo kwa bimkubwa huwa na huruma lakini ndiyo hivyo huwa hamsikii ngoja nikufuatilie japo nimechelewa
 
Kwa inavyoonekana Mali pekee iliyobaki kwa huyo mwanamke ni hiyo nyumba, mimi nashauri uiache nyumba Kama urithi wa watoto wako hao wawili yeye akiwa msimamizi, makubaliano haya inabidi uyafanye kisheria ili huyo mwanamke asiuze hiyo nyumba then watoto wakateseka hapo baadae. Kwa maana hiyo hao watoto utakuwa umemalizana nao kuhusu urithi.

Ili kuzuia migogoro ya baadae itakubidi uandike wosia, ndani ya wosia uelezee namna ulivyomalizana na hao watoto wawili ili wasipate chance ya kudai urithi kwa mke mkubwa. Ili ikitokea umetangulia kuwe na amani pande zote mbili.
 
Unadhani polisi ndiko uliko ulinzi wako?

Ngoja nikuambie baba yangu;
Unapofanya dhambi basi tambua unajitenga mbali na uso wa Mungu.

Salama yako ni kutubu na kuacha ili uso wa Mungu uwe karibu na wewe.

Uso wa bwana haukai na wenye dhambi.

Mithali inasema hivi;
"Mtu aziniye na mwamamke hana akili kabisa,Afanya Jambo litakalomwangamiza nafsi Yake"

Wewe kwa sasa akili hauna.siyo maneno yangu..ni Biblia inasema hivyo(samahani kama nitakuwa nimetumia lugha Kali...ila sina lugha nyingine ya faraja ninayoweza kuiandika zaidi ya hii)
Hivi hata ukijitathmini mwenyewe,unajiona uko sawa kweli??
Chanzo nini?
Chanzo ni dhambi.

Unafanya Jambo litakalokuangamiza nafsi yako.
Huyo mwanamke hujui anakuwazia nini.
Na lazima anakuwazia mabaya..
Wewe unaenda kuangamia kama unavyoona mwenyewe.
Na salama yako haipo polisi..salama yako ipo kwa Yesu.

Usipo kubali kugeuka basi upo njiani kuangamia.

Jumbe zangu nyingi huko juu umeziruka,ila hii usiiruke.
Na ikiwezekana rudi ukazisome japo zinaumiza ila kuna kitu utajifunza.
 
Pole sana mkuu kaka yaani duu, yaani jamani kaka zetu mngekuwa mnajua kidogo kwa bimkubwa huwa na huruma lakini ndiyo hivyo huwa hamsikii ngoja nikufuatilie japo nimechelewa
Nilshangaa kutokukuona mpaka kisa kinaisha my dear
 
Mzee sasa kapata frustration baada ya kumalizwa kiinua mgongo imagine mission za kijeshi alizofanya nje haja save alikuwa anahangaika na mchepuko usiokuwa na akili, ka invest nguvu nyingi biashara zinakufa tu maana huyu mchepuko ka kajifunza cherehani Basi ni standard seven kwa vitu alivofanyiwa Hadi umri huo hajaweza kusimama, ana kichwa kibovu na hafikirii mbele Wala, ni mtu wa kufuja, ingetakiwa asimame na aache kumsumbua huyu, sasa huyu mzee haja enjoy life yake ndoan na duniani maana most of the time ilikuwa migogoro, akashauriwa na mamake kuhusu huyo mchepuko kumbe ndo kaharibu. Maskini nguvu na hela kafulia na side chick wa ndoa ya kimila kaanza kumkimbia, loh inasikitisha ila ndo akome hyo karma, Sasa watoto hawamtaki wa mke mkubwa na mchepuko kamkimbia, wanaume jifunzeni kujihurumia kwanza aisee, Mimi simhurumii akome Tena achanganyikiwe kabisa
 
Ndugu Ahsante sana kwa mawazo na na ushauri,
Kuhusu hapo namba 1
Mama yangu hakunitaka niwe Na mchepuko,
Ila kipindi hicho nilikuwa bado kijana sana na ndio nimepata mtoto wa kwanza,

Alitaka tu kunifunza kama mzazi namna nzuri ya mtoto wa kiume kuishi,
Maana aliona kila nikitoka kazini break ya kwanza ni home
Sasa kwa uzoefu wake wa maisha aliona sio sawa
Ni bora nikitoka kazini niwe kwanza na vijana wenzangu huko kubadilishana mawazo

Kama umegundua hii tabia yangu moja kwa moja nyumbani labda Ndio imenifikisha hapa kutawaliwa na mke, maana mawazo mengi ya kihuni au namna ya kumnyanyasa mwanamke nilikuwa sina ( yaani ile roho mbaya ya kiume)

Namba mbili 2 hapo,
Mimi ni mpiganaji wa kutaka kumiliki mali
Ndio maana Alhamdulilah maisha yangu na uwekezajinimejitosheleza hilo sina wasiwasi nalo

Nikisema leo hapa Dar niuze Mali zangu zote leo nirudi kijijini, uhakika wa 700 m upo, na malipo

Nikiendeleza maaneo yangu angalau niongeze kama vyumba 30 vya wapangaji
Naiona 1 B, inaninyemelea,
Kwa hiyo uwezo wa kuachia mali yangu kumpa mtu ambaye kaniumiza NO tena nasema kwa sauti NO, nitaenda mpaka kushtakia kwa Mungu,
Maana mali yangu ninauhakika sijamdhulumu mtu yeyote,
Ni damu na nguvu yangu.
Hapo mwanzo nilisema kama huyu mtu asingeonyesha namna yoyote ya kutaka kuizungumzia nyumba hasa hasa wakati wa ugonvi,
Na kukawa na mwelekeo wa kuachana kwa roho yangu ilivyo ningemuachia nyumba,
Ila mpaka nimegundua ana mwanaume bado kweli nimwachie nyumba au tugawane nusu kwa nusu Hapana, big Hapana

Mwaka 2018, yalipozidi kuwa magumu na kunilaza polisi, kesho yake alikuwa kunitoa yeye na ndugu zake 3 dada zake wawili na Baba yake wa hiari wahapa Dar, ambaye kusema kwa kw a miaka yote niliyoishi na huyu mwanamke sijawahi hata kusikia akimzungumzia

Baada ya kinitoa, alishauliwa asilale nyumbani kwangu mpaka nitulie maana ninaweza kumfanyia kitu mbaya,
Sasa wakati tunaagana yule baba akashauri tufanye kitu kama kikao nyumbani kwangu kesho yake,

Tukaagana na mimi nikaridhia nikaona sasa ni muda mzuri wa kutoa yamoyoni yote mbele ya ndugu zake na huyo baba

Wakati mimi nimefika nyumbani, nikampigia yule mdogo wake kwa ajili ya matayalisho ya chakula kwa wageni kesho,

Sasa ile anapokea simu, nilitumia namba yasimu nyingine ambayo hakuwa nayo, ile ya kwanza ilivunjika kioo pale Polisi na ni Iphone na ya kazini kwangu!
Kusema kweli nilipishwa hiyo sh 700000

Ok sasa wakati anapokea ile simu kumbe kulikuwa na mjadara unaendelea pale yeye na mke wangu,

Nilimsikia mke wangu kwa sauti kubwa ile ya kupandisha hasa, akisema

MIMI NIMESHASEMA ILE NYUMBA NI YA KWANGU, YEYE AENDE ZAKE HUKO,.

Baadaye akanyamaza nadhani mdogo wake alimwambia ni mimi nipo kwenye simu,

Nikamuuliza mpaka namsikia huyo mtu anaropoka hivyo.
Yule dada akanyamaza, na mimi si kuendelea kumuuliza, nikampa maagizo ya kesho tu

Sasa ona kweli huyo mtu ni wa kumpa senti tano yangu.?
Kesho yake kwenye kikao yule mzee na wadogo zangu watatu wa kiume na dada zake 2 na majirani 5 na mjumbe, baada ya maelezo yangu marefu kusema kweli kila mtu alishika mdomo,

Lakini wale wadogo zangu watatu hawakuvumilia, walinyanyuka kwa hasira na kumkimbilia yule mwanamke na kutaka kumpiga watu wakaingilia pale na mimi kwa hasira niwaambia waache yule ni mke wangu,

Wakanielewa wakaacha lakini walilia sana,
Wakatoka nje huku wanalia na kusema, hatukujua kama kaka yetu unasumbuka hivi na huyu mwanamke,
Kaka ambaye umetusomesha umetutunza wote

Mbona mama...... ( bi mkubwa) hakuwa hivi, I I ingekuwa ni huyu kweli sisi tungefika hapa?

Mmoja tena akakurupuka kwenda kutaka kumpiga nikamkatalia, ni kikao kikaishia hapo,

Wakati namsindikiza yule baba aliniambia neno moja tu, KUWA MWANAUME!!!
 
Aahahahahaha haki nimecheka; nakutoa mawaidha kukaisha eeh. Na wakati mwingine unakuta mke mkubwa anaridhia kweli aletewe mwenzie; shida huyo mke wa pili anapokuja na hekaheka zake, mke mkubwa anaisoma namba.
 
Anavuna alichopanda.
Alilima mahindi,anavuna mahindi.
Huwezi kulima karanga halafu utegemee kuvuna mpunga.
 
Utaenda kushtakia kwa Mungu yupi?
Huyuhuyu Mungu aliyesema Usizini!?!

Mungu siyo wa mchezo namna hiyo aisee.
Huo ni mshahara wa dhambi...lazima uwe liable kubeba.
 
Bila Shaka huyu 'Mke mdogo' ni wa kutoka Morogoro (lakini sio Mlugulu au Mkutu) au Kanda ya ziwa - Mara
 

Hebu mkuu tuambie wewe umeamua nini sasa?
 
Maneno mengi umetunga, kama kufulia basi ni kumuacha huyo mwanamke labda ndio kufulia kwenyewe, lakini nipo njema, kazi ninayo,
Wala Watoto hawajanikimbia, wala wakubwa wananipenda kinoma,

Ila wakati mwengine kuwa Positive tu
Harafu uwe unatafakari ni nini binadamu wengine wanakuambia, huwezi kujua kila kitu hapa duniani, uwe unachukua na ya watu wengine,
Hasa hasa ukiona wamekuzidi umri,
Huwa wana jambo zuri moja hata kama yale 19 ni ya ovyo kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…