Unasema, akirudi nimpokee tena? Big hapana.
Naomba nisaidie kumwomba Mungu asirudi.
Kumuuliza ulikuwa wapi nilichokaga, ameshaondokaga mala nyingi tu,
Na kurudi mpaka nikaanza kumwangalia tu,
Nilishaanza kuhisi huyu ana matatizo ya akili, sio mzima huyu
Siku moja mwezi wa nne mwaka jana,
Nikikuta msg ya mwanaume, aakakana kumfahamu, nikamwambia kesho nakuja uniambie vizuri,
Nilivyoenda kesho nikakuta kachukua baadhi ya nguo zake kaondoka
Ilikuwa kipindi kile shule zimefungwa sababu ya corona, nikwaambia watoto nikijua shule zinafunguliwa lini, mmojawapo kabla hajarudi shule, amalizie hii mizigo kumpelekea huko kwao
Nadhani watoto walimwambia kuwa baba kasema tukuletee mizigo yako kabla ya kurudi shule,
Mala tangazo la kufunguliwa shule likatoka,
Akarudi haraka sana, nilipoenda nikamkuta,
Nikashinda hapo mpaka jioni bila kumuuliza kitu,
Wakati naondoka, nilimwambia nina mazungumzo na wewe, sio vizuri niondoke bila kujua ulikuwa wapi, na Ume rudi bila kujibu lile swali langu,
Akanijibu kwa mkato tu, kuwa nilikuwa kwa Baba mdogo , moro.
Sikutaka hata kuendelea kumuuliza tena,
Nikageuka nikaanza kuondoka,
Wakati naondoka akaniambia TENA ILE HATI IRUDISHE HAPA,
Niligeuka na kumwangalia na kutikisa kichwa na kuondoka bila kumjibu kitu,
Nilipata mawazo kuwa huwa sasa hivi si mtu,
Ni kichaa tayari hana akili za kibinadamu tena,
Hata mtoto mdogo akikosea hawezi kukufanyiatena kosa muda huo huo,
Kuhusu kuangalia simu yake, ni baada ya kuona mwenendo usio wa kawaida, Ndio nikaanza kufanya uchunguzi,
Mbona bi mkubwa siangalii simu yake, unataka kuniambia yeye yupo perfect sana, kwamba hana makando kando yanaendelea huko, hapana naye ni binadamu, lakini hakuna alichowahi kunitendea kila cha kunifanya nintilie shaka