Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Hivi huyu shetani tumemkosea nini sie wanadamu?! Huyu bwana bifu lake si na Mungu?! Sasa kisa cha kutuandama wanadamu ni nini wakati yeye bifu lake ni na Mungu Baba?! Hebu angalieni. Kutokana na stori kuwa lirefu sana ikafika wakati nikaamua nisome kwa haraka haraka (kuperuzi) na kwahiyo baadhi ya mistari nikawa nairuka. Sasa shetani alivyo mwanaharamu, nilipofika kwenye quote hiyo hapo, paragraph ya kwanza sikuiona na badala yake macho yakaenda kutua palipoandikwa " Wakati watu wengine wamelala, mimi nikapata viwili." Eti shetani akaniaminisha "ukapata bao mbili za chapchap huku raia wakiwa wamepiga mbonji! NIkajua ni bao zetu zile kupitia ulaji tunda kimasihara! Swali lililopita kichwani fasta fasta ulikula tunda kimasihara na kupata 2 chap chap kwa mazingira gani! Ehee! Naanza kusoma tena kumbe ulipata viwanja viwili!!

Nahama kanisa, nahitaji upako kwa kweli!!
Khhaaa! Ndicho ulichoambua[emoji15][emoji15]! Shetani shindwa, ashindwe na alegee [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hii shida yote ni katika kuficha dhambi ya mchepuko imekufikisha hapa.
Ukweli humuweka mtu huru ongea na mkeo wa ndoa juu ya hii shida labda mcheps anapata nguvu ya kufanya hivi akijua ana karata moja nzuri ya mkeo.
Nina swali binafsi ikiwa siku za mbeleni ukaja kusikia mkeo wa ndoa moja au wawili ya watoto unao dhani ni wako sio damu yako utafanyaje?? nasubiri majibu
Mm sina jibu, naomba tu nisifahamu
 
Huyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,

Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
Pole mkuu ushauri ni kwamba soma majibu na maandiko ya humu halafu chagua yanayokufaa
 
Hahaaa...dah!!umeona eeeh!!yaani Mimi untambulishe mtoto msibani.Wallahi namkataa na live!
Ndugu wa mume acheni roho mbaya na nyinyi ni wake pia na km wanaume mtazaa wa kikke watafanyiwa hila hizi hizi!!!

Kuna vitu huyu baba amefunika live kaficha haiwezekani kirahisi hivi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi hata angenitambulishia wapi !.
Simjui kabisa..na mtu asije fanya ujinga wake huko akitegemea ataleta mtu kwangu eti anitambulishe..atasimulia kitakachompata.

Hii ni kwa wote,mume wangu na baba yangu.
 
Mzee wangu ashakum si matusi, naomba niseme tuu mwenye kichaa ni wewe sio huyo mchepuko.

Sababu ziko wazi kabisa. Hebu kaa chini tafakari kwa kina na utajua mwenye shida huko upstairs ni wewe na si huyo mchepuko wako.

Mzee wangu wewe ni mwanaume, hebu fanya maamuzi ya kiume.
Unforgetable
Hajielewi, ndiyo maana hata wazazi wa bi mdogo wamemuona hivyo, hawahangaiki naye, wamemkalia kimya, hata huko mahakamani, polisi, majirani wote naamini wanamshangaa.
Na uhakika ushauri alishaupata huko kwenye vikao vyote ila hajaupokea!
Anataka kusikia bi mdogo akimwambia anampenda, anamtaka, anamhitaji!

Wanaume Mungu sometimes atutetee, baada ya shetani kutudhalilisha! Mzee anahitaji divine intervention, na psychological help kubwa SANA.

Kazama kwenye matope mazito, sijui quick sand!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hahaha mdogo wangu I can't you[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Basi Mimi nimeyafurahia kweli yaani
Na natamani wamvuruge hadi wamtapeli kila kitu .
Nasubiri waje hao wa kupiga ramli kwamba nina stress tujadili nao kinagaubaga.

Hii hata ingemkuta baba yangu mzazi Basi wavuruge haswaa hadi wamtapeli kila kitu...na hao watoto wanaoitwa wa nje sisi hatuwajui..hasa Mimi!naowajua ni ndugu zangu tu wa tumbo Moja..na asije akajichanganya akaleta huo ujinga..atasimulia.
Sisi huwa hatumfichi mtu mbona.

Nasema hivi wanaume wahuni na wanaojidai miili yao inawaka sana Moto wapelekwe Moto hivyohivyo ,
Kama yameamua kuwa mazezeta sisi tufanyaje???
Mimi sijawahi kuwa na huruma na mtu kwa mambo ya kipumbavu Kama haya.

Zaidi sana nampa pole na kumuonea huruma huyo mama mke wa ndoa kwa furushi Hilo la mzigo alilolipata..Mungu wa Mbinguni amtie nguvu.
 
Ahsante sana, Mwenyezi Mungu akubariki sana, ni ushauri mzuri, kwanza niliogopa sana, kumfukuza nikijua kuwa, atasema labda nimemtumia vya kutosha sasa nimemchoka narudi kwa mke,
Lakini baada ya kugundua anaendelea na mwanaume ambaye, nilishamtuhumu miaka 10 iliyopita pamoja na visa vyote hivi na kiburi, kumbe naye ana bwana yake pembeni, hapana uzalendo umenishinda, potelea mbali , kama ataniraumu basi ni mwendelezo wa akili zake ndogo kutokujua makosa, kwa kipindi chote hicho,

Lingine nililogundua kumbe hata hizo biashara ya mchele huko Morogoro walikuwa wapo pamoja,

Ila mbaya zaidi pamoja na malalamiko yangu kwa wazazi wake, lakini hawaonyeshi hata kushtuka,

Mfano halisi ni sasa hivi, mtoto wao yupo kwao lakini hata kunipigia simu, kuniulizia kulikoni hakuna! Mpaka bajiuliza hii ni familia ya aina gani,

Mpaka nawaeleza waziwazi kabisa mbona mtoto wenu anatembea na aliyewahi kuwa mkwenu ( huyo bwana alishawahi kuoa binamu ya mke mdogo) wakagombana baada ya kufumaniana,

Na jamaa akataka kumuua mgoni wake kisu,
Akatoroka kijiji kwa muda fulani.
Lakini mpaka nafikia hatua ya kuwaambia wazi wazi, kuwa mlikuwa mnanidanganya kumbe mnajua mtoto wenu ana wanaume wawili halafu mkiendelea kuniomba vimisaada, na kuwakatia simu ambapo leo ni wiki ya tatu hawanipigia tena!
Sasa wazazi unataka wajishughulishe na wewe na akati sio mume halali? Wenyewe wanatakiwa kuangalia mechi inavoenda mwenye kisu kikali ndo mla nyama, mwanamke mwenye wanaume wengi huyo ni kahaba sio mke wa mtu unataka wasluhishe kwako na kwa wenzio pia?
 
Mkuu uza nyumba endelea na mishe zako
watoto wa kike hao wameshapandikizwa sumu na mama yao.
Muhimu wanafahamu mambo mengi kuhusu ugomvi wako na mama yao itoshe tu kuwatambulisha hao wanao kwa ndugu zako watakutafuta wakikuhitaji kwa mambo yakifamilia.
Asiwatambulishe kwa sasa angojee hadi wajitambue maana Kwa sasa hawana msimamo, hawatakuwa na adabu kwa wakubwa zao maana Wana kiburi cha mama yao
 
Unasema, akirudi nimpokee tena? Big hapana.
Naomba nisaidie kumwomba Mungu asirudi.

Kumuuliza ulikuwa wapi nilichokaga, ameshaondokaga mala nyingi tu,
Na kurudi mpaka nikaanza kumwangalia tu,

Nilishaanza kuhisi huyu ana matatizo ya akili, sio mzima huyu

Siku moja mwezi wa nne mwaka jana,
Nikikuta msg ya mwanaume, aakakana kumfahamu, nikamwambia kesho nakuja uniambie vizuri,
Nilivyoenda kesho nikakuta kachukua baadhi ya nguo zake kaondoka

Ilikuwa kipindi kile shule zimefungwa sababu ya corona, nikwaambia watoto nikijua shule zinafunguliwa lini, mmojawapo kabla hajarudi shule, amalizie hii mizigo kumpelekea huko kwao

Nadhani watoto walimwambia kuwa baba kasema tukuletee mizigo yako kabla ya kurudi shule,

Mala tangazo la kufunguliwa shule likatoka,
Akarudi haraka sana, nilipoenda nikamkuta,

Nikashinda hapo mpaka jioni bila kumuuliza kitu,
Wakati naondoka, nilimwambia nina mazungumzo na wewe, sio vizuri niondoke bila kujua ulikuwa wapi, na Ume rudi bila kujibu lile swali langu,

Akanijibu kwa mkato tu, kuwa nilikuwa kwa Baba mdogo , moro.

Sikutaka hata kuendelea kumuuliza tena,
Nikageuka nikaanza kuondoka,
Wakati naondoka akaniambia TENA ILE HATI IRUDISHE HAPA,

Niligeuka na kumwangalia na kutikisa kichwa na kuondoka bila kumjibu kitu,

Nilipata mawazo kuwa huwa sasa hivi si mtu,
Ni kichaa tayari hana akili za kibinadamu tena,

Hata mtoto mdogo akikosea hawezi kukufanyiatena kosa muda huo huo,

Kuhusu kuangalia simu yake, ni baada ya kuona mwenendo usio wa kawaida, Ndio nikaanza kufanya uchunguzi,

Mbona bi mkubwa siangalii simu yake, unataka kuniambia yeye yupo perfect sana, kwamba hana makando kando yanaendelea huko, hapana naye ni binadamu, lakini hakuna alichowahi kunitendea kila cha kunifanya nintilie shaka
Kaka ingawa na siye yametukuta... Lakini ushauri wangu kwako Ni mgumu Lakini wenye manufaa.. Mali Ni kitu Cha kupatikanika... Hapo hakuna suluhisho rahisi Tena Mwanamke akiamua ameamua Inabidi wanaume tukubali Hilo bila ya kuangalia kosa liko kwa Nani. Unachoweza Kufanya Sasa Ni kukubaliana ukweli mchungu. Kubali uuze hiyo Nyumba ambayo umesema huwezi kuvumilia kuona mwanaume mwingine anaofaidi. Uza gawa Mara nne sehemu yako yake na watoto hao wawili.. Kisha Rudi kwa unyenyekevu kwa Mkeo Mungu aliyokupa. Ulikosea Sana Kumwacha na kujiongezea huyo Bi Mdogo. Umesema utapa Pension ya kutosha. Usihangaike na huyo Mwanamke Tena . Naona wazi roho ya mauti inakunyemelea kwa ukaribu. Kama Siyo kifo Basi stroke ipo njiani. Kubali ulikosea na utulizane. Tena hapo kataka mwenyewe kukuacha imekurahisishia Sana. Atakuua huyo kumbuka anaishi na Muhuni anayeweza kuchoma watu visu.. Unajuaje kuwa wanapanga njama za kukumaliza ili warithi Hiyo Nyumba?? Bro Jiongeze hata hivyo inaonekana Mungu anakupenda Sana misukosuko yote Hi Bado unadunda.. Na Hela unapata. Tulia na Mkeo Mungu aliyokupa. Huko mbeleni Ni Kilio na kusaga Meno. Unaweza kuja kujikuta Bi Mkubwa naye akakuchoka kwa Sababu ya Hili akakuacha maana naona na Yeye Ni mvumilivu Sana. Achana na huyo Kahaba(Pole kwa Kumwita hivyo Lakini ndo ukweli) Be Blessed
 
Nimesoma mwanzo mpaka mwisho.
Katika maisha kila mwanadamu ana mapungufu yake, japo Kuna waokudhihaki lakini amini Kuna mahali waliterereka kwa Mara moja au zaidi ya Mara moja.

Kikubwa elewa huyo ni mchepuko kwahyo hataka Kama umekaa naye zaidi ya miaka kadhaa bado hajawa na uhalali wa kuwa mke. Japo wewe ni upande wa pili hata dini Uislamu umeruhusu zaidi ya mke mmoja ila wanawake wote uliokuwa nao Wajue kwamba hawako peke yao. Kwa hapa ulifanya kosa la ufundi mchepuko kuupa hadhi ya mke.

Ila Unapokosea na ukijua kosa lako jua ndio mwanzo wa Tiba ya ugonjwa wako.

Nachokushauri usiuze nyumba, nyumba waachie watoto ndio urithi wao. Wewe toka hapo ikibidi pangisha. Usipomuachia hiyo nyumba atakusumbua mpaka ahakikishe umebaki maiti.

Pili mwambie mkeo ukweli una watoto wakubwa .pengine anafahamu kila kitu na kwakuwa hujamuonyesha kumdharau kwa namna yoyote na unayatambua majukumu yako. Ila kakupa mtego, anasubiri siku na saa ya mtego kuteguka, kwahiyo usisubiri mtego uteguke wenyewe, tegua sintofahamu hiyo wewe mwenyewe muombe msamaha mkeo.

La mwisho mandhari watoto ni wakubwa tafuta namna ya kuwasiliana na watoto wako Kama ni mahitaji muhimu watumie wao moja kwa moja siku hizi Kuna maendeleo hasa kwenye huduma za kifedha tafuta njia Bora ya kuwahudumia watoto wako. Huyo mama piga block kote wewe bakisha uhusiano na damu yako tu.

Mwisho huyo mwanamke usijaribu kumrudisha Tena kwenye maisha yako akirudi atakuvuruga kuliko Mara ya kwanza. Kwa Sasa anajua unakaribia kustaff tegemea ujio wake muda wowote.

Nakutakia kila lakheri kwenye kufanya maamuzi yako.
Bi mkubwa alishajua, unajua jitihada za michepuko kujitambulisha wenyewe kwa kina mama mjengo eti alimuwekea chupi ya mtoto kwene bag🤣🤣🤣🤣🤣 ishu ya kupewa 120000 na watoto ilianzia apo
 
Nimesoma karibu visa vyote ulivyoandika na nimeshawishika kuandika hivi vimstari vichache.

Kimoja kati ya haya yafuatayo huenda ikawa sawa

1. Una zile wanaaita laana za ukoo au umechezewa/Umetekwa akili kimazingara ama na huyo unayemuita mke mdogo au mtu mwingine tu (ndugu, jamaa, rafiki au mtu baki tu).
Mwanadamu mwenye ufahamu wa kawaida hawezi fanyiwa hayo uliyoyaandika umefanyiwa au fanya hayo uliyoandika umefanya na akaendelea kuona ni sawa tu.

2. Hiki ni kisa tu umeamua kufanya utunzi kwa nia ya kuelimisha. Kama nimesoma vizuri zile sehemu za mwanzo umeeleza kuwa mke mkubwa hana taarifa kama una mpango wa kando, lakini ukifuatilia mtirirko wa matukio ni kama maisha yako kwa kiasi kikubwa umetumia muda mrefu kuishi nyumba moja na huyo mpango wako wa kando.
Na kuna mahali umeeleza ya kwamba mpango wako wa kando wafahamika kwa nduguzo nawe kwa nduguze, sasa napata wakati mgumu kuelewa iweje taarifa hizi zikose mfikia mkeo wa kwanza.

3. Mkuu kama wewe unaona ni sawa kuwa na mpango wa kando, iweje umzue mpango wako wa kando kuwa na mpango wake wa kando?

4. Mwisho, hizi mambo za mipango ya kando hebu waachie watu wako na discpline ya kudeal na hizi mambo.
Uko vizuri mwanangu nakuamiani sana
 
Miranda I, hilo halina shaka, najiamini,
Ndugu yangu nimetumia kila mbinu, asiende huko, ikiwa ni pamoja na kumfukuza ndani mwangu,amewahi kulala nje mala mbili,

Nimeshamwitia mjumbe, mpaka majirani,
Nimeshapiga,
Nimeshatoa taarifa kwa wazazi wake,

Hebu fikiria hili,
Kwa zaidi ya miaka mitano tumekuwa tukipingana kuhusu biashara ya kusafiri
Na akisafiri ndio hivyo anakaa wiki anarudi tnagombana sana,

Lakini leo unathubutu kwenda kukodi shamba ulime, na ni hukohuko Moro ambako sitaki uende?
Unafikiri hii ni akili kweli ya binadamu
Hapana huyu ni kichaa tayali
Wewe ndo una kichaa kung'ang'ania mtu ambaye tayari ashakuonesha kila aina ya tendo kuwa hakuitaji
 
Hahaha mdogo wangu I can't you[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Mimi nilishamwambia mama ishu kama hizo zisikusumbue kichwa kabisa..
Zikikupata wewe niletee halafu kaa pembeni.

Mamndenyi Kuna scenario ulielezea kwenye uzi fulani ,niliumia sana mama yangu.
Nilitamani ningekuwa mtoto wako japo kwa muda mchache tu!niwanyooshe wale wajinga.
 
Naomba nitag kwenye hiyo scenario ya aunt yangu
Mimi nilishamwambia mama ishu kama hizo zisikusumbue kichwa kabisa.
Zikikupata wewe niletee halafu kaa pembeni.

Mamndenyi Kuna scenario ulielezea kwenye uzi fulani ,niliumia sana mama yangu.
Nilitamani ningekuwa mtoto wako japo kwa muda mchache tu!niwanyooshe wale wajinga.
 
Basi Mimi nimeyafurahia kweli yaani
Na natamani wamvuruge hadi wamtapeli kila kitu .
Nasubiri waje hao wa kupiga ramli kwamba nina stress nijadili nao kinagaubaga.

Hii hata ingemkuta baba yangu mzazi Basi wavuruge haswaa hadi wamtapeli kila kitu...na hao watoto wanaoitwa wa nje sisi hatuwajui..hasa Mimi!naowajua ni ndugu zangu tu wa tumbo Moja..na asije akajichanganya akaleta huo ujinga..aisee atasimulia.
Sisi huwa hatumfichi mtu mbona.

Nasema hivi wanaume wahuni na wanaojidai miili yao inawaka sana Moto wapelekwe Moto hivyohivyo ,
Kama yameamua kuwa mazezeta sisi tufanyaje???
Mimi sijawahi kuwa na huruma na mtu kwa mambo ya kipumbavu Kama haya.

Zaidi sana nampa pole na kumuonea huruma huyo mama mke wa ndoa kwa furushi Hilo la mzigo alilolipata..Mungu wa Mbinguni amtie nguvu.
Mimi huyu sijamuonea huruma ni ujinga wake wanaume huwa Wana roho nyepesi ila hawakomi kuhangaika na ningekuwa mke wa ndoa namtenga na watoto afie mwenyewe huko. Huyu mzee kastaafu kiinua mgongo kimeisha na mchepuko umemkimbia ndio anashtuka na mbaya zaidi Hana mahusiano na mkewe mkubwa kwanini ahurumiwe kwa ushenzi wa kudhulumu familia Halali, Mimi namjua mstaafu mmoja wa ofisi ya Raisi mchepuko michafu imemufilisi Hana hata kumi na mke wa ndoa kamwacha hana hata ya kula. Mwanaume muendekeza michepuko ni laana na uzeeni huishia pabaya Bora hata mwanaume mnunua michepuko, sijui Wana akili gani loh
 
Hii story imenisikitisha sana.

Yaani mwanamkee umlee, umlishe ,umtunze halafu akuendeshe kama gari moshi.
Hivi mkuu wewe ni kabila gani mbona huu mlenda mlenda sana????

Yaani kwa maneno yako ulikuwa vizuri kifedha amekuendesha kama gari moshi jee ukistaafu? Sii atakuingiza kidole hadi matakoni.

Mtu anakutusi, dharau hadi kakupeleka kituoni wewe bado tu umekomaa nae au ni nguvu ya K ilikuwa inatumika .

Tatizo wewe ndio ulilitengeneza, ulikuwa unamjaza pesa sana. Ulikuwa unanunua penzi kutoka Kwake japo umeficha ,basi bora hata angekuwa mkee halali wa ndoa yaani mchepukoo ni wakuuza nyumba unamuingizia mamilioni kwenye account??
 
Back
Top Bottom