Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Jamaa anakuambia akiuza assets zake una uhakika wa 700M - 1B[emoji38]

Halafu eti anang'ang'ania kieneo cha 50M
 

Mkuu una familia nzuri sana zaidi ya watu wanavyofikiri. Uzuri umejitoa sana kwao,Mungu akusaidie umalizana na huyo Bi mdogo salama,kitu ambacho kiko wazi utashinda hiyo vita kwani umeshikilia mpini
 
Mkuu kwa nini unajiumiza sana,hati ina majina yako,bi mdogo siyo mke halali,yaani kwa nini ujiuzie? Tafuta mteja kabisa akupe hela nzuri kama utahamua kumpa robo ya pesa its okay akafie mbele huko,si ameamua kuishi kama shetani

Mwitoro atakua na moyo sawa na mfalme Daudi
Mfalme Daudi @Mwitoro
 
Siku ambayo hao watoto wangenitamkia hivyo mimi haijalishi ni wangu au sio wangu wangepata adhabu inayokwenda sambamba na mama yao na kutokea hapo ningewatuma wakatafute baba yao
Hata ningefanya hivyo
 
Reactions: T11
Upo sahihi kabisa mkuu.

Lakini vipi kuhusu watoto wawili waliopatikana hapo. Nadhani ni busara ingetumika kuwawaza pia, tusiangalie tu matendo na hitimisho la hayo mapenzi ya baba na Mama yaliyopelekea kupatikana hao watoto.
Unajua Luv iko hivi,

Tayari mahusiano hayo ya wawili yameshakuwa shubiri. Kisheria hiyo mali ni yao hao wawili ambao wamekuwa wote katika mahusiano yasiyokuwa rasmi lakini kisheria yapo rasmi.

Na ndio maana nimeshauri kuwa ni bora akamalizane na mke wake halali na kumweleza kila kitu juu ya hilo. Natumaini atamwelewa vizuri na watoto pia awasogeze karibu na wenzie ili waweze kuwa pamoja kama familia, vinginevyo atapata shida sana.

Nyumba wauze, wagawane nuvu aelekeze kwa mkewe halali
 
Reactions: Luv
Jamaa anakuambia akiuza assets zake una uhakika wa 700M - 1B[emoji38]

Halafu eti anang'ang'ania kieneo cha 50M

Nakumbka alisema viwanja sita hapo alinnua kimoja ndio akajenga hiyo nyumba hivo nyumba na eneo nafkir zinapita jamani khaaa 50M eneo lote hilo[emoji16]
 
Kuchambwa lazima. Muhimu mnooo... maana unafanywa zoba.

Naomba nikuambie... acha kbs kujisemea eti una hela nyingi... hakuna kitu kitamu kama cha kupewa mzee wangu. Baba yangu ana jimudu vyema. Lakini vile vidogo nampatiaaa.... heheheeee yaanii anaona rahaaa. Usituongopee hapa. Yaan hakuna kitu raha kama kutunzwa. Yaan mashati alonunua babangu ameyatelekeza anavaa yangu. Na anasema malaika wangu ameninunulia haya ili nivae. Na yamepauka anayapenda balaa. Wewe hutaki hizo raha? Hakuna kitu kibaya kama kutengwa na familia. We rudi tu kwa mkeo ndo la msingi. Yaan rudi. Mwanao hata akakupa elf 10 ni tamu sana. Hela yako mwenyewe haina mzuka kama ya wale ambao wanakijali wewe na unawajali... rudi kundini.
 
Kufikia hapa mzee wangu nikupe tu moyo kuwa, umefanya maamuzi sahihi kuja kuomba ushauri hapa kabla hujachelewa ukapoteza kila kitu.

Wasamehe walio toa lugha chafu kukutukana ama kukufedhehesha, hawajui kesho yao,

Chukua ushauri unaoona unakufaa anza kuufanyia kazi tangu sasa, pesa juhudi ulizo poteza kwa huyo mwanamama chukulia tu ni kama ulikuwa unamsaidia mtu mwenye shida au mtoto yatima, hivyo Mungu atakukumbuka kwenye ufalme wake, amka asubuhi moja iliyo njema, Anza maisha mapya ukaipate jioni njema ya maisha yako.
 
Huyu mzee kuna vitu vingi sana katuficha na atapata ushauri ambao hautamsaidia sababu anafichaficha mambo.
King,
Nimeshazungumza kuhusu bi mkubwa, ni kweli baadaye sana alifahamu,
Tokea mwanzo nilisema huu uzi sitaki sana kumzungumzia,
Shabaha ya uzi ni bi mdogo, sasa nimejikuta nalazimishwa mpaka kufahamu mambo ya bi mkubwa,

Kiufupi hana tatizo na mimi, sasa kama ananichekea mdomoni tu mimi sijui
Kama ananitegea kunifanyia kitu mbaya, vile vile sijui, siwezi kuingia kwenye moyo wake

Nachoona tupo happy tu
Ameshakubali hali halisi tunaishi,
Hakuna anachokosa yetu uzima I mwake

Kama mnataka nifunguke zaidi kuhusu bi mdogo nitaendelea kadri nitakapokuwa nakumbuka mambo ya ovyozaidi

Kwa taarifa bado sijafunguka kuhusu vikao zaidi ya 8 tulivyokuwa tunaitisha, alikuwa anazungumza nini

Kwa nini alianza kuniita huyu hataki wageni

Majirani na marafiki zake walikuwa na tabia gani, na nini kiliwapa

Polisi.ustawi wa jamii, mahakama, ofisi za kata

Pote huko walikuwa Na mchango gani kuokoa huu uhusiano Na nini udhaifu mkubwa kabisa upo huko hapana nikashangaa hivi kweli wapo serious kabisa na matatizo ya watu au wapo kwa ajili ya kupiga soga tu, na kutaka kujua matatizo ya watu kiumbea

Mama ni mengi,
Na mwisho kwa ajili ya kumbukumbu zangu za baadaye, haya ni maandishi ambayo itabidi niyahifadhi kitaalaam ili niweze kutumia baadaye

Hasa tukifikia kipindi cha kupelekana mbele zaidi,

Ninachoshukuru kila tunapoendelea na michango na maswali, nashangaa nakumbuka mambo ambayo nilishayapotezea, Ahsante sana

Ila kumbukeni tu,

HII NI TRUE STORY
SIO TAMTHILIA

hata mimi kuna kipindi ninapokuwa mwenyewe nikifikiria haya matukio, iwe kwenye usafiri, ofisini, chooni, naoga, huwa nacheka sana,

Maana huo siamini kama haya mambo yanaweza kunitokea mimi na nikaendelea kuishi

Watu wengi sana wameshajiua kwa maana kama kama haya
 
Jamaa anakuambia akiuza assets zake una uhakika wa 700M - 1B[emoji38]

Halafu eti anang'ang'ania kieneo cha 50M
JF kisima cha burudani nimeamini😂😀

Wenye busara zao kimya kimya wasingetumia hilo eneo kama silaha dhidi ya huyo mchepuko.
Wangemuachia wakajitunzia heshima zao.
Jamaa kajivunjia heshima sana, hao watoto wa bi mdogo kwa wanayoyashuhudia, asijidanganye, eti kuna BOND, wanayashuhudia na mama yao anawaambia yote, baba yao anawafukuza anawadhulumu!

Miaka 100, hawezi kuwa na amani! Sababu kubwa haamini hapendwi na yule aliyempenda kwa kumhonga kila kitu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mi hapo ndo nabaki na maswali inawezekanaje yani

Mimi mfano ndio bimkubwa bac hata iwe Mwitore ana ratiba za kutoka ucku kwenda kazin mara asafiri haijalishi bac mm kama bimkubwa nagundua ndani ya mwezi mmoja tu kuwa una hali sio ya kawaida Yani hamna mwanamke pia atakaejua una mtoto nje halafu situation ikawa poa hata iwe ni mtakatifu kiac gani wachilia kuzaa nje mko kwenye ndoa iwe ana mtoto tu na akaoa bila kusema ana mtoto bac siri ikitoka bac ugomv unaibuka je azae nje watoto wawil halafu mke aseme tu wajengee tu huko waishi yani wanawake sisi wa karne hii? Ugomv usiibuke? Anyway hatufanani wanawake Labda hawajagombana na bimkubwa Ila kwa ushaur tu bado ana nafac me nawajua watu wametengana kwa miaka zaidi ya 20 na ni wanandoa na wakarudiana na mambo safi tu nayy arekebishe sakata la nyumba then arudi kwa bimkubwa aitwe mchungaji ndoa ibarikiwe upya waanze maisha yao wasubir matunda ya pensheni
 
Halafu anazuga eti hamtaki huku roho inauma
 
Mwanzo nilisema aseme ukweli upande wa bi mkubwa baadae akaja kukiri bi mkubwa alikuja kujua huu mchepuko
Bado kuna kitu hajasema baada ya kujua nini kilifuata, asiseme mambo yaliisha kwa amani
 
Mapenzi upofu
 
Exactly. Kuna heshima ipi na upendo gani mtu kwenda kuvunja agano lake la ndoa na mchepuko? Labda kama kuna definition mpya ya upendo na heshima
Mimi amenishangaza alivyo na ujasiri wa kujivika mizigo, wamejuana kidogo tu kurupu amempangia chumba, mara amemnunulia kiwanja, mara amemuweka miradi eti vya watoto[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]kajitesa sana maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…