Huyu mzee kuna vitu vingi sana katuficha na atapata ushauri ambao hautamsaidia sababu anafichaficha mambo.
King,
Nimeshazungumza kuhusu bi mkubwa, ni kweli baadaye sana alifahamu,
Tokea mwanzo nilisema huu uzi sitaki sana kumzungumzia,
Shabaha ya uzi ni bi mdogo, sasa nimejikuta nalazimishwa mpaka kufahamu mambo ya bi mkubwa,
Kiufupi hana tatizo na mimi, sasa kama ananichekea mdomoni tu mimi sijui
Kama ananitegea kunifanyia kitu mbaya, vile vile sijui, siwezi kuingia kwenye moyo wake
Nachoona tupo happy tu
Ameshakubali hali halisi tunaishi,
Hakuna anachokosa yetu uzima I mwake
Kama mnataka nifunguke zaidi kuhusu bi mdogo nitaendelea kadri nitakapokuwa nakumbuka mambo ya ovyozaidi
Kwa taarifa bado sijafunguka kuhusu vikao zaidi ya 8 tulivyokuwa tunaitisha, alikuwa anazungumza nini
Kwa nini alianza kuniita huyu hataki wageni
Majirani na marafiki zake walikuwa na tabia gani, na nini kiliwapa
Polisi.ustawi wa jamii, mahakama, ofisi za kata
Pote huko walikuwa Na mchango gani kuokoa huu uhusiano Na nini udhaifu mkubwa kabisa upo huko hapana nikashangaa hivi kweli wapo serious kabisa na matatizo ya watu au wapo kwa ajili ya kupiga soga tu, na kutaka kujua matatizo ya watu kiumbea
Mama ni mengi,
Na mwisho kwa ajili ya kumbukumbu zangu za baadaye, haya ni maandishi ambayo itabidi niyahifadhi kitaalaam ili niweze kutumia baadaye
Hasa tukifikia kipindi cha kupelekana mbele zaidi,
Ninachoshukuru kila tunapoendelea na michango na maswali, nashangaa nakumbuka mambo ambayo nilishayapotezea, Ahsante sana
Ila kumbukeni tu,
HII NI TRUE STORY
SIO TAMTHILIA
hata mimi kuna kipindi ninapokuwa mwenyewe nikifikiria haya matukio, iwe kwenye usafiri, ofisini, chooni, naoga, huwa nacheka sana,
Maana huo siamini kama haya mambo yanaweza kunitokea mimi na nikaendelea kuishi
Watu wengi sana wameshajiua kwa maana kama kama haya