Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Itakuwa hv:

Bi mdogo baada ya kuona nyumba imeuzwa na status yake mtaani kwa washirika kuonekana km imeshuka hv, basi atataka kumharibia Mzee Kwa bi mkubwa...
Captrait ,
Nashukuru bado hajafikiria kuniharibia huko ,
2, hilo la Watoto nakuja huko
3Kiuchumi Alhadulilah, pesa ya kula ipo, ipo ndio hivyo uchumi wa Magufuli na Covid 19
4.hilo la bi mkubwa ndio naliogpa sana, lakini bado tutafika huko
5, hasa waliokufa karibu na mimi ni kweli kabisa, pote huko tutafika
6, kama ulivyomnukuu Warren Buffet, ni kweli ndio maana ya kuwa hapa, maana hata mji nataka kuukimbia, hiyo ndio inajengeka kichwani sasa hivi
7. Sawa hayo matatizo ya mwisho, tutaona mwishoni kabisa,
Lakinimpaka hapo ushauri mzuri sana nipenda
 
Ushauri wenu ni muhimu sana.

Umri wangu ni miaka 50, nimeoa mke kanisani huu ni mwaka wa 25 naishi naye na tumejaliwa watoto wanne, wa kwanza na wapili wamemaliza tayari chuo kikuu na wa tatu yupo chuo kikuu mwaka wa pili...
Kumbe bado mdogo muulize Mohamed Said
 
Sawa, hilo lakuunganisha nashindwa nitamwanzaje mke wangu,
Lakini story bado inaendelea
Bado ushauri hapo baadaye utakuwa mzuri zaidi
 
Mzee kamata ulicho nacho usiangaliye nyuma nyumba ndugo adi sasa kuna kizaa
 
Captrait ,
Nashukuru bado hajafikiria kuniharibia huko ,
2, hilo la Watoto nakuja huko.....
Kaka usijali, we maliza kisa tutakushauri vema hutakaa ujutie.

Haya ni maisha ndugu yangu, na kila mmoja ana mapito yake, lait watu wangesimuliana nadhani yako ungeona nafuu mara dufu zaidi. So, relax wala usiogope kabisa chochote.

Ni kweli kwa muda utaumia na kuteseka lkn yatapita kama mengine yapitayo.
 
Nimejifunza na naendelea kujifunza kitu kupitia story yako Mzee wangu...
 
Mkuu, kama haya ni ya kweli basi hiyo nyumba uliuza kwa bei ya hasara sana. 80,000,000 by 2016 ni hela ndogo sana ukilinganisha na jinsi ulivyoielezea hiyo nyumba na hilo eneo.

Nyumba yangu yenye vyumba 4 nimeijenga kwa 60,000,000 lakini wala haipo eneo la kishua wala nini. Ipo huku uswazi kabisa how come wewe nyumba yenye kiwanja kikubwa na mazagazaga yote hayo uiuze kwa 80,000,000?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…