Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 24,893
- 47,768
Kuna sauti ni rahisi sana kuzitambua, hapo privacy itakua wapiJF waweke option ya voice clip
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna sauti ni rahisi sana kuzitambua, hapo privacy itakua wapiJF waweke option ya voice clip
Ahaaaa nacheka kama mazuri ila najiuliza wanawake wengine hii bahati wanayochezea hivi wanaitoaga wapi?.huyu dada kinachofata ni majuto. Ulosema yote yatatokea soonItakuwa hv:
Bi mdogo baada ya kuona nyumba imeuzwa na status yake mtaani kwa washirika kuonekana km imeshuka hv, basi atataka kumharibia Mzee Kwa bi mkubwa.
Pia, watoto wake aliozaa nao watatumika vilivyo na bi mdogo.
Mzee Baba kiuchumi utakuwa umeyumba mno mno na bi mdogo hatakuwa na uvumilivu wowote kwako
Suala likifika kwa bi mkubwa litakuwa suala la Moto sana infact bi mkubwa atakuwa disappointed SANA.
Familia ya bi mkubwa hasa watoto na Jamii nyingine iliyopo kwenye circle yako itakuwa disappointed mno.
Washkaji, ndugu na jamaa wengine watakuelewa tofauti at the end life goes on
Warren Buffet aliwahi kusema "....it takes 20 years to build reputation but it takes one minute to ruin it...."
Kwa minajili ya kujifunza kwa vijana wachanga kimaisha, Je nini kilipaswa kufanyika kabla kisa hakijafika hapa? Tusubiri mwishowe wa kisa, tuone
Ushauri wetu kwako ni upi? Ni hekima na busara kusubiri mwisho wa kisa kizima, lkn haya matatu hayana conditions:
One,
fight for bi mkubwa regardless
Two,
fight for your kids (wote wa bi mdogo na bi mkubwa)
Three,
Achana na bi mdogo akatafute maisha yake mengine, tena asitake mazoea na wewe
Tunaendelea kufuatilia kisa!
NAENDELEA,
Kumbuka hapo tayari tumeshaamia kwenye nyumba yetu (YETU) na baada kama ya miezi sita niliingiza umeme ambao ulinigharimu kama 400000 wakati huo ( nguzo 2)
Unataka kumuongezea preshaYaani wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika, kwanza hapo huenda hata hao watoto wa bi mdogo siyo wake, [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji848] namuwazia tu mwanaume mwenzangu
Pole sana baba. Kwa ufupi wewe na mke mdogo soon mtaachana. Ila kachezea bahati sana atajuta atalia kwa uchungu.Watoto wake sasa ndio wamemaliza la saba, nikawatafutia shule nzuri huko kanda, nauli kwenda tu ukihumuisha vikorokoro vyote tokea hapa mpaka afike shule kwa mmoja sio chini ya 200000, bado ada ambayo kwa mmoja kila baada ya miezi 3 ni sh500000 na mwingine kila baada ya miezi 3 ni 450000, na wakirudi unatuma pesa kama 100000, kwa mmoja...
Umenena Ba mjengo, Michepuko haijawahi kuacha mtu salamaUkweli hakunaga faida kwenye michepuko, nikujiongezea matatizo tu
Unawezaje kufanya mambo makubwa hivyo mke wako mkubwa hajui, ila mkuu ulitolewa ufahamu kabisaKipindi nipo nipo kikazi nje nilikuwa nikimtumia pesa ya matumizi kupitia rafiki yangu wa kazini, ambapo kila baada ya muda alikuwa akienda kuchukua pesa ya matumizi...
Unawezaje kufanya mambo makubwa hivyo mke wako mkubwa hajui, ila mkuu ulitolewa ufahamu kabisaKipindi nipo nipo kikazi nje nilikuwa nikimtumia pesa ya matumizi kupitia rafiki yangu wa kazini, ambapo kila baada ya muda alikuwa akienda kuchukua pesa ya matumizi...
AiseeBaada ya ujenzi kusimama na matumizi kuwa makubwa, nikamgusia bi mdogo kuhusu kupiga bei kila kiwanja cha pili, kusema kweli kile cha pili kilikuwa kinafahamika kwa bi mkubwa, kiujumla kilikuwa cha kwake, lakini kwa sababu naye ujenzi wa nyumba yake ulikuwa umesisimama nilimshawishi mpaka akakubali tukiuze, nikimwambia mikopo kazini imebizidi kimo, kwa hiyo nusu, nimpigie plasta na mambo mengine kama umeme na maji, akakubali
Hata robo bado ndugu yangu wewe unaMkuu story bado inaendelea !?
wewe mawazo yako mtu akiitwa Bi mdogo basi lazima muwe mmepishana 30 au arobaini,Una lako jambo! Huchomoki! Umenasa!
Bi mdogo anasubiria mgao wa kikokotoo.
R.I.P Mengi R.I.P Dr P Ng'wandu.
Hakuna jipya chini ya jua!
Jasiri haachi asili, huna cha kufanya!
Utafanya vile atakavyo bimdogo, COZ unataka kuonyesha uwezo wako kummudu na kummiliki!
Everyday is Saturday............................... 😎
Sawa kabisa, naomba uwaite, na kule yule bwana anaitwa sijui wytson , nimekosea jina ila mkali mkali hivi, avatar yake nadhani ni yule mwenzie Martin Luther King
Pole sana mkuuWatoto wake sasa ndio wamemaliza la saba, nikawatafutia shule nzuri huko kanda...........nauli kwenda tu ukihumuisha vikorokoro vyote tokea hapa mpaka afike shule kwa mmoja sio chini ya 200000, bado ada ambayo kwa mmoja kila baada ya miezi 3 ni sh500000 na mwingine kila baada ya miezi 3 ni 450000, na wakirudi unatuma pesa kama 100000, kwa mmoja
Sio kwamba nina pesa nyingi kiasi hicho lakini waswahili wanasema maji ukishayavulia nguo huna budi kuyaoga,
Sasa umeshawaingiza huko inabidi tu waendelee na mimi meenyewe umri ndio nnasogemea, na kustaafu Ndio huko kunapiga hodi,
Vijana huko makazini ndio kila siku wanakuuliza ‘utastaafu lini ‘ wakikuona unakopa hata sh 100000 wanakushangaa kweli, maana wanajua una mabillion bank,
Hata ukiwaambia jamani nasomesha, wanakuuliza mpaka sasa hivi una somesha tu? Ee ulichelewa kuzaa, na anayekuuliza hivyo ana miaka 30 hata mke hana, sasa anafikiri mpaka apate mtoto wa 3 tu atakuwa na umri gani?
Mpaka mtoto wa mwisho amalize chuo,
Mimi sasa mwaka kesho mtoto wa tatu anamaliza chuo, na nitakuwa na 51 Mungu akijalia huyu wa form 4 naye amalize chuo nitakuwa na 55, sio mbaya sana
Ok
Sasa pesa ndio hiyo imepotea kwenye kuku,
Wazo lililoniijia haraka baada ya kutafakari sana ni KUPIGA BEI ILE NYUMBA,
Sasa nitamshawishi vipi mwenzangu? Ikawa sasa ni ishu.
Ukitilia maana pale ameshakaa zaidi ya miaka kumi, na ameshajenga mtandao wa kutosha na akina mama wenzake wenye nyumba na kulinga juu,
Ila sasa kabla ya yote hayo kuna mambo yalikuwa yananiudhi mimi binafsi mpaka nikawa naona wazo la kijana linapata nguvu, alikuwa anapenda sana kusifisifia nyumba za watu, kuanzia nyumba imeisha vizuri, ina garden, mala gari nzuri, ingawa hata mimi nilikuwa na gari ya kutembelea baadaye nikaipiga bei,
Mala watu wanamsema kwa kuwa yeye ni binti mdogo kwa nini anakubali kuwa nyumba ndogo, na hivyo vyote ananieleza,
Mimi nikawa namjibu wewe angalia familia yako, kama ni watoto unao, kama shule nzuri hata watoto wako wanasoma shule nzuri, wakati meingine hata kuwazidi wakwao, una as vizuri, mimi nakupenda, unakula vizuri, na hili la kula kuna hata ndugu waliolewa kabisa makanisani , wakija kumtembelea pale Ndio huwa kipindi cha kubadili mboga,
Sasa nikiona amezidi namuuliza niambie hapa wanaokusema wewe, alivyonitajia mpaka nikashangaa, mmoja mme kwa mwaka anakaa hapo nyumbani kwa wiki mbili tu, mwingine mmewe alishafariki muda mwingi yupo baa, mwingine na mume wake wapo wanauza genge la nyanya pamoja,
Watoto hata nguo za kushindia shida,
Mwingine kila siku na mumewe ugonvi, sasa namuuliza wanakuzidi nini hao mpaka uumie na maneno yao,
Nikamwambia PENDA MME NA WATOTO WAKO, hayo mengine ni mwembwe tu za hapa duniani, maisha ni wewe mwenyewe unayachukuliaje, ukiwa wanazidi waambie mimi nampenda huyu huyu.
Lakini nikaona tena yanazidi, mala mume wa mama fulani anasema wewe mbaya sana mbona umekutana naye bars Arabia hukumsalimia, nikamuuliza mbona yeye hakunisalimu, hata hivyo kama ni yule mimi nimemzidi umri yeye ndio alitakiwa anisalimie, lakini hili sio tatizo, kumbe huyo bwana kaniona njiani narudi nyumbani usiku wa 3 mimi akili yangu yote ipo nyumbani,
Nikamwambia ukionesha dalili ya kunidharau hata hao watu watatudharau,
Ila kwa ufupi, yule aliyekuwa na nyumba nzuri na garden sasa hivi yupo gerezani, yule mama mmewe wanaonana kwa mwaka wk mmewe kafariki, yule chapombe naye hatunaye, wale genge ni choka mbaya majuzi nilipita huko,
Hizo taarifa kila alipokuwa akinipa nikawa na Namuuliza umejifunza nini hapo kuhusu maisha,
Lakini haelewi kitu,
Maamuzi niliyochukuani kuuza nyumba na kama nilivyowaeleza hapo mwanzo kile kiwanja kilikuwa eneo linalolipa, kwa hiyo sikupata shida kuuza, na kwa kilikuwa kimeendelezwa sana, kuanzia nyumba kubwa iliyoishia lenta, ile nyumba ya nyumba vitatu tuliyokuwa tukiishi, pamoja na Banda kubwa la kuku, na eneo kubwa tu Kinabalu kwa ajili ya garden na parking hata ya gari ndogo 6
Baada ya yeye kukubali lakini kwa mabishanomakali ,
Tulimpata mteja wa 80M lakini kwa malipo ya 40M kila baada ya miezi 2
Hiyo ilikuwa 2016 November, na ilitakiwa baada ya miezi miwili baada ya kukamilisha malipo tuondoke, ambayo ingekuwa ni April 2017
Kwa ufupi mteja alikuwa muungwana sana,
By December malipo ya kwanza yalikamilika (40,000,000) CASH
nini kilitokea, kumbuka nilikuwa na madeni yanayokaribia mil 15M,
Hapo nyumba imeshauzwa na bado installment 1 ambayo by February lazima ilipwe na sisi tuwaachie wenye nyumba yao, maana sisi hatuna chetu tena, nikama tunarudi kwenye kile chumba kimoja,
JE WEWE KAMA BABA UTAANZA KUFANYA NINI?
Kumbuka kuna katabia fulani nilianza kukaona kwa mke wangu, hasa hasa ka kunidharau na kuwa karibu na vijamaa jamaa.
Na hata wakati mwingine kama simpigii simu anaweza kukaa hata siku nne bila kunitafuta
NGOJA NIONDOE MACHUNGU
ENDELEENI KUNIOMBEA
KaribuNimefika hapa
Ahsante ndugu yanguAisee..pole kwa unayoyapitia