Watoto wake sasa ndio wamemaliza la saba, nikawatafutia shule nzuri huko kanda...........nauli kwenda tu ukihumuisha vikorokoro vyote tokea hapa mpaka afike shule kwa mmoja sio chini ya 200000, bado ada ambayo kwa mmoja kila baada ya miezi 3 ni sh500000 na mwingine kila baada ya miezi 3 ni 450000, na wakirudi unatuma pesa kama 100000, kwa mmoja
Sio kwamba nina pesa nyingi kiasi hicho lakini waswahili wanasema maji ukishayavulia nguo huna budi kuyaoga,
Sasa umeshawaingiza huko inabidi tu waendelee na mimi meenyewe umri ndio nnasogemea, na kustaafu Ndio huko kunapiga hodi,
Vijana huko makazini ndio kila siku wanakuuliza ‘utastaafu lini ‘ wakikuona unakopa hata sh 100000 wanakushangaa kweli, maana wanajua una mabillion bank,
Hata ukiwaambia jamani nasomesha, wanakuuliza mpaka sasa hivi una somesha tu? Ee ulichelewa kuzaa, na anayekuuliza hivyo ana miaka 30 hata mke hana, sasa anafikiri mpaka apate mtoto wa 3 tu atakuwa na umri gani?
Mpaka mtoto wa mwisho amalize chuo,
Mimi sasa mwaka kesho mtoto wa tatu anamaliza chuo, na nitakuwa na 51 Mungu akijalia huyu wa form 4 naye amalize chuo nitakuwa na 55, sio mbaya sana
Ok
Sasa pesa ndio hiyo imepotea kwenye kuku,
Wazo lililoniijia haraka baada ya kutafakari sana ni KUPIGA BEI ILE NYUMBA,
Sasa nitamshawishi vipi mwenzangu? Ikawa sasa ni ishu.
Ukitilia maana pale ameshakaa zaidi ya miaka kumi, na ameshajenga mtandao wa kutosha na akina mama wenzake wenye nyumba na kulinga juu,
Ila sasa kabla ya yote hayo kuna mambo yalikuwa yananiudhi mimi binafsi mpaka nikawa naona wazo la kijana linapata nguvu, alikuwa anapenda sana kusifisifia nyumba za watu, kuanzia nyumba imeisha vizuri, ina garden, mala gari nzuri, ingawa hata mimi nilikuwa na gari ya kutembelea baadaye nikaipiga bei,
Mala watu wanamsema kwa kuwa yeye ni binti mdogo kwa nini anakubali kuwa nyumba ndogo, na hivyo vyote ananieleza,
Mimi nikawa namjibu wewe angalia familia yako, kama ni watoto unao, kama shule nzuri hata watoto wako wanasoma shule nzuri, wakati meingine hata kuwazidi wakwao, una as vizuri, mimi nakupenda, unakula vizuri, na hili la kula kuna hata ndugu waliolewa kabisa makanisani , wakija kumtembelea pale Ndio huwa kipindi cha kubadili mboga,
Sasa nikiona amezidi namuuliza niambie hapa wanaokusema wewe, alivyonitajia mpaka nikashangaa, mmoja mme kwa mwaka anakaa hapo nyumbani kwa wiki mbili tu, mwingine mmewe alishafariki muda mwingi yupo baa, mwingine na mume wake wapo wanauza genge la nyanya pamoja,
Watoto hata nguo za kushindia shida,
Mwingine kila siku na mumewe ugonvi, sasa namuuliza wanakuzidi nini hao mpaka uumie na maneno yao,
Nikamwambia PENDA MME NA WATOTO WAKO, hayo mengine ni mwembwe tu za hapa duniani, maisha ni wewe mwenyewe unayachukuliaje, ukiwa wanazidi waambie mimi nampenda huyu huyu.
Lakini nikaona tena yanazidi, mala mume wa mama fulani anasema wewe mbaya sana mbona umekutana naye bars Arabia hukumsalimia, nikamuuliza mbona yeye hakunisalimu, hata hivyo kama ni yule mimi nimemzidi umri yeye ndio alitakiwa anisalimie, lakini hili sio tatizo, kumbe huyo bwana kaniona njiani narudi nyumbani usiku wa 3 mimi akili yangu yote ipo nyumbani,
Nikamwambia ukionesha dalili ya kunidharau hata hao watu watatudharau,
Ila kwa ufupi, yule aliyekuwa na nyumba nzuri na garden sasa hivi yupo gerezani, yule mama mmewe wanaonana kwa mwaka wk mmewe kafariki, yule chapombe naye hatunaye, wale genge ni choka mbaya majuzi nilipita huko,
Hizo taarifa kila alipokuwa akinipa nikawa na Namuuliza umejifunza nini hapo kuhusu maisha,
Lakini haelewi kitu,
Maamuzi niliyochukuani kuuza nyumba na kama nilivyowaeleza hapo mwanzo kile kiwanja kilikuwa eneo linalolipa, kwa hiyo sikupata shida kuuza, na kwa kilikuwa kimeendelezwa sana, kuanzia nyumba kubwa iliyoishia lenta, ile nyumba ya nyumba vitatu tuliyokuwa tukiishi, pamoja na Banda kubwa la kuku, na eneo kubwa tu Kinabalu kwa ajili ya garden na parking hata ya gari ndogo 6
Baada ya yeye kukubali lakini kwa mabishanomakali ,
Tulimpata mteja wa 80M lakini kwa malipo ya 40M kila baada ya miezi 2
Hiyo ilikuwa 2016 November, na ilitakiwa baada ya miezi miwili baada ya kukamilisha malipo tuondoke, ambayo ingekuwa ni April 2017
Kwa ufupi mteja alikuwa muungwana sana,
By December malipo ya kwanza yalikamilika (40,000,000) CASH
nini kilitokea, kumbuka nilikuwa na madeni yanayokaribia mil 15M,
Hapo nyumba imeshauzwa na bado installment 1 ambayo by February lazima ilipwe na sisi tuwaachie wenye nyumba yao, maana sisi hatuna chetu tena, nikama tunarudi kwenye kile chumba kimoja,
JE WEWE KAMA BABA UTAANZA KUFANYA NINI?
Kumbuka kuna katabia fulani nilianza kukaona kwa mke wangu, hasa hasa ka kunidharau na kuwa karibu na vijamaa jamaa.
Na hata wakati mwingine kama simpigii simu anaweza kukaa hata siku nne bila kunitafuta
NGOJA NIONDOE MACHUNGU
ENDELEENI KUNIOMBEA