Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

INAENDELEA

Kipindi nipo nipo kikazi nje nilikuwa nikimtumia pesa ya matumizi kupitia rafiki yangu wa kazini, ambapo kila baada ya muda alikuwa akienda kuchukua pesa ya matumizi.

Na mimi kwa muda huo nirudipo likizo, nikaanza ujenzi wa nyumba kubwa zaidi hapohapo, vyumba vitati., kimoja master, common toilet, sebule kubwa kabisa ambayo mnaweza kucheza table tenis kwa nafasi, jiko, store, vibaraza viwili, cha mbele na nyuma jikoni.

Kiufupi kwa sababu nilikuwa nje kipindi na kwa wazungu huko, nyumba ilikuwa ya kisasa hasa.

Ukiongezea na eneo lenyewe na la washua sikutaka mchezo lakini vilevile kwa msukumo wa huyo mwanamama au MDADA (to be specific).

Mpaka namaliza mkataba na kurudi, nyumba ilikuwa imebaki kufunga lenta tu.

Sasa kutokana na majukumu mengine pesa ikawa kama imepungua kidogo.

Kumbuka wakati huo sio kwamba nilikuwa nimepasahau kwa bi mkubwa, hapana majukumu yalikuwa kama kawaida, watoto wanasoma na wenyewe shule za kuheshimika na ujenzi wa nyumba ya pili kubwa ukiwa unaendelea vizuri.

Kiufupi sikuwa na ubaguzi wowote, kati ya hizo familia mbili
 
Yaani wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika, kwanza hapo huenda hata hao watoto wa bi mdogo siyo wake, 😂 😂 😂 🤔 namuwazia tu mwanaume mwenzangu...
Hapana watoto ni wangu kabisa, tabia mwendo, kuzungumza, kucheka, kukasirika, ukaribu ni mimi tupu, hata watu wakiwaona, wanasema nina damu kali sana
 
INAENDELEA

Sasa ujenzi wa nyumba kubwa umesimama kipindi hicho ni 2012 au 2013 mwanzoni, nimerudi naendelea na kazi yangu hapa.

Sasa nikiangalia kamshahara kenyewe na matumizi mbambali kabisa kipindi sasa watoto ni kama wameambiana wanikomeshe na mashule yao hayo, wapo watano kwa mpigo na wengine ndio chuo, kila waki-apply mkopo wanapigwa chini, kigezo, private school, mpaka nikawa na wasiwasi labda hata hawaombi huo mkopo wenyewe.

Ila mpaka naandika hapa wala hawajuani labda wa bi mdogo ndio wanawafahamu kwa sura za kwenye picha, lakini wa bi mkubwa wala.

Nikirudi nyumba kidogo, wakati tumepanga niliwahi kuambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa nikiwa sipo huo kuna madogo fulani wanakuja pale nyumbani, wanaongea na kuondoka, tatizo ni kuwa wakati ananieleza alikuwa amekunywa na aliniambia kipindi ambacho bi mdogo kagombana na mke wake, ila alinieleza baada ya kuja chumbani kwangu na mbele ya mke wangu.

Mimi niliishia kumtazama tu, kwa kuwa nilimwamini sana bi mdogo na yeye kwa kweli ni mcheshi sana kwa kila mtu, ila ni mkali sana ukiingia kwenye anga zake.

Na isitoshe wale vijana hara mimi nikiwepo huwa wanabisha hodi na wananisalimu, wanaondoka au wanakaa nje hapo wanapiga story, sasa kwa sababu labda ya umri wangu na wao story sio za hivyo, tunaishia kucheka naondoka basi.

Hata ipo siku mke wangu aliibiwa simu chumbani akamtuhumu mmoja wao, na baada ya kuwawekea mkwara mzito kweli alirudisha.

Ki ufupi sikumtuhumu yeyote kati yao kulingana na maelezo ya mpangaji mwenzangu
 
Mkuu kusema ukweli hata kabla hujamaalizia hii story yako kwanzaa nikupe pongezi maana kwa Umri ulionao na mafanikio uliyonayo ni makubwa sana, Umefanikiwa kusomesha watoto wengi namna hiyo ni jambo la kujivunia sana.

Sasa Ushauri wangu kuhusu hao wanawake wako wawili kama kuna yoyote anakusumbua Piga chini. Ni bora kutokuwa na mke kuliko kuwa na mwanamke pasua kichwa, Itakuletea magonjwa tu kama presha. So kama kuna sgida yoyote waachie kika kitu then fanya maisha yako..
 
Kwa hapo ulipofikia na wake zako umevumilia na kuamua kuyaoga, usikate tamaa endelea kuyaoga mkuu.
 
INAENDELEA...

Baada ya ujenzi kusimama na matumizi kuwa makubwa, nikamgusia bi mdogo kuhusu kupiga bei kila kiwanja cha pili, kusema kweli kile cha pili kilikuwa kinafahamika kwa bi mkubwa, kiujumla kilikuwa cha kwake, lakini kwa sababu naye ujenzi wa nyumba yake ulikuwa umesisimama nilimshawishi mpaka akakubali tukiuze, nikimwambia mikopo kazini imebizidi kimo, kwa hiyo nusu, nimpigie plasta na mambo mengine kama umeme na maji, akakubali,

Lakini ni ukweli nilikuwa na mikopo kuanzia bank mpaka SACCOS, achilia mbali mikopo kidogo midogo ya mtaani (almaaluf ya riba ya asilimia mpaka 30 kwa mwezi na mwezi ukipita riba inaongezeka).

Ila bi mdogo ndio alinishawishi zaidi nikiuze, mpaka kwa misemo kuwa ‘kifaacho mtu chake ‘

Na kweli haikuchukua muda, kiwanja kikapata mteja, kama 20 M.

Haraka sana nikatoa kama 10m kwa ya bati za msouth, tena nikaenda kiwandani mwenyewe ambapo zilini cost kama 7.5M

Zilzobaki nikamalizia lenta. Sasa nyumba ikaonekana inasubiri bati tu.

Na bati baada ya kutoka kiwandani, moja kwa moja zikaenda kwenye banda la kuku, kuzihifadhi zikisubiri mbao tu.

Ile 10M nyingine nilimkabidhi bi mkubwa ili naye ahangaike nazo kwenye nyumba yake, huwa sitaki kujionyesha boss sana kwa mke wangu, kwa hiyo nampaga uhuru sana wa matumizi yake.
DA SASA KASHESHE LINAANZA, NGOJA KWANZA NITAFAKARI NIONE KAMA NIENDELEE AU VIPI MAANA SIPENDI KUCHAMBWA!!

ILA HII HABARI NI YA UKWELI NA USHAURI WENU MUHIMU
 
Mkuu kusema ukweli hata kabla hujamaalizia hii story yako kwanzaa nikupe pongezi maana kwa Umri ulionao na mafanikio uliyonayo ni makubwa sana, Umefanikiwa kusomesha watoto wengi namna hiyo ni jambo la kujivunia sana..
Da Ahsante sana kwa ushauri wako, na kubeba hisia zangu , pamoja na pongezi, ila kuhusu maendeleo huwa nawaza sana mambo ya mbele.

Na sitaki kuona familia yangu au zangu zinapata shida au kutokuwa na mwelekeo na mimi binafsi sio mtu wa viwanja kihivyo, ila mala moja moja hupenda kutoa familia out
 
Kwa hapo ulipofikia na wake zako umevumilia na kuamua kuyaoga, usikate tamaa endelea kuyaoga mkuu.
Kama kuyaoga ndio nayaoga sasa hivi, ila naomba tu ushauri wenu wakuu, tusichekane maana leo mimi kesho labda wewe au hata mtoto wako mwenyewe yakamkuta, sasa kupitia visa kama hivi unaweza kumpa ushauri kabla hayamkuta,
Bahati mbaya akina Mama zetu, kama sio mama yako mzazi huwa wanakucheka, au hata kukudhihaki,

Lakini wanasahau kuwa na wenyewe wana watoto wa kiume na haya yanaweza kuwakuta wakiwa bado hai
 
Kama kuyaoga ndio nayaoga sasa hivi, ila naomba tu ushauri wenu wakuu, tusichekane maana leo mimi kesho labda wewe au hata mtoto wako mwenyewe yakamkuta, sasa kupitia visa kama hivi unaweza kumpa ushauri kabla hayamkuta,
Bahati mbaya akina Mama zetu, kama sio mama yako mzazi huwa wanakucheka, au hata kukudhihaki,

Lakini wanasahau kuwa na wenyewe wana watoto wa kiume na haya yanaweza kuwakuta wakiwa bado hai

Pole mkuu, tushirikishe kilichokusibu
 
Tunasubiri umalize tukushauri kwa upendo sana
Amina ndugu yangu,
Maana kama sasa hivi nipo hai namshukuru da Mwenyezi Mungu,

Maana akina mama zetu hawa, tunawapenda sana na tunajitoa sana lakini utafikiri wakati mwingine wana wadudu kichwani,

Ukitenda wema tatizo ukiwa mbaya tatizo, sasa wanataka nini lakini?
 
Back
Top Bottom