INAENDELEA...
Mambo ya mbao na bati tuache kidogo, tutaendelea baadaye!,
Turudi nyuma kidogo kipindi nimerudi safari ile 2013, kwa bahati mbaya sana ilitokea tu nimeshika simu yake, sielewi nini kilinifanya niishike ile simu? Lakini ni Mungu tu kwa uwezo wake (hivi vitu wakati mwingine ni Mungu tu mwenye uwezo wa kukuonyesha hata ufanye mbinu gani za kutaka kujua au kuficha muda utafika Mungu atakuonyesha tu).
Basi katika kuishika ile simu nikaona Message kutoka jina (niipe jina L la mwanaume, kwa sababu ni kisa halisi nitaweka majina ya herufi)
Msg ilikuwa ina maneno kuwa ‘nilifika salama. Vipi nitakuja tena unifundishe hayo maujuzi)
Ni maneno mepesi sana, lakini ukitakuta kwa mkeo inabidi ujiulize sana, bahati mbaya mimi binafsi vitu vidogo ambavyo havieleweki kwenye simu ya mke wangu tena kutoka kwa mwanaume lazima nipate majibu.
Nilipouliza huyu ni nani? Jambo baya alilofanya ni kunipokonya simu ndio anijibu kuwa yule ni kaka fulani tulisoma naye kutoka kijijini kwao, ni mfanyabiashara wa mazao, kwa hivyo alikuja pale nyumbani kupajua na kumtembelea.
Nilipoulizia zaidi aliniambia huwa akija anamletea maharage kidogo.
Sikuona kama ni ishu kubwa, ila nilimwambia tu Naomba jenga tabia kwanza ya kuogopa majirani, maana wakiona mwanaume anakukuja hapa nyumbani kipindi ambacho mume wako hayupo utaanza kuwapa shaka, na habari zinaweza kunifikia mimi kwa njia tofauti ambayo hata kama sio mtu mbaya basi ninaweza kuwa na mashaka na wewe, nikazidi kumweleza kuwa, kama una ugeni hasahasa mwanaume panga siku ambayo mimi nipo umwambie aje ili na mimi nimfahamu.
Yakaishia hapo, maisha yakaendelea.
Lakini haikupita muda mrefu, nikaanza kupata taarifa nyingine, kuwa huyu mkeo mara nyingi anaonekana na wafanyabiashara toka huko kwao maeneo ya Kariakoo, yaani wakija wanawasiliana anaenda Kariakoo kwenye manunuzi yao halafu anarudi nyumbani muda mbaya, wakati wanakutwa kwenye baa au restaurant wanakula.
Na aliyekuwa analalamika ni mdogo wake wa kike ambaye alikuwa ameajiriwa kwenye maduka ya Kariakoo, ila aliyekuja kuniambia hiyo habari ni mume wake katika mazungumzo na mimi ya kawaida tu.
Nikaja kumuuliza, wewe mbona nasikia mara nyingi unaambatana na wanaume Kariakoo na mimi hunipi taarifa, sikukatazi kutembea lakini tupeane taarifa, wewe sasa hivi ni mke kabisa kwa sababu ndugu zako wote wanajua upo na mimi, kwa hiyo likitokea la kutokea nitaulizwa mimi.
Majibu aliyoniambia kwa kiburi tu ni KWANI WEWE NI NANI MPAKA NIWE NAKUAGA?
Mungu wangu,,!!!!
Niaendelea, ila ninaookuwa nakata stori kwamba nitaparudia tukumbushane