Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Mkuu uko sure kweli Mke mkubwa hafahamu yote haya? Nasema hivyo kwa kuwa kuna sehemu umesema una mtoto anasoma kwa mama yako,je mkeo mkubwa hana mazoea na ukweni? Hamna mtu anaweza kumpa yanayoendelea pale ukweni kama yule msamaria mwema aliyekujulisha mkeo anahamisha vitu mjini? Wanawake ni wazuri sana wa kupandikiza spies ili kupata taarifa flani flani mkuu
Kama familia haimpendi sana mke mkubwa wanaweza mficha, yaani huyu mzee jamani japo si Mzee anaweza kuwa mchumba tu[emoji23][emoji23] sijui aliishwa nini huyo mwanamke wake, kashamuona zuzu tu ndiyo maana anamfanyia hivyo, halafu ukute mke mkubwa hana hata shida masikini
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Tatizo wakizidiwa hoja wanaanza personal attacks
Yani hafu wamecremisha kila Uzi wanaanza personal attack, hawa ni wavulana tu maisha yamewashinda kwa kweli woooi
 
Nimeelewa kuwa wanaume hawana kifua cha kuhimili mikikimikiki, kidogo tu mnalainika au niseme mnajirudi.

Wanawake yamkute haya kama wewe angeshaacha kila kitu na kuondoka na ndo hivyo kafanya mwenzetu.

Jitahidi kuutuliza moyo wako ili usiuumize zaidi ukapata maradhi.
 
Wanajifariji ooh hamna mwanaume sijui nini hzo ndoa za wake wenza huwa ni machungu Sana asilimia zote sijawahi ona furaha yao angalia kina queen Darlene, kero tupu. Mbona wazazi wetu wamezeeka pamoja na watoto tuko Moja chah
Yaani mie huwa nashangaa, basi kama wakristo wasiende madhabahuni wajichukulie tu vyeti bomani, mie kwetu mpaka wazazi wanamaliza uzazi tulikuwa wengi tu, mama na Baba mmoja, kama Mzee alikuwa na makando kando huko sikuwahi sikia mpaka Mzee anapumzika, lakini hawa wasikuhizi ambao hata afya zao shida mtu mke tu wa ndani kupata haki yake hakuna, lakini anavyohangaika huko nje, kama ngiri anayekimbizwa na Chinta
 
Aisee wanawake wanatusababishia tunaishi maisha mafupi mno
Hakuna cha wanawake ni nyie wenyewe huyu Baba si anamke nyumbani, lakini anayemsumbua nani huyo kaenda kumkwaramla huko angeacha atafute Mme wake mwenyewe kwanza hajafunga naye hata ndoa , hatuombi mabaya ghafla hayupo hao watoto wa huyo binti wanaendaje kujichanganya kwa watoto wa mke mkubwa , wakati mwingine vifo vya mapema huwa mnavitafuta wenyewe
 
Kusema kweli kama sio kukomaa mpaka sasa hivi ningekuwa nmeshamwachianyumba kwa vituko alivyonifanyia,

Kinachonitia wasiwasi huyo bwana ambaye wanae, kwanza alimwoaga binamu wa mke wangu, wakaachana baada ya bwana kumfumania mke wake na bwana mwingine,

Jamaa alipiga mwanamke karibu aue, haikutoshaakamfuata mwanaume na kumchima visu na kukimbia kijiji, amerudi juzi tu, huko

Kwa hiyo jamaa ni mshari wasiwasi wasije kuunda njama wanipotezee uhai,

Ila Mungu ameendelea kuwa na mimi,

Nimeshaenda kutoa taarifa polisi,
Makubwa haya kwahiyo bidada kafuata vifu [emoji23][emoji23]
 
OMBI WAKUU NA USHAURI

hii nyumba niifanye nini, ni nyumba kubwa,
Ipo kwenye kiwanja cha eka moja,

Eneo ni ni zuri sana, sasa hivi nyumba ni nyingi, lakini ya kwangu kila mtu anaitamani,

Ila bado haijaisha,

Madilirisha nilishaweka ya aluminium bado matatu tu ya dining room
Mpange mtu uiuze kwa mlango wa nyuma ila iwe yako, nusu mpe atambaye na wanaye, tena hao watoto usije wachanganya na bimkubwa wako utaleta mbegu mbaya sana kwako
 
Huyu mwanamke simtaki tena, lakini naona kama anawapambe,

Nipeni ushauri wapendwa,
Maana ninachokiona siku moja huyu mwanamke anaweza rudimentary hapa kwa gia ya watoto
Uza lakini uinunue wewe lete mtu asiye mjua hapo
 
Hivi mzee wangu unachofosi kwa huyo bi mdogo ni nini? Kwani si una mke wako mzuri tuu nyumbani? Si muachane kwa amani tuu kila mtu ajue hamsini zake?

Unavoendelea kufosi unatafuta kuwekewa sumu ama mtakuja kupigana mgawane majengo ya serikali, mmoja aende mortuary mwingine jela.

Mzee bado hukachelewa, shtuka mzee, piga moyo konde uendelee na maisha mengine.
Yawezekana ni mrembo sana kuzidi mke wa nyumbani, si unajua unaoa ukiwa bado kapuku flani sasa ukipata pesa ndiyo unaona warembo ndiyo haya yanayomkuta mwenzenu.
 
Nimeelewa kuwa wanaume hawana kifua cha kuhimili mikikimikiki, kidogo tu mnalainika au niseme mnajirudi.

Wanawake yamkute haya kama wewe angeshaacha kila kitu na kuondoka na ndo hivyo kafanya mwenzetu.

Jitahidi kuutuliza moyo wako ili usiuumize zaidi ukapata maradhi.
Ni huyo mmoja kaamua kuacha na kutimka, kwa kwa sababu ni mwanamke mpumbavu,
Mi sijaona mwanamke mwenye akili anatimka anaacha watoto wake na maisha yake ya toka ujana,

Huyu ni malaya na bwege,

By the way, nimemfunyia nini kibaya mpaka useme wanawake yakiwashinda ni rahisi kutimua Na kuacha kila kitu,

Ukweli ni kwamba baadhi yenu huwa mpo tayari hata kuua mme ili ubaki wewe na watoto na mali,

Lakini ni nadra sana mwanaume wako kukufanyia ubaya eti sababu nina mali au nimekuchoka ndio maana tujioneaga bora tucheat,
 
Nimejifunza kitu. Michepulo sio dili. Heri mara mia machangudoa
Na changudoa atakuletea mimba nyumbani,
Kama hutaki hayo mambo acha kabisa kudeal nayo

Kwa nini uhangaike na machangu,

Na ukiacha tunajua wewe ni mwanaume suruali,

Hivi kwa akili yako unafikiri tupo hapa duniani kwa ajili ya nini ndugu,

Mimi nilishajitambua, kuwa, hapa duniani tupo kwa ajili ya vitu 3 tu,

1- KULA

2- KWENDA CHOONI

3- NGONO

basi, vingine vyoteeee ni mbwembwe tu!!!!
 
Hakuna cha wanawake ni nyie wenyewe huyu Baba si anamke nyumbani, lakini anayemsumbua nani huyo kaenda kumkwaramla huko angeacha atafute Mme wake mwenyewe kwanza hajafunga naye hata ndoa , hatuombi mabaya ghafla hayupo hao watoto wa huyo binti wanaendaje kujichanganya kwa watoto wa mke mkubwa , wakati mwingine vifo vya mapema huwa mnavitafuta wenyewe
Kwani wasipojichanga wanapungukiwa na nini?

Yaani una uhakika gani wakijichanganya ndio watakuwa na furaha
 
Yawezekana ni mrembo sana kuzidi mke wa nyumbani, si unajua unaoa ukiwa bado kapuku flani sasa ukipata pesa ndiyo unaona warembo ndiyo haya yanayomkuta mwenzenu.
Mke wangu ni mrembo sana,
Tena kusema kweli hata hiyo zamani sikujua kama ni mrembo hivi,
Ila pamoja na ezee unaomnyemelea, aiseee
Siamini kama huyu ni mke wangu!!!

Na anavyopigilia vitu, mpaka naona wivu

Kwa hiyo kusema nilioa sijui ovyo sio kweli
 
Back
Top Bottom