Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Kwani wakati Unamjengea Jina la Hati ya nyumba uliandika ya nani??? Hati ya kiwanja je??? Huyo mwanamke unaweza mfukuza hapo kama hivi vyotr vipo kwa jina lako na hamjawahi kuishi pamoja at least kwa mwaka pia ufanye mpango ukamzunguke polisi kulee hilo tuu otherwise nyumba itauzwa hiyo mgawane au wewe utaambiwa Umuache hapo aishi na mwanao na Kingine kama Umeoa huyo mwanamke hana chake kabisa hapo ila Tu ishu ni Kwa mkeo vitaumana.
So jiandae kupigania mali zako lakini kwa mkeo hizi habari kufika ni lazima.
vyote vipo kwa jina langu na sijamwoa,na mke anafahamu
 
Shida kubwa ya wanaume ni kuishi kwa kutaka kuficha ficha mambo...
Mtu unamletea mke mdogo ulimuandaa kisaikolojia kwamba utamuolea mke wa pili?.
Mapenzi una maintain ama umehamishia nyumba ndogo?

kweli Mungu hachelewi

Kaka Mwitore kaa tulia jiulize kwa nini ulihitaji/unahitaji wanawake wawili?jiulize sana
WHY?
Js because u can?
Wewe ni mwanaume una hitaji hilo?
Mkeo mkubwa hakukutosheleza?
Unawapenda wote wawili?
Ulipenda watoto wengi?

pata sababu

Kama ni genuine need ambayo Mungu kaweka moyoni mwako waeleze wote wawili..
Rasimisha...jamii ikutambue hivyo na familia nzima...
Wape uhakika wa mapenzi yako kwao...

Short of that...endelea kuomboleza
Ulitegemea mke mdogo aishi kificho miaka yote bila ndoa rasmi?

Polygamy is not for the faint hearted...
Its double trouble but on the positive side its double blessings na faraja na attention na kila kitu

issue ni mwanaume umejipanga kufurahia na kukabiliana nayo ama mnaingiaga kichwa kichwa kama huyu mtoa mada?. Hehe
naona huja ielewa mada,kama nyumba nimejenga ,watoto wamesoma academy, kuna la zaidi ya upendo huo?
 
huyu mwanamke amerudi ili kuja kutaka nyumba iuzwe , ameondoka huu ni mwezi wa tisa na si mala moja anaondoka na kuludi tumshapelekana mpaka mahakamani ameshanilaza polisi kwa mambo kusingizia, kiufupi story nzima nlishaieleza nuymba nimejenga mimi na hati au karatasi ninazo,

kwa ufupi naombeni ushauri wa namna ya kumwondoa ili niepuke mambo ya polisi,

rbya polisi nilichukua toka alipoondoka mwezi wa january,
je hiyo rb itanisaidia nikimwondoa kwa nguvu ?
 
naona huja ielewa mada,kama nyumba nimejenga ,watoto wamesoma academy, kuna la zaidi ya upendo huo?
Ujue binadamu nje ya mahitaji hayo uliyotaja,
anahitaji heshima yake kwenye jamii....
Hicho kitu ndio hujampa mke mdogo....
Ndo mana anawaya waya kutafuta mwanaume mwingine amrasimishe aitwe mke rasmi wa mtu...
 
huyu mwanamke amerudi ili kuja kutaka nyumba iuzwe , ameondoka huu ni mwezi wa tisa na si mala moja anaondoka na kuludi tumshapelekana mpaka mahakamani ameshanilaza polisi kwa mambo kusingizia, kiufupi story nzima nlishaieleza nuymba nimejenga mimi na hati au karatasi ninazo,

kwa ufupi naombeni ushauri wa namna ya kumwondoa ili niepuke mambo ya polisi,

rbya polisi nilichukua toka alipoondoka mwezi wa january,
je hiyo rb itanisaidia nikimwondoa kwa nguvu ?
Miezi 9 imetosha sana kusema mmeachana mkuu nasema Nenda kamfukukuzee beba watu wakambebee juu juu...!! Hana chake hapoo hawezi kwenda kufanya umalaya huko alafu anarudi hapo anavyotaka....
 
vyote vipo kwa jina langu na sijamwoa,na mke anafahamu
Hapo ndo unapokosea

mtu uko nae 20+ yrs ni mke na watoto wakubwa th
Hana tu cheti
Na hicho ndo kinamfanya asitulie ajiheshimu...

mke mkubwa kinachomfunga cheti tu...

usiseme hujamuoa ni mkeo huyo
Sasa mtreat kama mke aliyekosea na utafute suluhu usilete habari za sijamuoa na mahakamani sijui

ama option B muoe ya Kiserikali afu umtaliki rasmi ili upate nguvu ya kisheria kugawa mali
 
ndiomaana naomba ushauri,hivi hata kama ni mke a ndoa ndio ana haki ya kufanya chochote mradi tu anataka mgawane mali , wewe hilo unakubali, kiufupi mimi nimeshindwa tabia zake hizo ambazo nimekueleza, nimeomba ushauri tu wa namna ya kumwondoa ili kama ni mali kugawana aende mahakamani lakini akiwa hayupo nyumbani kwangu
 
Mleta mada tunaomba picha yako tafadhali!

Tangu nimeanza kukusoma sielewi kwanini huwezi kuchukua maamuzi ya kiume.
 
Ushauri wenu ni muhimu sana.

Umri wangu ni miaka 50, nimeoa mke kanisani huu ni mwaka wa 25 naishi naye na tumejaliwa watoto wanne, wa kwanza na wapili wamemaliza tayari chuo kikuu na wa tatu yupo chuo kikuu mwaka wa pili. Wa nne kamaliza kidato cha 4 mwaka jana, katikati hapo miaka 18 iliyopita bahati mbaya nikajiingiza kwenye mahusiano na binti wa miaka 20 wakati huo na akapata ujauzito, nilipomwambia nimeoa ili aitoe mimba ile na kwa kuwa bado ni binti mdogo anaweza kupata wa kumwoa, alikataa katakata. Na mimi kwa kuogopa maana alinitamkia kuwa atajiua kama nitamlazimisha kutoa mimba na kuwa yupo tayari kuishi na mimi kama mke wa pili na ujauzito ule hawezi kutoa kamwe.

Niliendelea kumshawishi atoe, matokeo yake akakimbia akaenda kwao mpaka akajifungua huko.

Lakini kiufupi zaidi, alirudi tena na kunitafuta na kunitishia kumwambia mke wangu, hivi ninavyoandika ilibidi nirudishe nyuma majeshi na kuanza kuishi naye kama mke wa pili.

Nilimpangishia chumba na maisha yakaendelea, baada ya muda alipata mtoto wa pili, wote ni wa kike, baada ya muda nilianza kuwasomesha kuanzia chekechea mpaka sasa hivi wa kwanza anafanya mtihani wa form Six mwaka huu na wa pili anafanya wa form 4 mwaka huu na wote wamesoma shule za Private toka chekechea mpaka sasa hivi na kwa wastani kila mmoja alikuwa ananigharibu 2.5m hasa shule za msingi mpaka secondary. Hapo bado michango mbalimbali na usafiri, kwa maana walikuwa wanasoma mikoani.

Baada ya kumpata mtoto wa kwanza akiwa kwenye chumba cha kupanga, niliona sina budi watoto wangu na mimi binafsi niwe na uhuru maana maisha ndio yalishaanza hivyo, na mimi upendo tayari ulishaingia na kuona ni maisha kama maisha mengine.

Ndipo nilipoamua kununua viwanja, kama unakumbuka miaka ile ya 2000 nadhani kuanzia 2006 serikali ilipima viwanja 20,000 maeneo mbalimbali ya DSM, mimi nilichukua viwanja viwili, wakati ule nakumbuka kimoja nilinua 1,800,000 na kingine 1,300,000 ml. Ukubwa ni sq m 1200 na 1000. Kimoja kikubwa nikamjengea nyumba ya mgongo wa tembo, vyumba 2 na sebule katikati na choo kizuri cha nje, nikaacha eneo kubwa tu kwa ajili ya kujipanga na kujenga nyumba kubwa baadaye, kumbuka huo ni mwaka 2007 alipohamia hapo au tulipohamia hapo.

Baadaye nimfungulia biashara ya saloon, akafanya kama miaka 2 vibaka wakaingia nakuiba kila kiatu, nikaona isiwe shida nikamfungulia mghahawa ambao ulikuwa na vitu 16 na meza nne kubwa, bado na wenyewe haukufanya kazi vizuri, nikamfungulia grocery ya bia na kuweka kila aina ya kinywaji kwa kutumia viti na meza za mghahawa.

Nayo haikufanya kazi vizuri, nikamnunulia Hiace iliyotumika tayari kama dala dala.

Na yenyewe usimamizi ukawa mgumu.

DA NITAENDELEA, MAANA DA SIPO VIZURI KABISA KIAKILI NI NIMECHANGANYIKIWA SASA HIVI.

MUENDELEZO WA TUKIO HILI SOMA HAPA CHINI:
SEHEMU YA 2

SEHEMU YA 3

SEHEMU YA 4

SEHEMU YA 5

SEHEMU YA 6

SEHEMU YA 7

SEHEMU YA 8

SEHEMU YA 9

SEHEMU YA 10

SEHEMU YA 11

SEHEMU YA 12

SEHEMU YA 13

SEHEMU YA 14

SEHEMU YA 15

SEHEMU YA 16

SEHEMU YA 17

SEHEMU YA 18

SEHEMU YA 19

SEHEMU YA 20

SEHEMU YA 21
Unapoatelekeza kichwa cha juu ukaendekeza cha chini matokeo ndiyo haya. Hivyo, jilaumu tu mwanangu au ubadilike
 
Back
Top Bottom