Naendelea tulipoachia pale, alipopata zile pesa,
Tulipo tulia kidogo, nilimuuliza kwa utaratibu sana kuwa ni biashara gani anataka kufanya?
Hakunijibu kitu, alichagua kukaa kimya,
Baadaye nikawaita watoto na kuwasimulia, kilichosababisha tugombane na mama yao,
Na nini wazo lao, je wanakubaliana na mimi au mama yao,sasa sielwe labda ni umri au mama yao tayari alishawapa matumaini ya biashara yake mpya au italipa sana.
Nikawaambia umuhimu wa kuwa na kiwanja kwanza na biashara ifate baadaye kwa kuwa huo ni mwezi December 2016 na fungu la kwanza ndio hilo tunapigana,
Mwezi wa kwanza au wa pili tunapata fungu la pili, na hapa sio kwetu tena, sisi ni wapangaji, muda ukifika mwenye nyumba anahitaji kwake,
Sikuona jibu lolote la kueleweka.
Baaday kabisa tena nikamuuliza mmama aniambie ni biashara gani anataka kufanya,
Akanijibu anahitaji biashara ya kupeleka nguo mikoani,
Mimi nikamjibu hiyo biashara mimi sitaiafiki,
Na sababu ninazo.
NATUMA HII KWANZA ISIJE IKAPOTEE NA YENYEWE HALAFU NAENDELEA