Wakati bado kijana, nlishawahi ku twist mguu wangu, sasa wakati sina hasira najua namna ya kuutembelea na kukimbia kidzain fulani hivi,
Sasa kumbe wakati ule nakimbia nilijisahau nikautwist na kuangukavibaya, niliendelea kukaa pale chini, kwa muda huku nataka kunyanyuka nashindwa, baadaye nikajivuta na matako mpaka kwenye kiti, kusema kweli hata kwenye kiti sikuweza kukaa,
Nikaaa pale chini baada ya muda, ndio akaja yule mwanamke na watoto wakaninyanyua na kunikalisha kwenye kiti,
Watoto wakachemsha maji na kunikanda kwa chumvi, kusema kweli siku nilikuwa naenda kwa bi mkubwa, lakini sikuweza,
Lakini nilimpa taarifa kuna msiba umetokea ofisini kwetu na huyo ni mtu wangu wa karibu.
Kesho yake maumivu bado yalikuwa makubwa nikajijikokota mpaka CCBRT, picha ikaonyeshwa kitu kinaitwa sijui LIGAMENT, ndio imepata madhara madhara,
Ile pesa kusema kweli yule Mwanamke aliikatalia
NI BUASHARA GANI ANATAKA KUFANYA?
Nitaendelea