Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Yaani nimwachie nyumba kweli? Nikiwa hai naona anafaidi nyumba yangu na wanaume wengine!?

Kweli? Hapana hapo sasa mnataka ndio mniue,
Kabisa au mimi niue mtu, sipo tayari kumwachia nyumba yangu, labda kama mimi ndio ningeonyesha simtaki, ningemwachianyumba ili apunguze machungu, lakini yeye anifanyie vituko vyote hivyo halafu nimwachie nyumba, hapana,
Fanya hivi uza nyumba halafu kila mtu akajenge upya anapopataka.na kama amekuzidi nguvu gawaneni kati kwa kati baada ya mauzo.
Watoto waamue wakae na wewe kwa bi mkubwa au mama yao.au kihostel hostel hata baada ya kumaliza masomo yao.
 
Bado unampenda mmnooo tena sana si rahisi km unavyodhani kumtema.Unamchukia kwa kua unampenda

Sent using Jamii Forums mobile app
Ray,
Kipindi cha nyuma alikuwa akiondoka nilikuwa mpaka naumwa, sio message hizo sio simu hizo, mpaka ananizimia simu,
Lakini mimi nipo tu,
Toka alivyoondoka ile mwezi wa nne mwaka jana sikuwahi kumpigia simu wala message, hata kumuulizia tu kwa watoto na ndugu zake sikuwahi,
Alirudi mwenyewe,

Safari hii kaondoka ana mwezi, sijampigia simu wala msg,

Nasema tena, nitaendelea kmkumbuka na kumuwaza, huwezi kuishi a mtu miaka 20 usimuwaze, hapo itakuwa uongo

Ila kwangu tena Hapana, ndio maana namwomba mungu aendlee kuwa huko ili nizidi kumsahau
 
afu mwitore kaficha tu.
ukwel n kwamba kwa mke mkubwa alipakimbia hakanyag kabsa huko.

kumbukeni kuna siku alituambia,ngoja aingie jikoni kwanza,ina maana anaishi peke yake kwenye hyo nyumba wakat huu ambapo watoto wako shule
Hsta mimi nimehisi hivyo kwakweli..anakwepa sana kila swali analoulizwa kuhusu bi mkubwa...ni dhahiri hawako katika good terms ndio maana aliweza kuwekeza muda na mali kwa bi mdogo..hakuna mwanamke mwenye akili timamu asiyajue mahusiano ya nje ya mume kwa miaka yote hiyo
 
afu mwitore kaficha tu.
ukwel n kwamba kwa mke mkubwa alipakimbia hakanyag kabsa huko.

kumbukeni kuna siku alituambia,ngoja aingie jikoni kwanza,ina maana anaishi peke yake kwenye hyo nyumba wakat huu ambapo watoto wako shule
Hata mimi naona huyu mzee alitelekeza bi mkubwa baada ya pesa kuchanganya na penzi la bi mdogi kuwa zito akakimbia.

Kwa sasa kinachomtesa ni kumkosa bi mdogo sababu hana tena hela na kule nyumba kubwa alishaharibu.

Angekuwa yuko poa na bimkubwa kusingekuwa na mateso haya nayopitia mpk kumfuatilia bi mdogo yupo mkoani anaenda.
Ila mkuu pole sana rudi kwa bi mkubwa kamuombe msamaha na hiyo nyumba umpe atakupokea.
 
Ray,
Kipindi cha nyuma alikuwa akiondoka nilikuwa mpaka naumwa, sio message hizo sio simu hizo, mpaka ananizimia simu,
Lakini mimi nipo tu,
Toka alivyoondoka ile mwezi wa nne mwaka jana sikuwahi kumpigia simu wala message, hata kumuulizia tu kwa watoto na ndugu zake sikuwahi,
Alirudi mwenyewe,

Safari hii kaondoka ana mwezi, sijampigia simu wala msg,

Nasema tena, nitaendelea kmkumbuka na kumuwaza, huwezi kuishi a mtu miaka 20 usimuwaze, hapo itakuwa uongo

Ila kwangu tena Hapana, ndio maana namwomba mungu aendlee kuwa huko ili nizidi kumsahau
Ndugu yangu unakwepa sana suala la bi mkubwa.
1. Je anafahamu kua una mtu nje
2. Je mko katika hali gani kwa wakati huu
 
afu mwitore kaficha tu.
ukwel n kwamba kwa mke mkubwa alipakimbia hakanyag kabsa huko.

kumbukeni kuna siku alituambia,ngoja aingie jikoni kwanza,ina maana anaishi peke yake kwenye hyo nyumba wakat huu ambapo watoto wako shule
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]daah hiyo siku naikumbuka hahahah mkuu una kumbu kumbu mno
 
Bila Shaka huyu 'Mke mdogo' ni wa kutoka Morogoro (lakini sio Mlugulu au Mkutu) au Kanda ya ziwa - Mara
Atakuwa Mkaguru au Msagara au Mpogolo?? 😂 😂 😂

Wote tu watu wa Morogoro, lazima wakuchezeshe ngoma, wakuneme!
Watani zangu waluguru ausindile, anogaah!

Everyday is Saturday................................😎
 
Nyie Wote hapa mnapiga kelele tu,huyu mzee wetu amelogwa sio amelogwa ila kapikwa na kaiva.
Dawa yake kumkamata kinguvu afungwe kamba na kumpeleka kwa mwamposa au mganga.
Hii sio akili ya kawaida,marufuku kuoa mwanamke masikini,acha masikini waoane wenyewe kwa wenyewe'ukioa masikini utalishwa kila Haina ya uchafu
Kwa Mwamposa akagalagazwe kwenye mafuta tena wayapashe moto kidogo yawe ya uvuguvugu!

Everyday is Saturday................................😎
 
Naomba ukamweleze mkeo tafadhali achana na hiki kirambasi. You are too innocent jamani kupitia haya yote.
Yaani kwa heshima niliyonayo kwa mke wangu na upendo Anaonionyesha, ni nguvu tu za Roho mtakatifu ndio zitaniongoza nimtamkie hilo neno, Mimi mwenyewe kama binadamu, naona siwezi
 
Ila nlichokigundua we jamaa una ufala fulani, mtu ni mchepuko, viwanja ulinunua wewe ili umpe hifadhi saivi unahangaika sjui mpelekane ustawi mara unamuogopa jamaa anayemkaza mchepuko wako, mara una bond na watoto lakini mkizinguana na mchepuko nao waja juu eti toka kwetu khaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] afu unaogopa mchepu adi unaenda polisi
Hii stori kuna mambo yamefichwa, kwanza upande wa bi mkubwa hatujaambiwa ukweli
Pili yawezekana huyo sio mchepuko
Angekuwa mchepuko wachungaji wangefuata nini kusuluhisha?
Kama ni mchepuko mama mzazi wa mleta mada angefikaje kwa uhuru nyumbani hapo?

Unapotaka ushauri eleza jambo kwa uhalisia wake maana watu watakushauri kwa kile ulichoeleza, ukidanganya utashauriwa kwa kitu ambacho hakipo na ushauri hautasaidia
 
Mwitore ni muongo! Alimpata huyo mchepuko akiwa na miaka 20, wameishi miaka 18 na sasa ana miaka 42. Hapo piga hesabu angalikuwa na miaka 38. Pili fumanizi zote tangu watoto wanamwambia rudi kwenu, yupo tu. Tatu analala kwa bi mdogo bila bi Mkubwa kusituka miaka yote 18. Huyo ni mke au jini. Hii story ya kubumba akina Shunie cariha Espy angalieni anawachota
Nakubali
 
Ila nlichokigundua we jamaa una ufala fulani, mtu ni mchepuko, viwanja ulinunua wewe ili umpe hifadhi saivi unahangaika sjui mpelekane ustawi mara unamuogopa jamaa anayemkaza mchepuko wako, mara una bond na watoto lakini mkizinguana na mchepuko nao waja juu eti toka kwetu khaaa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 afu unaogopa mchepu adi unaenda polisi
Kama ulisha invest kule kama mimi nilivyoinvest ingukuwa wewe ungefanyaje?
Halafu kumbuka serikali ipo na sheria zipo!
 
Ila nlichokigundua we jamaa una ufala fulani, mtu ni mchepuko, viwanja ulinunua wewe ili umpe hifadhi saivi unahangaika sjui mpelekane ustawi mara unamuogopa jamaa anayemkaza mchepuko wako, mara una bond na watoto lakini mkizinguana na mchepuko nao waja juu eti toka kwetu khaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] afu unaogopa mchepu adi unaenda polisi
Umechelewa kugundua mkuu, huyu mzee ajui hajielewi.
 
Mzee wangu kwanza naomba nikutukane kidogo ila samahani kwa hilo tusi..

WEWE NI LIJINGA SANA TENA DHAIFU( tayari nimekutukana samahani lakini)

Hivi hao watoto ni wako? kweli kabisa wanakutamkia maneno mabaya mpaka watoto wako?

Kama haujastafu nakuomba mafao yako uyafaidi wenyewe.

Hiyo nyumba waachie watoto kama urithi then wewe baada ya kupata mafao yako ni rudi kwa mke mkubwa au tafuta sehemu nyingine ununue nyumba, uvute mkoko maisha yaendelee

Unaonekana ni mtu wa huruma sana na huyo mwanamke ameshajua udhaifu wako, anza kuwa mbabe na kwanza hata siku akirudi kwako usimruhusu hata akupigie goti najua muda sio mrefu ataharibikiwa.

Kama huwezi kuwapa watoto hiyo nyumba kama urithi ni bora ufanye kama anavyotaka kuwa mgawane bcoz baada ya hapo hatokuwa na kigezo cha kukusumbua tena kama mali mmeshagawana.

NB: angalia hata pension yako usije ukaipoteza kwa huyo mwanamke na ukaja kuwa chizi, najua ukivuta mafao yako huyo mwanamke atakuja analia kuwa umsamehe na ukikubali kusamehe umeisha hayo mafao yatapotea bcoz anajua udhaifu wako...

Nyongeza nenda kawapime DNA hao watoto maana wanavyokufanyia naona kama wana baba yako mwingine..

KUPANGA NI KUCHAGUA

1. mafao yapotee Au
2. Ufaidi mafao yako

Mwisho: Vipi mke mkubwa mna maelewano?
 
Ndugu Ahsante sana kwa mawazo na na ushauri,
Kuhusu hapo namba 1
Mama yangu hakunitaka niwe Na mchepuko,
Ila kipindi hicho nilikuwa bado kijana sana na ndio nimepata mtoto wa kwanza,

Alitaka tu kunifunza kama mzazi namna nzuri ya mtoto wa kiume kuishi,
Maana aliona kila nikitoka kazini break ya kwanza ni home
Sasa kwa uzoefu wake wa maisha aliona sio sawa
Ni bora nikitoka kazini niwe kwanza na vijana wenzangu huko kubadilishana mawazo

Kama umegundua hii tabia yangu moja kwa moja nyumbani labda Ndio imenifikisha hapa kutawaliwa na mke, maana mawazo mengi ya kihuni au namna ya kumnyanyasa mwanamke nilikuwa sina ( yaani ile roho mbaya ya kiume)

Namba mbili 2 hapo,
Mimi ni mpiganaji wa kutaka kumiliki mali
Ndio maana Alhamdulilah maisha yangu na uwekezajinimejitosheleza hilo sina wasiwasi nalo

Nikisema leo hapa Dar niuze Mali zangu zote leo nirudi kijijini, uhakika wa 700 m upo, na malipo

Nikiendeleza maaneo yangu angalau niongeze kama vyumba 30 vya wapangaji
Naiona 1 B, inaninyemelea,
Kwa hiyo uwezo wa kuachia mali yangu kumpa mtu ambaye kaniumiza NO tena nasema kwa sauti NO, nitaenda mpaka kushtakia kwa Mungu,
Maana mali yangu ninauhakika sijamdhulumu mtu yeyote,
Ni damu na nguvu yangu.
Hapo mwanzo nilisema kama huyu mtu asingeonyesha namna yoyote ya kutaka kuizungumzia nyumba hasa hasa wakati wa ugonvi,
Na kukawa na mwelekeo wa kuachana kwa roho yangu ilivyo ningemuachia nyumba,
Ila mpaka nimegundua ana mwanaume bado kweli nimwachie nyumba au tugawane nusu kwa nusu Hapana, big Hapana

Mwaka 2018, yalipozidi kuwa magumu na kunilaza polisi, kesho yake alikuwa kunitoa yeye na ndugu zake 3 dada zake wawili na Baba yake wa hiari wahapa Dar, ambaye kusema kwa kw a miaka yote niliyoishi na huyu mwanamke sijawahi hata kusikia akimzungumzia

Baada ya kinitoa, alishauliwa asilale nyumbani kwangu mpaka nitulie maana ninaweza kumfanyia kitu mbaya,
Sasa wakati tunaagana yule baba akashauri tufanye kitu kama kikao nyumbani kwangu kesho yake,

Tukaagana na mimi nikaridhia nikaona sasa ni muda mzuri wa kutoa yamoyoni yote mbele ya ndugu zake na huyo baba

Wakati mimi nimefika nyumbani, nikampigia yule mdogo wake kwa ajili ya matayalisho ya chakula kwa wageni kesho,

Sasa ile anapokea simu, nilitumia namba yasimu nyingine ambayo hakuwa nayo, ile ya kwanza ilivunjika kioo pale Polisi na ni Iphone na ya kazini kwangu!
Kusema kweli nilipishwa hiyo sh 700000

Ok sasa wakati anapokea ile simu kumbe kulikuwa na mjadara unaendelea pale yeye na mke wangu,

Nilimsikia mke wangu kwa sauti kubwa ile ya kupandisha hasa, akisema

MIMI NIMESHASEMA ILE NYUMBA NI YA KWANGU, YEYE AENDE ZAKE HUKO,.

Baadaye akanyamaza nadhani mdogo wake alimwambia ni mimi nipo kwenye simu,

Nikamuuliza mpaka namsikia huyo mtu anaropoka hivyo.
Yule dada akanyamaza, na mimi si kuendelea kumuuliza, nikampa maagizo ya kesho tu

Sasa ona kweli huyo mtu ni wa kumpa senti tano yangu.?
Kesho yake kwenye kikao yule mzee na wadogo zangu watatu wa kiume na dada zake 2 na majirani 5 na mjumbe, baada ya maelezo yangu marefu kusema kweli kila mtu alishika mdomo,

Lakini wale wadogo zangu watatu hawakuvumilia, walinyanyuka kwa hasira na kumkimbilia yule mwanamke na kutaka kumpiga watu wakaingilia pale na mimi kwa hasira niwaambia waache yule ni mke wangu,

Wakanielewa wakaacha lakini walilia sana,
Wakatoka nje huku wanalia na kusema, hatukujua kama kaka yetu unasumbuka hivi na huyu mwanamke,
Kaka ambaye umetusomesha umetutunza wote

Mbona mama...... ( bi mkubwa) hakuwa hivi, I I ingekuwa ni huyu kweli sisi tungefika hapa?

Mmoja tena akakurupuka kwenda kutaka kumpiga nikamkatalia, ni kikao kikaishia hapo,

Wakati namsindikiza yule baba aliniambia neno moja tu, KUWA MWANAUME!!!
Ukashindwa kuwa mwanaume??🤔🤔
Daah! Ulipenda mpaka kero, hiyo ni dhambi. Kila kitu ni kwa kiasi

Everyday is Saturday................................😎
 
Ray,
Kipindi cha nyuma alikuwa akiondoka nilikuwa mpaka naumwa, sio message hizo sio simu hizo, mpaka ananizimia simu,
Lakini mimi nipo tu,
Toka alivyoondoka ile mwezi wa nne mwaka jana sikuwahi kumpigia simu wala message, hata kumuulizia tu kwa watoto na ndugu zake sikuwahi,
Alirudi mwenyewe,

Safari hii kaondoka ana mwezi, sijampigia simu wala msg,

Nasema tena, nitaendelea kmkumbuka na kumuwaza, huwezi kuishi a mtu miaka 20 usimuwaze, hapo itakuwa uongo

Ila kwangu tena Hapana, ndio maana namwomba mungu aendlee kuwa huko ili nizidi kumsahau
Kweli mie nimekuelewa na nikweli unavyo simulia, ila madhaifu yako yafanyie kazi:

1.Usipende mwana mke kupitiliza hatakama umezaa nae

2.Never ever trust a woman hata kama umekanae miaka 20.

3.Umezidisha kutumia logic na common sense kwa mkeo some Time ujinga na ubabe ni suluhisho kwa wana wake.

Usimuachie nyumba wala usiiuze acha tu hiyo ni mali yako labda akuue.
4. Anza maisha mengine (move on) upya wewe bado mdogo at 50yrs tafuta mke mgine ila usimjengea wala usimuonyeshe mali zako panga umueleza una mke lazima alijue hilo.
5. Watoto wako wasimamie wakileta dharau achana nao watajirudi wenyewe
6. Acha kusimulia watu wanao kujua visa vyako wanakuenjoye tu. Pambana kama mwana umme we only live once here usiogope mahakama au usitawi it will buy time for you to settle huwezi kufungwa kwa civil suite
 
Back
Top Bottom