Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Uza nyumba we mzee mbona mzito hivyo

Yaani unasubiri mpaka mgawane?

Dah Mungu aliumba
Connection aliyonayo na mchepuko ni hiyo nyumba, akiiuza, anajua ndiyo kampoteza mchepuko kimoja, hatomuona tena! Na hatamani hili litokee, thin line between love & hate!

Wala watoto hawajawaunganisha, kilichowaunganisha ni hela na nyumba.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Ahaahhahahaahahahhaahhaah
Kukarangiza, mbona kama alisema aliishia kuunguza [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Anakaa kule nyumba ndogo hakuna kelele, pia anashinda na boxer tu, haingizi mwanamke, majirani wanamshangaa![emoji23]
Utunzi wa mahaba niue, uniponde kama nyanya, kumbe wengine wanayaishi,

JF imejua kunipa burudani!!

Everyday is Saturday................................[emoji41]
 
Bimdogo ndo nani? Bimdogo ama mchepuko? Mbona Heaven Sent nimeaona anamuulizia mke na si mchepuko. Wewe ndo hujaelewa mada. Ameuliza analia nini angali mke yuko na anadai wanabond vizuri..
Exactly nilimuuliza mke halali. Maana sielewi una mke na mpo vizuri ila unaishi kwa stress kisa mtu mwingine asiyekutaka
 
Mzee wangu kwanza naomba nikutukane kidogo ila samahani kwa hilo tusi..

WEWE NI LIJINGA SANA TENA DHAIFU( tayari nimekutukana samahani lakini)

Hivi hao watoto ni wako? kweli kabisa wanakutamkia maneno mabaya mpaka watoto wako?

Kama haujastafu nakuomba mafao yako uyafaidi wenyewe.

Hiyo nyumba waachie watoto kama urithi then wewe baada ya kupata mafao yako ni rudi kwa mke mkubwa au tafuta sehemu nyingine ununue nyumba, uvute mkoko maisha yaendelee

Unaonekana ni mtu wa huruma sana na huyo mwanamke ameshajua udhaifu wako, anza kuwa mbabe na kwanza hata siku akirudi kwako usimruhusu hata akupigie goti najua muda sio mrefu ataharibikiwa.


Kama huwezi kuwapa watoto hiyo nyumba kama urithi ni bora ufanye kama anavyotaka kuwa mgawane bcoz baada ya hapo hatokuwa na kigezo cha kukusumbua tena kama mali mmeshagawana.


NB: angalia hata pension yako usije ukaipoteza kwa huyo mwanamke na ukaja kuwa chizi, najua ukivuta mafao yako huyo mwanamke atakuja analia kuwa umsamehe na ukikubali kusamehe umeisha hayo mafao yatapotea bcoz anajua udhaifu wako...

Nyongeza nenda kawapime DNA hao watoto maana wanavyokufanyia naona kama wana baba yako mwingine..

KUPANGA NI KUCHAGUA

1. mafao yapotee Au
2. Ufaidi mafao yako


Mwisho: Vipi mke mkubwa mna maelewano?
Siku ambayo hao watoto wangenitamkia hivyo mimi haijalishi ni wangu au sio wangu wangepata adhabu inayokwenda sambamba na mama yao na kutokea hapo ningewatuma wakatafute baba yao
 
Hakuna heshima wala upendo kwa bi mkubwa kadanganye wengine

Usingeteseka hovyo namna hii
Wenye upendo, heshima au hekima na wake zao, wana michepuko, ila hawana ulimbukeni huo wa mapenzi,

Hutosikia anapigana na mchepuko, au wanatoana ngeo, au wamepelekana polisi sijui ustawi wa jamii au wanashinda kutwa kujaza watu wa mtaa wakigombana,
Hiyo nyumba wangeiacha wangesonga mbele, hakuna mwenye busara anayejijua ana mali za 500M na atapokea pension 250M, atakubali ajidhalilishe katika mazingira hayo.
Especially kama watoto wa mke mkubwa wapo tiyari vizuri, NEVER!
Ni zaidi ya kurogwa!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Nimesoma story yako karibia kila kipengele ila Kuna maelezo sijaelewa vzr
Picha linaanzia Dar means maisha yenu yote ni Dsm!!
Watoto wanakua umri wa kwenda shule unawatafutia shule nje ya dar ambayo nauli inagharimu karibia 200k kwa wote wawili, means muda mwingi hawapo nyumbani siku ile unataka kumpiga mama yao watoto nao wanakushikia mawe wanakuambia uende kwenu let's say walikua likizo
Wasiwasi wangu unaanzia hapa[emoji116][emoji116][emoji116]

Graduation; sijui Ni ya kumaliza darasa la 7 au form 4 muda huo huyo mchepuko wako hakuepo nyumbani anakuja dar bila kufika nyumbani kwako mnaenda kwenye graduation unamsalimia anauchuna unataka kuongea nae anagoma muda wa kulishwa keki unataka kulishwa na mwanao unagoma swali je watoto walihamia Dar au shule ilikua nje ya dsm ila graduation ilifanyikia dsm (chai).
Swali lingine penye utata je watoto hawako Tena boarding school make Kuna mmoja Yuko Kwa mama yako anasomea huko japo hapataki

Anyway story yako ni nzuri inafunza lakini maswali ya sintofahamu ni mengi kuliko kawaida natamani niseme Ni chai lakini members wa Jf watanimeza jumlajumla!!!
Pengine hiki Ni kisa kilikutokea lakini Kuna mambo umeongeza mpk umepoteza content nzima.

Jamiiforums; we dare to talk openly.[emoji38][emoji38][emoji38]

cc: Mwitore

Sehem nyengne alieka vipande vidogo dogo sana nafkir hukupitia humo mimi nimeelewa vizuri
 
Kipo kitu kimejificha hapa miaka 18 sio rahic sisi wanawake ucgundue tabia ya mume nakusiwe na ugomv wowote Yani wiki tu tayar umejua kua ana mchepuko me nafkiria hapa nyumba kubwa alijua kuhusu nyumba ndogo na mke mkubwa akagombana na mume na hapo mume akahamishia makazi nyumba ndogo
Mi hapo ndo nabaki na maswali inawezekanaje yani
 
Mkuu rudia kusoma huyu bwana sasa hivi yupo kwa mke mkubwa toka yule kimeo wake aondoke kwaiyo hichi kisa anasimulia akiwa kwa mke wake halali
Sio kweli kuna mahali anasema watoto wake mpaka sasa wamemtumia 120000 tu lakini mkewe anasikia tu mara nguo mpya mara nini
 
Yaan halina kitu kabisa kichwani.. ndo maana unaambiwa chagua marafiki bora. Hivi umewahigi kuona show off za mtu ambaye hana shule?[emoji23]
Mzee ni empty set huyu jinsi alivochezea bahati ya maisha huyu na mchepuko wake standard seven wamekutana akili sawa
 
Ndugu Ahsante sana kwa mawazo na na ushauri,
Kuhusu hapo namba 1
Mama yangu hakunitaka niwe Na mchepuko,
Ila kipindi hicho nilikuwa bado kijana sana na ndio nimepata mtoto wa kwanza,

Alitaka tu kunifunza kama mzazi namna nzuri ya mtoto wa kiume kuishi,
Maana aliona kila nikitoka kazini break ya kwanza ni home
Sasa kwa uzoefu wake wa maisha aliona sio sawa
Ni bora nikitoka kazini niwe kwanza na vijana wenzangu huko kubadilishana mawazo

Kama umegundua hii tabia yangu moja kwa moja nyumbani labda Ndio imenifikisha hapa kutawaliwa na mke, maana mawazo mengi ya kihuni au namna ya kumnyanyasa mwanamke nilikuwa sina ( yaani ile roho mbaya ya kiume)

Namba mbili 2 hapo,
Mimi ni mpiganaji wa kutaka kumiliki mali
Ndio maana Alhamdulilah maisha yangu na uwekezajinimejitosheleza hilo sina wasiwasi nalo

Nikisema leo hapa Dar niuze Mali zangu zote leo nirudi kijijini, uhakika wa 700 m upo, na malipo

Nikiendeleza maaneo yangu angalau niongeze kama vyumba 30 vya wapangaji
Naiona 1 B, inaninyemelea,
Kwa hiyo uwezo wa kuachia mali yangu kumpa mtu ambaye kaniumiza NO tena nasema kwa sauti NO, nitaenda mpaka kushtakia kwa Mungu,
Maana mali yangu ninauhakika sijamdhulumu mtu yeyote,
Ni damu na nguvu yangu.
Hapo mwanzo nilisema kama huyu mtu asingeonyesha namna yoyote ya kutaka kuizungumzia nyumba hasa hasa wakati wa ugonvi,
Na kukawa na mwelekeo wa kuachana kwa roho yangu ilivyo ningemuachia nyumba,
Ila mpaka nimegundua ana mwanaume bado kweli nimwachie nyumba au tugawane nusu kwa nusu Hapana, big Hapana

Mwaka 2018, yalipozidi kuwa magumu na kunilaza polisi, kesho yake alikuwa kunitoa yeye na ndugu zake 3 dada zake wawili na Baba yake wa hiari wahapa Dar, ambaye kusema kwa kw a miaka yote niliyoishi na huyu mwanamke sijawahi hata kusikia akimzungumzia

Baada ya kinitoa, alishauliwa asilale nyumbani kwangu mpaka nitulie maana ninaweza kumfanyia kitu mbaya,
Sasa wakati tunaagana yule baba akashauri tufanye kitu kama kikao nyumbani kwangu kesho yake,

Tukaagana na mimi nikaridhia nikaona sasa ni muda mzuri wa kutoa yamoyoni yote mbele ya ndugu zake na huyo baba

Wakati mimi nimefika nyumbani, nikampigia yule mdogo wake kwa ajili ya matayalisho ya chakula kwa wageni kesho,

Sasa ile anapokea simu, nilitumia namba yasimu nyingine ambayo hakuwa nayo, ile ya kwanza ilivunjika kioo pale Polisi na ni Iphone na ya kazini kwangu!
Kusema kweli nilipishwa hiyo sh 700000

Ok sasa wakati anapokea ile simu kumbe kulikuwa na mjadara unaendelea pale yeye na mke wangu,

Nilimsikia mke wangu kwa sauti kubwa ile ya kupandisha hasa, akisema

MIMI NIMESHASEMA ILE NYUMBA NI YA KWANGU, YEYE AENDE ZAKE HUKO,.

Baadaye akanyamaza nadhani mdogo wake alimwambia ni mimi nipo kwenye simu,

Nikamuuliza mpaka namsikia huyo mtu anaropoka hivyo.
Yule dada akanyamaza, na mimi si kuendelea kumuuliza, nikampa maagizo ya kesho tu

Sasa ona kweli huyo mtu ni wa kumpa senti tano yangu.?
Kesho yake kwenye kikao yule mzee na wadogo zangu watatu wa kiume na dada zake 2 na majirani 5 na mjumbe, baada ya maelezo yangu marefu kusema kweli kila mtu alishika mdomo,

Lakini wale wadogo zangu watatu hawakuvumilia, walinyanyuka kwa hasira na kumkimbilia yule mwanamke na kutaka kumpiga watu wakaingilia pale na mimi kwa hasira niwaambia waache yule ni mke wangu,

Wakanielewa wakaacha lakini walilia sana,
Wakatoka nje huku wanalia na kusema, hatukujua kama kaka yetu unasumbuka hivi na huyu mwanamke,
Kaka ambaye umetusomesha umetutunza wote

Mbona mama...... ( bi mkubwa) hakuwa hivi, I I ingekuwa ni huyu kweli sisi tungefika hapa?

Mmoja tena akakurupuka kwenda kutaka kumpiga nikamkatalia, ni kikao kikaishia hapo,

Wakati namsindikiza yule baba aliniambia neno moja tu, KUWA MWANAUME!!!

Ile nyumba nani ana hati na zina majina ya watoto bado na viwanja vya hapo karibu kumaliza mzozo wa nani ana mwenye nyumba bac ataipiga bei yeye nyumba hiyo urudi hakuna chako au ataiombea mkopo bank ibaki na deni aondoke na pesa yeyote atakayopata hana hasara yeye baada ya hapo nyumba itapigwa mnada
 
Kuna mahali uligusia kuna mchepuko umeamua mpaka kunpangia chumba unajilia zako vyako alimaliza form four sijui mchepuko namba 2. Nakushauri usiongeze matatizo

Halafu wewe soma vizuri uzi wote acha kusumbua watu. Unaonekana mmbea mmbea mtu wa kudandia dandia vitu. Sijui unasoma kuanzia huku chini,katikati,yani hueleweki.
 
afu mwitore kaficha tu.
ukwel n kwamba kwa mke mkubwa alipakimbia hakanyag kabsa huko.

kumbukeni kuna siku alituambia,ngoja aingie jikoni kwanza,ina maana anaishi peke yake kwenye hyo nyumba wakat huu ambapo watoto wako shule
Huu ni ukweli kabisa. Kuna uwezekano mkubwa wakawa walishatengana na mke mkubwa.
 
Poa,
Mimi baba yangu mdogo ana wake wanne na watoto zaidi ya 38, lakini leo anafanya vibarua vya kulimia watu, wanawake wakubwa wapo kwa watoto zao, na alikuwa ana ng’ombe za kutosha, wote wameisha kwa kusomesha watoto na mambo mbalimbali ya kufanilia. Na amekumbia kijiji kabisa kutokana na chuki za wake zake.

Wanaume ni ukweli mtakatifu , anza kuandaa future yako wewe mwenyewe,
[emoji33][emoji33][emoji33][emoji33]
 
Fanya hivi uza nyumba halafu kila mtu akajenge upya anapopataka.na kama amekuzidi nguvu gawaneni kati kwa kati baada ya mauzo.
Watoto waamue wakae na wewe kwa bi mkubwa au mama yao.au kihostel hostel hata baada ya kumaliza masomo yao.

Huyo mwanamke hajachangia kitu kwenye hiyo nyumba hivo hajamzidi kitu Yani ni mapenz tu pesa za ujenzi zote ni nguvu ya baba[emoji16]
 
Ila Mzee kwenye hii scenario umeplay sana victim... hujaeleza mambo kinaga ubaga. Hujasema ukweli wako kabisa ili tulishauri vyema.
Sasa ndo naelewa kwanini wanao wamekupa 120,000/= despite the fact kwamba umewasomesha ingawa kwa mimi ningeendelea kukuhudumia kama baba. Familia yako waliona unafuja hela kwa huyo mchepuko maana ndo hadhi yake hata sasa. Usaliti kwa familia ni somo lenye gharama sana. Tunakuomba kama ni kurudi kwa mkeo upime kwanza Afya maana uliishi na mgawaji hakika.

Kumbe mkeo alishajua kila kitu kama ambavyo tulikueleza huko nyuma ila wewe hukuweka wazi ukafanya kama hajui kitu kabisa na ukaplay kwamba ulikua msafi sana. Yaan kiujumla tulikueleza kwamba kuna vitu unaficha. Tuogope sana na utuheshimu wanawake. Wewe unaona leo wenzako tunaona wiki 2 zijazo. Yaani ukisema kitu tunaweza kujua hapohapo kama umedanganya ama umesema ukweli. Hii karama Mungu amejua kutujalia sana. Tunaweza tukuitikie "ndio" lakini mioyoni mwetu tunasema hili lijinga kweli.

Unapotaka ushauri ili upone nafsi yako lazima uwe mkweli na muwazi ili ushairi utakaopewa uwe halali na uende kuponya nafsi yako moja kwa moja. Usitake wewe kuonewa huruma ili kuhalalisha makando kando yako.

Kwa maana hiyo... uligombana na mkeo. Kumkomoa ukaenda kwa huyu malaya na limbukeni aka dogodogo... ukala maisha sana. Na inaonekana ulimuoa kimila. Ulipomuoa si ulipaswa rasmi kwenda kudai ama kutoa talaka serikalini kwaajili ya ndoa ya mkeo ya kanisani kabla ya huyo mchepuko?

Tujifunze... kutofautiana kidogo isiwe sababu ya kwenda kuchukua hawara.
Kwasisi wakristu ndoa ni moja tena Takatifu sana. Tuangalie namna nyingine ili tuepuke migogoro isiyo ta kilazima kama hii. Nachohofia endapo mulipotofautiana na mkeo uliongea maneno ya dhihaka na jeuri sana enzi hizo na chombo kipya juu tena kibichi. Na ndoa ukute iliingia mgogoro baada ya kuwa na huyu malaya baada ya mke kujua. Nilitaka nishangae mke vipi asijue lolote. Ningemwona zuzu.

Uzee ndo huwa fainali. Utaota moto uliookota nao kuni. Maradhi huwa mengi.
Nakushauri onana na washauri wa Afya wakusaidie maana hii ni depression inakuja. Pain changes people.

Next time uwe muwazi. Usiandike kitu kikubebe kuhurumiwa. Achana na huyo malaya. Samahani kwa maneno makali maana ndo hadhi yake.
Lakini unanichamba bure kabisa, tena kwa kuziamini hisia zako,
Umekasirika sana kwa kitu ambacho sio kweli kabisa

1,mimi sikuwahi kumuacha mke wangu hata kidogo,
2. Mimi sijawahi kugombana na mke wangu kiasi hata cha kukataliana tendo la ndoa
3.haya amekuja kuyajua kwa uhakika zaidi watoto wakiwa form na std 7
4 ukiangalia miaka hiyo ndio kipindi nimeanza kusumbuliwa huko nje,kwa hiyo ndio upendo ulizidi sana kwa bi mkubwa
5. Watoto kunitumia hiyo laki, kwanza huwa najiuliza wanitumie zaidi ili nifanyie nini
Mimi nina pesa yangu, viwanja natoka na mama, na anachangia kununua kinywaji ingawa mimi sio mywaji sana, bia mbili tu chali,

Najua wanamtumia mama yao, na uzuri wakati mwingine akitumiwa ananiambia,

Na akisha tumiwa nitaona nguo mpya hapo
Na mwenyewe anafurahi na mimi natafurahi kumwona mke wangu kapendeza na anakuwa kijana zaidi

Sijawahi kununua boxer wala fulana za ndani, vyote nashtukia zipo kabatini, na zile za zamani anatupa, tena wakati nakasirika anatupa zikiwa bado nzuri kabisa

Kiujumla hajawahi nichukia wala sijawahi mchukia
Turudi kwa watoto kutonitumia pesa, walishaona sizishobokei pesa zao, kwa sababu hawajui wanitumie kiasi gani ili nilizika, mimi nina pesa yangu ya kunitosha
Lakini wakati mwingine wadogo wanawapiga mizinga huko, unaona tu dogo karudi nyumbani na shati jipya , hapo si wanakuwa wamesaidia,

Mimi ninachohitaji kwao ni usafiri tu, na wameshaniahidi kunako majaliwa kama hawajajenga wanisuprise na usafiri,

Kwa hayo machache kuwa na amani tu
 
Back
Top Bottom